Bawasiri ni mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa ambayo ni sehemu ya kawaida ya mwili wako. Zinaweza kuwa za ndani yaani mishipa ya damu inayokuwa kwenye tishu yenye unyevunyevu ndani ya ukuta laini wa njia ya haja kubwa. Bawasiri zinaweza pia kuwa za nje, yaani mishipa ya damu inayokuwa chini ya ngozi nje ya njia ya haja kubwa. Bawasiri zinaweza kuwa za kawaida na zenye matatizo pale zinapokaa muda mrefu bila kupata matibabu.
Je, Ugonjwa Wa Bawasiri Ni Nini?
Ugonjwa wa bawasiri ni hali ya kawaida inayotokea pale mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa inapovimba kutokana na kuongezeka kwa shinikizo la damu. Kuvimba huku kunapalekea kuwepo hali mbaya na kusababishi dalili za bawasiri. Dalili na madhara ya bawasiri hutofautiana kutegemeana na huenda bawasiri ni ya ndani au ya nje.
Je, Dalili Za Bawasiri Ya Ndani Zinakuwaje?
Wakati bawasiri ya ndani inapopanuka kwa kawaida huwa haina maumivu na huambatana na kushuka kwa njia ya haja kubwa na kutokwa na damu kidogo kidogo. Hali ya kushuka hutokea pale tishu ya bawasiri inapotokeza nje ya njia ya haja kubwa wakati wa kutoa kinyesi. Ni kawaida kujihisi tishu ya ndani ya njia ya haja kubwa kutoka nje na inachanganuliwa kwa hatua nne. Hatua hizi ni kama hivi ifuatavyo;
- Hakuna kutokeza kwa tishu
- Tishu ya ndani ya njia ya haja kubwa inapotokeza hurudi ndani yenyewe
- Tishu ya njia ya haja kubwa unalazimika kuirudisha ndani mwenyewe
- Tishu ya ndani ya njia ya haja kubwa huwezi kuisukuma mwenyewe
NUKUU: Mkakati wa kutokeza kwa tishu kwa kawaida hutokea kwa taratibu sana. Hali ya kutokeza kwa tishu ya njia ya haja kubwa inaweza kusumbua njia ya haja kubwa na inaweza kusababisha muwasho.
Je, Dalili Za Bawasiri Ya Nje Zinakuwaje?
Damu kuganda iliyotokeza huonekana kama uvimbe chini ya ngozi ya njia ya haja kubwa na inaweza kuendelea papo hapo baada ya kusukuma kinyesi kigumu kwa nguvu. Wakati mishipa ya damu inapochubuka, inamaanisha mgando wa damu umejengeka nah ii hutengeneza uvimbe. Bawasiri ya nje huwa na maumivu makali mno na inaweza kutoa damu.
Baada ya bawasiri ya nje kupona au damu iliyoganda inaporudi ndani ya mwili, basi alama ya ngozi inaweza kuachwa nyuma. Mkundu au njia ya haja kubwa ni eneo linalokazwa na ngozi inayofunika bawasiri huonekana kubaki kutanuka baada ya kutoweka. Alama za ngozi hazina maumivu, ni ndogo, na karibia hubana vipande vya ngozi. Japokuwa zinaweza kuleta usumbufu, basi alama za ngozi huwa hazina madhara na hutibika.
Je, Nini Husababisha Bawasiri Isiyo Ya Kawaida?
Mara nyingi, kukosa choo, kuharisha au kutoa kinyesi kwa kujisukuma kwa nguvu husababisha bawasiri isiyo ya kawaida. Ingawa inaweza pia kusababishwa na ujauzito au umri kuwa mkubwa.
Je, Nani Anayekuwa Katika Hatari?
Bawasiri isiyo ya kawaida inaonekana kuwa ya kurithi. Unaweza kuipata ikiwa kama wazazi wako waliwahi kuwa na tatizo hili. Wanawake wajawazito huwa na hatari ya kuendelea kuwa na bawasiri isiyo ya kawaida kutokana na msukumo wa mfuko wa uzazi kwenye mishipa ya damu katika eneo hilo. Hatari hiyo pia huongezeka kutokana na umri wa muhusika.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Bawasiri isiyokuwa ya kawaida huwa ina dalili mbalimbali nazo huwa kama ifuatavyo;
- Muwasho
- Kutojisikia vizuri
- Kutokwa na majimaji njia ya haja kubwa
- Kujisikia kwamba choo au kinyesi kinataka kutoka
- Kutokwa na damu katika njia ya haja kubwa.
NUKUU: Damu unayoweza kuipata unapokuwa na tatizo la bawasiri huwa ni nyepesi, kiwango kidogo, na yenye rangi nyekundu ya kung’aa. Unaweza kuiona chooni unapojitawaza au kwenye kinyesi unakunya.
Je, Nini Chanzo Chake?
Ugonjwa huu mara nyingi husababishwa na mambo mengi mbalimbali hasa ulaji wa vyakula vibaya visivyo vya asili. Mambo haya ni kama hivi ifuatavyo:
1. Ulaji Wa Vyakula Vibaya
Ulaji wa vyakula vilivyosindikwa, vilivyokobolewa, nyama, nk, ndivyo husababisha matatizo haya kutokana na kwamba huchelewesha usagaji chakula tumboni na kumfanya muhusika kupatwa na hali ya kukosa choo huenda siku 1, 2, 3 na kuendelea, na anapokipata choo chake huwa kigumu mno kama cha mbuzi.
2. Kikohozi Kizito
Tatizo la kukohoa linapokuwa la muda mrefu na kikawa kigumu, basi kinaweza kuwa chanzo pia cha kupatwa na tatizo la bawasiri. Baadhi ya watu wanaosumbuliwa na kikohozi kwa muda mrefu hupatwa na tatizo la ugonjwa huu kwa namna fulani.
3. Mwili Kuongezeka Uzito Au Mimba
Hali hii kwa kawaida imekuwa ikionekana pia kwa wanaume au wanawake wenye mwili mkubwa kutokana na kuongezeka kwa unene. Baadhi yao hushindwa kupata choo kutokana na chakula kushindwa kusagwa kwenye matumbo yao.
Je, Jinsi Gani Unaweza Kuzuia Bawasili Isiyo Ya Kawaida?
Fuata njia hizi ili zikusaidie kuzuia hali ya kukosa choo na hali ya kutumia nguvu kubwa wakati unapojisaidia chooni.
- Kula vyakula vingi vyenye wingi wa nyuzinyuzi au fiber
- Kunywa maji mengi
- Fanya mazoezi kila siku
- Epuka kuwa chooni kwa muda mrefu
- Hakikisha unapumzika vizuri mara unapopata chakula
Je, Lini Unaweza Kuonana Na Daktari
Kama unahisi maumivu sehemu ya njia ya haja kubwa, kutokwa na uteute kwenye njia ya haja kubwa, au kuhisi muwasho katika njia ya haja kubwa, au kuona damu kwenye kinyesi, basi hakikisha unafika hospitali bila kuchelewa. Madaktari wanaweza kubaini chanzo cha dalili ulizo nazo na wanaweza kukupa ushauri mzuri kabisa.
Nipende kuishia hapa mpendwa msomaji na Mungu akubariki sana popote ulipo. Unahitaji msaada kwa ajili ya tatizo hili, basi tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSSAP au TELEGRAM tukakuunganisha na GROUP au darasa letu ambapo unaweza kupata masomo muda wote, na unaweza kupata huduma popote ulipo ili kukusaidia matatizo yako.
Karibuni sana!
Kwa maelezo Dr inaonyesha nna bawasiri ya nje, sasa naomba kujua gharama za matibabu.
Pole sana, na uwe na amani kabisa kwamba utapona tu. Gharama ni shilingi 70,000/=. Unaweza kutuma namba zako za whatsap pia
asanteni kwa somo zuri
Karibu sana
Nawapataje
Tupo arusha, karibu sana