Bakteria mwenye umbo la kujikunja kunja ambaye kitaalam anaitwa Treponema pallidum anaweza kuvamia kila pembe ya mwili wako.
Kila maradhi ya kaswende, dalili zake, ishara zake pamoja na madhara yake ya muda mrefu, kuwa huwa ni ya pekee sana. Kaswende inaweza kuharibu kila aina ya tishu na kila kiungo ndani ya mwili wako, kwahiyo orodha ya ya madhara yanaweza kutokea yaliyosababishwa na ugonjwa wa kaswende huendelea kwa muda mrefu.
Orodha ya madhara ya ugonjwa wa kaswende ni pamoja na maradhi ya mwili na ubongo pia.
Mwanzoni kabisa mwa maambukizi, vimelea huvamia mfumo wa mkondo wa damu pamoja limfu. Hali hii inaweza kutokea hata kabla ya kidonda(chancre) cha awali.
NUKUU: Mfumo wa limfu(lymphatic system) ni tishu pamoja na viungo ambavyo huzarisha, huhifadhi na kubeba chembe hai nyeupe za damu ambazo hupambana na maambukizi pamoja na magonjwa mengine. Mfumo huu ni pamoja na sifongo za mifupa, bandama, mishipa ya limfu, tezi ya thymus, nk(ni mtandao wenye mirija myembamba ambayo hubeba chembe hai nyeupe za damu pamoja na uteute unaokuwa kwenye mishipa ya damu).
Kimelea hiki kisichoonekana kwa macho chenye umbo la kujikunjakunja kinaweza kuenea katika kila kona ya mwili wako. Hushambulia moyo, mifupa, pamoja na njia ya umeng’enyaji chakula.
Kinaweza kushambulia sehemu zako za masikio, macho, na viungo vyako vyote vikuu. Kinaweza kuvamia ini, na ngozi. Ni kimelea ambacho huenda kila mahali. Kwa mwanamke mjamzito, bakteria huyu aina ya Treponema pallidum hupita kwenye kondo ili kumuambukiza mtoto.
Pale bakteria anapoambukiza mfumo kati wa neva, ubongo pamoja na uti wa mgongo huitwa, “Neurosyphilis.” Ki historia neurosyphilis ni moja ya aina ya kaswende inayoogopeka. Inaweza ikasababisha upofu wa macho, mwili kupooza, wenda wazimu, na hata kifo.
Je, Nguvu Ya Maambukizi Ya Muda Mrefu Inakuwaje?
Bakteria Treponema pallidum wasiotibiwa hukaa mwilini bila kujulikana. Watu wenye maambukizi ya kaswende hubaki kuwa wameambukizwa kwa muda mrefu kama hawajatumia antibiotic.
Matibabu yanayofanyika mapema kwa kutumia antibiotic yanaweza kuzuia madhara makubwa. Lakini kama matibabu yako yataanza baada ya tishu au viungo vyako kuwa vimeharibika, basi antibiotic haziwezi kuondoa uharibifu huo uliofanyika.
NUKUU: Uwezo wa bakteria kuenea mwilini mwako mwote huipatia kaswende nguvu ya kusababisha mabadiriko ya madhara ya muda mrefu, lakini sio tu katika hatua zake za hivi karibuni.
Je, Ugonjwa Huu Mgumu Wenye Hatua Nyingi Unakuwaje?
Kaswende inahusisha hatua nne tofauti, lakini wakati mwingine hatua hufanana au hata kutokea kwa wakati mmoja. Sio kila hatua itajenga dalili zenye kuonekana, na dalili hazionekani kwa mpangilio ule ule kwa kila mmoja.
Jambo la msingi la kujua juu ya kaswende ni kwamba bila matibabu, kaswende inakaa, na humfanya mtu kuwa mwenye maambukizi na inaweza kufanya madhara makubwa. Ni lazima upate dawa zenye uwezo wa kuponya maambukizi kaswende na kuzuia muendelezo wake kupitia hatua zake mbalimbali.
Huu hapa ndio mzunguko wa hatua za kaswende, kwa dalili za kawaida na nguvu za madhara kwa kila hatua:
1. Hatua Ya Awali
Hapo awali kwenye maambukizi huwa kuna kidonda kisichokuwa na maumivu, nacho hujitokeza mahali popote ambapo bakteria aliweza kuingia mwilini mwako. Kidonda kinaweza kisionekane au kikajificha ndani ya kinywa chako, uke wako, mlango wa kizazi, njia ya haja kubwa au mahali popote. Vidonda hivi vya mwanzo mara nyingi hupona vyenyewe ndani ya mwezi mmoja au miwili.
2. Hatua Ya Pili Ya Kaswende(Second Syphilis):
Hatua hii hutokea wiki 4-10 baada ya mtu kupata kaswende ya awali. Dalili ya aina hiyo ya kaswende huwa ni pamoja na uchovu, kuumwa kichwa, homa, kunyofoka nywele, vidonda vya koo, kuvimba kwa matezi mwili mzima, Maumivu ya mifupa au kupungua uzito.
NUKUU: Kaswende ya aina hii huwa inakuwepo kwa wiki kadhaa na hupotea bila hata kupata tiba kwa mtu aliye athirika. Pia inaweza kujirudiarudia katika kipindi cha mwaka mmoja na mtu huingia kwenye kundi la hatua ya ugonjwa wa kaswende iliyojificha(Latent Syphilis)
3. Kaswende Iliyojificha(Latent Syphilis):
Aina hii ya kaswende hujulikana kama kaswende ambayo inaweza kuthibitika tu kwa kutumia vipimo vya maabara(serological test). Nayo imegawanyika katika makundi mawili; (1). Kaswende iliyojicha ya awali(early latent syphilis) ambayo hutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya mwathirika kuona kaswende aina ya pili(secondary syphilis) kama nilivyoeleza hapo juu mwanzo.
NUKUU: Kaswende ya aina hii huwa inakuwepo kwa wiki kadhaa na hupotea bila hata kupata tiba kwa mtu aliye athirika. Pia inaweza kujirudiarudia katika kipindi cha mwaka mmoja na mtu huingia kwenye kundi la hatua ya ugonjwa wa kaswende iliyojificha(Latent Syphilis).
4. Kaswede Ya Baadaye(Tertiary syphilis):
Asilimia ya wagonjwa wa kaswende ambao hawakupata tiba hapo awali huingia kwenye kundi hili kuanzia miaka 15-30 baada ya maambukizi ya kaswende hapo awali. Aina hii inaweza kuathiri viungo vya mwili kama vile macho, ubongo, mishipa ya fahamu(neurosyphilis), viunganishi vya mifupa(jointi), uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu, na hivi vyote husababisha madhara makubwa kama vile, upofu wa macho, magonjwa ya moyo, magonjwa ya akili, kuwa kiziwi, kupungukiwa kumbukumbu na hatimaye kifo.
NUKUU: Aina hii ya kaswende pia inaweza kuathiri mfumo wa usagaji chakula, mfumo wa upumuaji, na mfumo wa uzazi
5. Matatizo Ya Neva
Kaswende inaweza kusababisha matatizo mengi ya mfumo wa neva za fahamu hasa maumivu ya ghafla. Maumivu haya yanaweza kutokea katika viungo mbalimbali, mara nyingi tumboni na yanaweza kusababisha kutapika. Maumivu makali maeneo ya njia ya haja kubwa, kibofu cha mkojo, na kwenye koo la chakula yanaweza kutokea. Kaswende pia inaweza kumfanya muhusika mabadiriko ya joto mwilini mwake. Pia matatizo ya macho au upofu wa macho, uvimbe kwenye ubongo, na hata kiharusi kinaweza kutokea. Kuharibika kwa mfumo wa neva pia husababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.
6. Matatizo Ya Moyo
Hali hii hujitokeza kati ya miaka 10 hadi 25 baada ya maambukizi ya kaswende kujirudia. Yanaweza kuambatana na uvimbe na kuvimba kwa mshipa wa aorta, mshipa mkuu wa ateri mwilini. Ugonjwa wa kaswende unaweza pia kushambulia mishipa mingine ya damu na vali za moyo.
7. Madhara Ya Kaswende Kwa Ujauzito Na Kiumbe Tumboni
Kama ukiwa na maambukizi ya kaswende huku ukiwa mjamzito, unaweza kumfanya mtoto naye akapata maambukizi hayo. Mtoto mwenye maambukizi ya kaswende huwa yuko katika hatari ya kuzariwa akiwa na kasoro nyingi zitakazokuwa zikiendelea.
Kaswende wakati wa ujauzito husababisha hasa mimba kuharibika au mtoto kufia tumboni, na mtoto anayepata kaswende kutoka kwa mama huwa yuko katika hatari ya kufa muda mfupi baada ya kuzariwa.
Nipende kuishia hapa wapendwa wasomaji wa makala hii. Niwakaribishe wenye maswali, naomba mtume maswali na maoni yenu katika website yetu.
Je, Unahitaji Huduma?
Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP au TELEGRAM tukakuunganisha na darasa letu ili uweze kupata masomo ya afya kila siku.
Karibuni sana.