Fahamu Dalili Za Ugonjwa Wa Kisonono Kwa Mwanaume Na Mwanamke

Je, Kisonono Ni Nini?

Huu ni ugonjwa mbaya wa maambukizi ya bakteria, nao huambukizwa kwa njia ya kujamiiana kupitia shahawa au majimaji ya kwenye uke ikiwa kama mmoja kati ya wapenzi wawili ana maambukizi na mwenzi wake hajatumia kinga, yaani mume na mke hawajatumia kinga.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Nusu ya wanawake na 1/10 ya wanaume wenye ugonjwa wa kisonono huwa hawaonyeshi dalili zozote hata kidogo. Dalili anazozipata mwanamke ni kutokwa na uchafu ukeni, kukojoa mara kwa mara, Maumivu au hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa, na anapokojoa pindi anapokuwa hedhini.

70+ Black Woman Stomach Pain Stock Illustrations, Royalty-Free Vector Graphics & Clip Art - iStock | Refuse bread, Prescription, Irritable bowel syndrome

NUKUU: Samahani wapendwa wanagroup najua hapa ni mahali pa masomo ya kujifunza, uonapo picha kama hiyo ujue hatuna maana nyingine mbaya, bali tunaelimishana kabisa. Weka simu yako mbali na watoto tafadhali.

Kumbuka wanaume hupatwa na Maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa uchafu kwenye uume.   

Je, Dalili Za Kisonono Kwa Wanawake Zinakuwaje?

  • Tatizo hili linapojitokeza linaweza kuchukua siku kadhaa ili mwanamke aweze kulitambua. Kwa kawaida wanawake dalili huwa kama ifuatavyo:
  • Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu mbaya ambao unaweza kuwa mwepesi na wenye majimaji na wenye rangi ya njano au ukijani.
  • Muwasho au kutokwa na uchafu sehemu ya njia ya haja kubwa,
  • Kutokwa na hedhi isiyo ya kawaida
  • Maumivu makali ya nyonga au kuhisi hali ya kuwaka moto hasa wakati wa kukojoa
  • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu na wakati mwingine huambatana na kichefuchefu

Je, Dalili Za Kisonono Kwa Wanaume Zinakuwaje?

Dalili za maambukizi ya ugonjwa wa kisono huwa sio nyingi sana kwa upande wa wanaume, nazo huwa kama hivi ifuatavyo;

  • Kuvimba kwa korodani au tezi dume
  • Muwasho sehemu za njia ya haja kubwa ama kutokwa na uchafu sehemu ya njia ya hajakubwa
  • Kuwasha kwa ndani sehemu za mirija ya mkojo na Maumivu ama kuwaka moto wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na uchafu mweupe au wa kijani mwembamba sehemu ya ncha ya uume

Je, Nini Madhara Ya Kisonono?

Maambukizi ya kisonono yanaweza kusambaa kupitia mkondo wa damu na kuenea maeneo mengine  ya mwili na kusababisha madhara na matatizo yafuatayo;

  • Kupata ujauzito nje ya uzazi
  • Kuziba kwa mirija ya uzazi
  • Ugumba/utasa
  • Maumivu makali ya nyonga ya muda mrefu 

a). Kwa wanaume husababisha;

  • Uvimbe kwenye korodani wenye maumivu makali ambao unaweza kusababisha ugumba katika maisha yake ya ndoa kutokana na kushindwa kuzarisha mbegu au shahawa.

Je, Nini Madhara Ya Kisonono?

Maambukizi ya kisonono yanaweza kusambaa kupitia mkondo wa damu na kuenea maeneo mengine  ya mwili na kusababisha madhara na matatizo yafuatayo;

b).  Kwa wanawake husababisha:

  • Kupata ujauzito nje ya uzazi
  • Kuziba kwa mirija ya uzazi
  • Ugumba
  • Maumivu makali ya nyonga ya muda mrefu

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James & Ferdinand Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili bila bila kujirudiarudia. Waweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Je, unahitaji huduma? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *