Kutokwa na uchafu ukeni mara nyingi huwa ni tukio la kawaida kabisa. Hata hivyo huwa kuna aina mbalimbali za uchafu ambazo zinaweza kuonyesha maambukizi. Uchafu usiokuwa wa kawaida unaweza kuwa wa kijani au njano na wenye harufu mbaya. Uchafu usio wa kawaida mara nyingi husababishwa na fangasi ama maambukizi ya bakteria.
James Herbal Clinic tunakusahauri kuwa, uonapo uchafu wenye muonekano usio wa kawaida au wenye harufu mbaya, yafaa kumuona daktari haraka sana kwa ajili ya vipimo.
Aina Za Uchafu Utokao Ukeni
Zipo aina mbalimbali za uchafu unaotoka ukeni. Aina hizi hutofautiana katika rangi na muonekano. Baadhi ya uchafu unaotoka huwa wa kawaida, lakini mwingine unaweza kuonyesha hali ya utando ambao unahitaji matibabu.
1. Uchafu Mweupe
Uchafu ulio mweupe kidogo, hasa unaotoka mwanzoni ama mwishoni mwa mzunguko wako wa hedhi huwa ni wa kawaida. Hata hivyo, ikiwa uchafu utaambatana na muwasho na una ute kama maziwa ya mgano, huu sio wa kawaida na unahitaji matibabu. Aina hii ya uchafu yaweza kuwa dalili za maambuki ya fangasi.
Unaweza ukauona hapo uchafu huo unavyokuwa
2. Uchafu Mwepesi Wa Majimaji
Uchafu mwepesi wa majimaji hakika huwa ni wa kawaida na unaweza ukaonekana muda wowote ndani ya mwezi. Unaweza kuwa mzito wakati mwingine kutokana na mazoezi au kazi nzito.
Unaweza ukauona jinsi unavyokuwa uchafu wa majimaji, lakini pia unaweza ukaona kwenye nguo ya ndani jinsi unavyokuwa, angalia kwenye picha hapo chini.
Angali pia jinsi unavyokuwa kwenye nguo ya ndani
3. Uchafu Mweupe Wenye Wenye Kuvutika
Uchafu unapokuwa mweupe lakini wenye utando na wenye muonekano kama makamasi kamasi, kama ute wa yai, ni ishara ya kwamba uko katika hali ya siku za hatari. Hii huwa ni aina ya kawaida ya uchafu utokao ukeni.
Unaweza ukaona hapo juu jinsi ute huo unavyokuwa hasa unapokuwa katika siku za hatari.
4. Uchafu Wenye Rangi Ya Kahawia Au Wenye Damu
Uchafu wa kahawia au wenye damu mara nyingi huwa wa kawaida, hasa unapoonekana baada ya kutoka hedhini. Uchafu unachelewa kutoka baada ya hedhi unaweza kuonekana wa kahawia badala ya kuwa na rangi nyekundu. Unaweza pia ukaona kiwango kidogo cha uchafu wenye damu katikati ya mwezi, ambao huwa kama matone ya damu. Kama matone ya damu yanatokea katika kipindi cha kawaida na umekuwa ukifanya tendo la ndoa na mumeo bila kutumia kinga, basi hii inaweza kuwa dalili ya ujauzito. Kutokwa na matone ya damu wakati hali ya awali ya ujauzito yaweza kuwa ishara ya kuporomoka kwa mimba, hivyo yafaa kumuona daktari mapema sana hospitali.
NUKUU: Kwa upande mwingine, uchafu unaotoka wenye rangi ya njano au damu unaweza kuwa ishara ya tatizo la salatani ya shingo ya kizazi. Ndio maana wanawake wanashauriwa kupata vipimo vya salatani ya shingo ya kizazi kila mwezi.
5. Uchafu Wa Njano Au Kijani
Uchafu wa njano au wa kijani hasa unapokuwa na mabonge ama ulioambatana na harufu mbaya, huwa sio wa kawaida. Aina ya uchafu huu yaweza kuwa dalili za maambukizi ya ugonjwa wa malengelenge(trichomoniasis), ambao kwa kawaida husambaa ama kuenea kwa njia ya kujamiiana ama ngono.
Unaweza ukauona hapo juu kwenye tishu jinsi unavyokuwa uchafu huo, lakini unaweza kuuona kwenye nguo ya ndani jinsi unavyokuwa kama unavyoona kwenye picha hapo chini.
Ona pia kwenye nguo ya ndani jinsi uchafu huo unavyokuwa
Je, Nini Humfanya Mwanamke Kutokwa Na Uchafu Ukeni?
Uchafu wa kawaida utokao ukeni hutokana na utendaji kazi wa mwili wenye afya, na ndio huwa njia pekee ya mwili kujisafisha na kuulinda uke. Ni jambo la kawaida uchafu kuongezeka kutoka kutokana na mazoezi, kazi nzito, nyege ama hisia za kimapenzi, na msongo wa mawazo.
Uchafu usio wa kawaida utokao ukeni mara nyingi husababishwa na maambukizi, nayo huwa kama ifuatavyo;
1. Bakteria Ukeni
Hali hii hutokana na maambukizi ya bakteria, nayo huwa ya kawaida. Maambukizi haya husababisha muongezeko wa kutokwa na uchafu ambao huwa una harufu mbaya, na wakati mwingine unakuwa kama shombo la samaki, ingawa huwa haunyeshi dalili yoyote.
Unaweza ukaona hapo jinsi uchafu huo unavyoweza kuonekana.
Wanawake wanaokuwa na wapenzi wawili au watatu mara nyingi wakuwa katika hatari ya kupatwa na maambukizi.
2. Ugonjwa Wa Malengelenge
Hii ni aina nyingine ya maambukizi, lakini protozoa ndio husababisha ugonjwa huu. Maambukizi haya mara nyingi huenezwa kwa njia ya kujamiiana, lakini pia unaweza kunezwa kwa kuchangia taulo ama brashi ya kuogea. Dalili za ugonjwa huu huonekana katika uchafu wenye rangi ya njano au kijani ambao huwa una harufu mbaya. Pia huwa kuna dalili za maumivu, uvimbe sehemu za mashavu ya uke kwa ndani ama nje, muwasho, nk, ingawa wengine huwa hawaonyeshi dalili zozote.
3. Maambukizi Ya Fangasi Ukeni
Maambukizi ya fangasi ukeni hutoa dalili za uchafu mweupe, wenye utando kama maziwa mgando pamoja na muwasho na hali kama ya kuungua moto. Hali ya kuwepo kwa fangasi ukeni huwa ni ya kawaida, lakini ukuaji wake unaweza kuongezeka na kushindikana kwa hali fulani. Mambo yafuatayo hapo chini yanaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya fangasi ukeni:
· Msongo wa mawazo
· Kisukari
· Vidonge vya mpango wa uzazi
· Ujauzito
· Madawa ya vidonge ikiwa yanatumiwa zaidi ya miaka 10
4. Kisonono Na Pangusa(Chlamydia)
Kisonono na pangusa ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu usio kuwa wa kawaida, ambao mara nyingi huwa wenye rangi ya njano, kijani au kijivu.
5. Magonjwa Ya Maambukizi Katika Via Vya Uzazi(PID)
Maambukizi katika via vya uzazi nayo pia hunea kwa njia ya kujamiiana. Huonekana wakati bakteria wanapoenea kwenye uke hadi kwenye viungo vya uzazi. Maambukizi haya yanaweza kumfanya mwanamke kutokwa na uchafu mzito, wenye harufu mbaya.
6. Salatani Ya Shingo Ya Kizazi
Maambukizi haya ambayo huenea kwa njia ya ngono, yanaweza kusababisha tatizo la salatani ya shingo ya kizazi. Ingawa kunaweza kusiwepo na dalili zozote, lakini aina hii ya salatani inaweza kutoa damu, uchafu wa kahawia au majimaji yenye harufu mbaya. Salatani ya shingo ya kizazi inaweza kuzuiwa kwa urahisi kabisa baada ya kupima maambukizi ya Human Papillomavirus.
Ushauri
Unapoona dalili zozote za kutokwa na uchafu usiokuwa wa kawaida pamoja na dalili zingine kama vile homa, maumivu ya tumbo la chini, kupungua kwa uzito wa mwili, uchovu, au kukojoa mara kwa mara, basi yafaa ufike hospitali umuone daktari haraka iwezekanavyo.
Je, unahitaji huduma kutoka James Herbal Clinic? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626.
Karibuni sana!