Fahamu Madhara Ya Ugonjwa Wa PID

Je, Madhara Ya PID Isipotibiwa Yanakuwaje?

Madhara kutokana na maambukizi ya PID ambayo hayajatibiwa yanaweza kuchukua miaka mingi kuendelea. Matokeo ya tatizo hili yanaweza kuwa yenye maumivu makali. Yanaweza pia kusababisha uharibifu wa kudumu katika viungo vya uzazi. NUKUU: Madhara yanaweza kusababisha hali ya ugumba. Mwanamke anapokaa muda mrefu na ugonjwa bila kutibiwa, ndipo nafasi kubwa ya matatizo ya ugonjwa huu hutokea kwa baadaye, nayo huwa kama haya yafuatayo:

  1. Uvimbe Maji

Mfumo kinga wa mwili hutengeneza usaha katika eneo la tishu iliyoambukizwa kwenye mirija ya uzazi au vifuko vya mayai. Hali hii inaitwa jipu. Uvimbe unaonekana kutungika muda mfupi baada ya maambukizi ya PID kuanza. Unaweza kuwa wenye maumivu sana, na unaweza ukachukua miezi kadhaa ili uweze kupona wenyewe. Endapo kama hautatibiwa, basi unaweza kusababisha uharibifu wa kudumu na maumivu kwa ujumla.

  1. Makovu Na Muunganiko

Maambukizi husababisha mirija na vifuko vya mayai kuvimba. Kama tishu iliyovimba hupona taratibu, basi ndipo kovu hujengeka. Mirija ya uzazi, vifuko vya mayai, mfuko wa uzazi, au viungo vingine vinaweza kuunganika pamoja kwa muunganiko wa tishu za makovu.

NUKUU: Hali hii huitwa mshikamano. Kovu na mshikamano vinaweza kuwa vyenye maumivu makali na vinaweza kuvifanya viungo vya uzazi visiweze kufanya kazi vizuri.

  1. Mirija Ya Uzazi Kuziba

Mirija ya uzazi inaweza kuziba kutokana na jipu, makovu kwenye tishu, au muunganiko wa tishu zenye makovu. Hali ya kuziba kwa mirija ya uzazi huzifanya mbegu za mwanaume kushindwa kulifikia yai ili kulirutbisha. Nyuzinyuzi zinazokuwa kwenye mirija ya uzazi pia huharibika. NUKUU: Tishu zilizoharibika haziwezi kusaidia mbegu na yai kuweza kusafiri kwenye mirija ya uzazi. Matatizo yote haya mawili hufanya kuwa vigumu sana mwanamke kupata ujauzito.

  1. Mimba Kutunga Nje Ya Uzazi

Mimba kutunga nje ya kizazi hutokea wakati uharibifu wa mrija wa uzazi unapolizuia yai lililorutubishwa lisiweze kusafiri kwenye mrija mpaka kwenye mfuko wa uzazi(uterus). Badala yake, kiinitete huanza kukua ndani ya mrija wa uzazi. Kumbuka mrija wa uzazi hauwezi kutanuka kama unavyokuwa mfuko wa uzazi. Wakati kiinitete kinapofikia ukubwa Fulani, basi mrija unaweza kupasuka. Hali hii inaweza kuwa ya kutisha kwa mama na ni hatari pia kwa kiumbe kinachokuwa tumboni.

  1. Kama Maambukizi Yakienea

Maambukizi ya PID yanaweza kusambaa katika maeneo mengine ya mwili. Bakteria wanaweza kutoka kwenye mirija ya uzazi na kuambukiza tumbo la chakula. Hali hii huitwa, “Peritonitis”. Karibu na viungo kama vile utumbo mpana pamoja na kibofu cha mkojo, vinaweza kushikamana pamoja kwa makovu ya tishu. Hali hii inaweza kusababisha maumivu na hivyo kuvifanya viungo visiweze kufanya kazi kwa usahihi.

Ni mara chache sana maambukizi ya PID yanaweza pia kuingia kwenye mfumo wa damu. Maambukizi haya ya damu yanaweza kuwa mabaya na tena hatari.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James & Ferdinand Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili kwa urahisi kabisa. Unaweza pia ukatuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Je, Unahitaji Huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *