Epuka Sana Ulaji Wa Nyama Ili Usipate Magonjwa
Faida za kiafya na maisha ya Kanisa la Waadventista Wasabato zimefuatiliwa hadi jinsi wanavyoishi na kula. Tangu miaka ya 1800, Waadventista Wasabato wametekeleza siri nane za afya ambazo hupunguza hatari yao ya ugonjwa wa moyo na saratani … sababu mbili kuu za kifo cha mapema. Kwa kuwaweka pembeni wauaji hawa wawili, Waadventista Wasabato wanafurahia afya njema na maisha marefu kuliko idadi ya watu kwa ujumla….Uthibitisho wa kisayansi umepatikana tu katika miaka ya hivi karibuni, kwa hivyo walijuaje kabla ya wanasayansi? Kutoka kwa mwanamke anayeitwa Ellen G. White. Mwonaji huyu alisema Mungu hakutaka watu wateseke na magonjwa na kifo kisicho cha lazima na Alimwongoza ili awaambie watu jinsi wanavyoweza kufurahia afya njema kabisa. Ellen G. White aliandika kwa urahisi na usahihi wa ajabu kile ambacho tangu wakati huo kimethibitishwa kuwa fomula bora zaidi ya afya na maisha marefu.
Wanyama wanazidi kuwa wagonjwa, na haitachukua muda mrefu mpaka chakula cha wanyama kitakapokuwa na watu wengi nje ya Waadventista Wasabato. Vyakula vyenye afya na kudumisha maisha vinapaswa kutayarishwa, ili wanaume na wanawake wasihitaji kula nyama.— Testimonies for the Church 7:124, 1902 CD 384.3
Ni lini wale wanaoijua kweli watachukua msimamo wao upande wa kanuni zilizo sawa kwa wakati na umilele? Ni lini watakuwa waaminifu kwa kanuni za matengenezo ya afya? Ni lini watajifunza kuwa ni hatari kutumia vyakula vya nyama? Nimeagizwa kusema kwamba ikiwa kula nyama ilikuwa ni salama, basi kwa sasa sio salama.—Manuscript 133, 1902 CD 384.4
Nuru niliyopewa ni kwamba muda si mrefu tutalazimika kuacha kutumia chakula chochote cha wanyama. Hata maziwa italazimika kuachwa kabisa. Ugonjwa unaongezeka kwa kasi. Laana ya Mungu iko juu ya nchi, kwa sababu mwanadamu ameilaani. Tabia na mazoea ya wanadamu yameifanya dunia iwe katika hali hiyo kiasi kwamba baadhi ya vyakula vingine zaidi ya vyakula vya nyama lazima vitumiwe katika familia za wanadamu badala ya nyama. Hatuhitaji chakula cha nyama hata kidogo. Mungu anaweza kutupatia vitu vingine.— Australasian Union Conference Record, Julai 28, 1899 CD 384.5
Kama ungejua asili ya nyama unayokula, au ungewaona wanyama wanapokuwa hai ambao nyama huchukuliwa wakiwa wamekufa, bila shaka ungebadirika na kuchukia nyama. Wanyama walewale ambao nyama zao unakula, mara kwa mara huwa ni wagonjwa kiasi kwamba, kama wakiachwa peke yao, watakufa wenyewe; lakini wakati pumzi ya uhai imo ndani yao, wanachinjwa na kupelekwa masokoni. Unaingiza moja kwa moja kwenye mfumo wako wa mwili na sumu ya aina mbaya zaidi, na bado hutambui hilo.—Testimonies for the Church 2:404, 405, 1870 CD 385.1
Mateso ya Wanyama na Madhara Yake
Mara nyingi wanyama hupelekwa sokoni na kuuzwa kwa ajili ya chakula, wanapokuwa wagonjwa kiasi kwamba wamiliki wao huogopa kuwatunza kwa muda mrefu. Na baadhi ya michakato ya kuwanenepesha mifugo kwa ajili ya soko hutengeneza magonjwa. Ukiwa umewafungia mbali na mwanga na hewa safi, huku wakivuta hewa chafu ya kwenye zizi, au kuwanenepesha kwa kutumia chakula kilichooza, mwili mzima huchafuliwa na vitu vichafu. CD 385.2
Wanyama mara nyingi husafirishwa umbali mrefu kuelekea sokoni na kupata mateso makubwa katika mchakato wa kulifikia soko. Waacha marisho ya kijani kibichi, na kusafiri kwa maili nyingi na hata kupata uchovu wenye barabara zenye joto, na vumbi, na msongamano kwenye magari machafu, yenye homa na uchovu, mara nyingi hukaa masaa mengi bila kupewa chakula na maji, viumbe hao maskini huburuzwa kwa ukali hadi kuelekea kwenye kifo chao cha kuchinjwa, ili tu wanadamu wa wakashereekee katika kuila mizoga yao.— The Ministry of Healing, 314, 385 CD.
Watu wengi wanakufa kwa ugonjwa unaosababishwa kabisa na ulaji wa nyama; bado ulimwengu hauonekani kuwa wenye hekima zaidi. Wanyama mara nyingi huuawa ambao wamesafirishwa umbali mrefu kwa ajili ya kuchinjwa. Damu yao huchemka na kuwa ya moto. Wamejaa nyama, na wanapungukiwa mazoezi ya kiafya, na wanapotaka kusafiri kwenda mbali, wanaishiwa nguvu na kuchoka, na katika hali hiyo wanachinjwa kwa ajili ya soko. Damu yao huvimba sana, na wale wanaokula nyama zao, hula sumu. Baadhi hawaathiriwi haraka sana, huku wengine wakishambuliwa na maumivu makali, na kufa kutokana na homa, kipindupindu, au magonjwa mengine yasiyojulikana. CD 385.4
Wanyama wengi sana wanaouzwa kwenye soko la jiji wanafahamika kuwa na magonjwa yaliyosababsihwa na wale walio wauza, na wale wanaowanunua sio kila wakati hawajui jambo hilo. Hasa katika miji mikubwa hii inafanywa kwa kiwango kikubwa, na walaji nyama hawajui kwamba wanakula wanyama wagonjwa. CD 386.1
Baadhi ya wanyama wanaoletwa machinjioni wanaonekana kutambua kile kinachoenda kufanyika, na wanakasirika, na kuwa vichaa kabisa. Wanachinjwa wakiwa katika hali hiyo, na nyama zao zinatayarishwa kwa ajili ya soko. Nyama yao ni sumu, na inasababisha vichomi tumboni, degedege, mishipa midogo ya damu kwenye ubongo kupasuka au kiharusi, na kifo cha ghafla. Hata hivyo sababu ya mateso haya yote hayachangiwi na nyama. CD 386.2
Baadhi ya wanyama hutendewa unyama wanapopelekwa machinjioni. Wanateswa kabisa, na baada ya kuvumilia masaa mengi ya mateso makali, wanauawa kwa kuchinjwa. Nguruwe hutayarishwa kwa ajili ya soko hata wakati ugonjwa unapokuwa juu yao, na nyama yao yenye sumu hueneza magonjwa ya kuambukiza, na vifo vingi hufuata.— Spiritual Gifts 4a:147, 148, 1864 CD 386.3
Matokeo Ya Kimwili Ya Mlo Wa Nyama Huongeza Dhima Ya Ugonjwa Na Kifo Cha Ghafla
Dhima ya kupata magonjwa huongezeka mara kumi kwa kula nyama.— Testimonies for the Church 2:64, 1868 CD 386.4
Madaktari wa kilimwengu hawawezi kutoa hesabu kwa ajili ya ongezeko la haraka la magonjwa katika familia ya kibinadamu. Lakini tunajua kwamba mateso mengi hayo husababishwa na kula nyama iliyokufa.—Letter 83, 1901 CD 386.5
Wanyama wana magonjwa, na kwa kula nyama zao, tunapanda mbegu za ugonjwa kwenye tishu na kwenye damu zetu wenyewe. Kisha panapoonekana mabadiliko katika miili yetu, haya huonekana kwa busara zaidi; pia tunapokabiliwa na magonjwa ya mlipuko na magonjwa ya kuambukiza, mfumo hauko katika hali ya kupinga ugonjwa huo.—Dondoo kutoka kwa Ushuhuda Usiochapishwa Kuhusu Flesh Foods, 8, 1896. CD 386.6
Una ulaji wa nyama, lakini sio kitu zuri. Uko katika hatari kubwa kwa kiasi hiki cha nyama. Ikiwa kila mmoja wenu atafikia kutumia kiasi kidogo cha lishe, ambayo itapunguza kwako paundi ishirini na tano au thelathini ya uzito wako wote, mngepata ugonjwa kwa kiasi kidogo zaidi. Ulaji wa vyakula vya nyama umefanya duni ubora wa damu na mwili. Mifumo yenu iko katika hali ya kuvimba, iko tayari kupata magonjwa na kifo cha ghafla kwasababu hamna nguvu za afya ya kushindana na kupinga magonjwa. Utafika wakati nguvu na afya mliyosifu mnayo vitaonekana kuwa uchafu.— Testimonies for the Church 2:61, 1868 CD 387.1
Rafiki Mpendwa,
Mungu akubariki sana unapojifunza na kusoma makala hii, na nikukaribishe kwa maswali na maoni yako.
Ni mimi Dr. Samson,
Kutoka James Herbal Clinic,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!