JE, UNAJUA CHANZO NA DALILI ZA CHANGO LA UZAZI KWA MWANAMKE?

Hali ya chango au tumbo kuunguruma wakati wa hedhi inaweza kumfanya mwanamke akakosa raha kabisa. Mwanamke anaweza kujihisi kama vile mwili wake umeongezeka uzito au kwamba tumbo lake limejaa na kujampa jampa. Lakini pia, huwa kuna mabadiriko ambayo mwanamke anaweza kuyapata na kupunguza dalili hizo.

NUKUU: Tumbo linapokuwa likiunguruma au chango ndio wakati mwanamke anapoanza kuhisi tumbo lake kuwa limejaa tena zito kabla au pindi anapoingia hedhini.

Baadhi ya wanawake wamekuwa wakisumbuliwa sana na maumivu chini ya tumbo au usawa wa kitovu. Na mara nyingi maumivu haya huwapata wasichana waliokwisha vunja ungo na wanawake watu wazima wenye umri wa kuzaa.

Je, Hali Hii Husababishwa Na Nini?

Chango au tumbo kuunguruma au kuuma kabla au wakati wa kipindi cha hedhi inaweza kutokana mabadiriko ya kiwango cha vichochezi au homoni za progesterone na estrogen.

Viwango vya homoni ya progesterone hushuka karibia wiki moja kabla kipindi cha hedhi cha mwanamke hakijaanza. Kupungua kwa kiwango cha homoni hii husababisha ngozi laini ya ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus) kubanduka, hali ambayo ndiyo husababisha kuvuja kwa damu ya hedhi.

NUKUU: Pamoja na kubanduka kwa ngozi laini ya ukuta wa mfuko wa kizazi inayosababisha kuvuja kwa damu ya hedhi, lakini bado kiwango cha homoni ya progesterone pamoja na estrogen kinachobadirika husababisha mwili uzarishe maji mengi na chumvi chumvi. Hivyo basi, seli za mwili huvimba kutokana na maji, na kusababisha hali ya tumbo kuunguruma au chango la tumbo.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kwa kawaida huwa kuna dalili nyingi mno, yaweza kuwa chango au tumbo kuunguruma, nazo huwa kama hivi ifuatavyo:

  • Mwili kuchoka
  • Kuhisi vichomi
  • Kutokwa na chunusi usoni
  • Kutamani vyakula
  • Matiti kuvimba
  • Kichwa kuuma
  • Mgongo kuuma

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Na ufahamu kuwa, tatizo la change lisipotibiwa mapema likapona linaweza kusababisha madhara haya yafuatayo;

  • Kwa mwanamke ni vigumu kupata mimba
  • Mwanamke anaweza kuwa mgumba kabisa
  • Kuingia na kutoka kwa mimba
  • Kuwa na hamu ya tendo la ndoa lakini hafikii kileleni
  • Kuwa na uke mdogo sana

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Chango la uzazi halisababishi madhara menine, bali linaweza kuingiliana na kazi au masomo kwani linaweza kukufanya usifanye shughuli zako au kuwa masomoni mwako. Pia linaweza kusababisha kutokupata ujauzito.

Nipende kuishia hapa mpendwa msomaji, tutaonana kipindi kingine kifuatacho.

Je, Unahitaji Huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

 

Pia tunatoa masomo mengi mbalimbali ya afya katika GROUP letu la TELEGRAM na WHATSAP, hivyo unaweza kutuma namba zako tukaweza kukuunganisha na group letu.

Karibu sana!

 

 

 

11 thoughts on “JE, UNAJUA CHANZO NA DALILI ZA CHANGO LA UZAZI KWA MWANAMKE?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *