JE, YAWEZEKANA TABIA YA KUTOA MIMBA IKAMFANYA MWANAMKE KUPATWA NA LAANA MBAYA KATIKA MAISHA YAKE?

Siku hizi utoaji mimba unaelekea kuwa utamaduni wa wanawake wengi duniani, vilevile na hata katika nchi yetu hapa Tanzania. Jambo la kutoa mimba limekuwa la kawaida sana na inaelekea jamii imeanza kulizoea na kuliona kuwa ni tukio la kawaida. Ni kama vile halina madhara makubwa.

Leo tunaanza kujadili mada inayohusu LAANA itokanayo na utoaji mimba. Kwanza kabisa tunaweza kusema, neno LAANA maana yake ni kama kisababishi cha madhara au maumivu au huzuni au mateso.

NUKUU: Laana ya utoaji mimba inatokana na ukiukaji wa amri ya Mungu ‘USIUE’ (Kut. 20:13). Uuaji ni kosa linalokwenda kinyume na matashi ya binadamu ya kuheshimu na kulinda uhai wa binadamu. Hata katika sheria za nchi mbalimbali zinaweka adhabu kali kwa kosa la binadamu kumwua binadamu mwingine.

 

Na anayemwuua mwingine katika dhamiri yake anaisikia ile laana ya Mungu ikitamkwa waziwazi ‘UMELAANIWA WEWE’ na baada ya hapo anakabiliwa na adhabu zinazomsabishia mateso, maumivu, majuto au huzuni katika maisha yake.

Laana ya utoaji mimba inajitokeza katika maumbo na matendo mabalimbali na kwa watu mbalimbali. Iko laana anayoipata mwanamke mtoaji mimba au anayetupa mtoto; iko laana inayowapata watoto wanaosalimika katika jaribio la kutoa mimba au waliozaliwa kabla au baada ya mwenzao kuuawa, au watoto waliozaliwa katika nchi ambayo imepitisha sheria ya utoaji mimba. Vilevile iko laana inayompata daktari au mtu yeyote aliyemwua huyo mtoto kabla hajazaliwa. Tutatazama vilevile jinsi laana ya utoaji mimba inavyozikumba familia. Tutajadili pia laana ya utoaji mimba ambayo imetapakaa katika jamii yetu ya leo.

 

 

Je, Laana Kwa Mwanamke Aliyetoa Mimba Au Aliyetupa Mtoto Inakuwaje?

 

 

 

Hebu tuiangalie kwanza laana katika muktadha ya Biblia Takatifu ili tuone jinsi inavyohusiana na laana ya utoaji mimba katika enzi zetu hizi tulizonazo. Laana hutolewa  au hutamkwa na Mungu baada ya mwanadamu kukiuka amri zake au maagizo yake. Daima laana inaambatana na adhabu ambayo yaweza kuwa ya kimwili, kisaikolojia(yaani akili kuchanganyikiwa) au kiroho

 

 

NUKUU: “Kaini akamwambia Habili nduguye, ‘Twende uwandani”. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, AKAMWUA. Bwana akamwambia Kaini, “Yuko wapi Habili ndugu yako?” Akasema, “Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” Akasema, “Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhiBasi sasa UMELAANIWA wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wakoutakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani” (Mwa.4:8-12).

 

NUKUU: Katika kisa hiki, Kaini analaaniwa na Mungu baada ya kutenda kosa kubwa, yaani la kumwua nduguye Abel. Laana ya Mungu kwa Kaini inaambatana na adhabu ambayo ndiyo inakuwa kisababishi cha mateso yaliyomkabili Kaini katika maisha yake. Yawezekana Kaini hakuweza kuishi maisha ya kutulia mahali au sehemu moja, huenda alikuwa ni mtu wa kutangatanga huko na kule lakini bila mafanikio kwasababu ya laana hiyo.

 

 

Laana ya kwanza

 

 

 

 

Laana inayomkabili mwanamke anayemwua mtoto wake kabla hajazaliwa. Kuna baadhi ya wanazuoni wanagawa laana hiyo katika makundi ya muda mfupi na muda mrefu.  Hebu tuangalie laana hiyo katika mtazamo wa kisa cha Kaini na Abel.

 

Kwa kumwua mtoto wake mwanamke ni kama anatoa kafara ya mtoto wake na damu yake kuwa chakula cha Ibilisi. Mungu anamwambia Kaini ‘damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi’. Kumbe damu ya mtoto anayeuawa inamwagika ardhini na maiti ya mtoto aliyeuawa inatupwa ardhini na hivyo kuwa ndicho chakula cha Ibilisi. Kwa kadiri idadi ya wanawake watoaji mimba inavyoongezeka ndivyo hivyo Ibilisi anavyojipatia chakula chake kwa wingi.

 

NUKUU: Ndugu wapendwa, tukumbuke daima kuwa katika kila tendo la utoaji mimba, mwanamke anamwaga damu yake na mtoto sio tu anamwaga damu bali pia mwili wake. Kwa hiyo Ibilisi anajilisha kwa damu itokayo kwa mama wa mtoto, damu na maiti ya mtoto aliyeuawa katika kitendo cha utoaji mimba. Na Ibilisi anachochea sababu au visingizio vingi kwa wanawake kuwaua watoto wao, kwa mfano; mwanamke anapopata ujauzito bila kutarajia anaweza akawa na visingizo vingi akidai kwamba:

 

  1. Hataki kuzaa maana muda bado,

 

  1. Hataki kujizeesha mapema,

 

 

  1. Au kwamba mwanaume aliyempatia ujauzito hakutarajia kuishi naye katika ndoa,

 

  1. Kapata ujauzito lakini bado yuko masomoni,

 

 

  1. Wazazi wake watamfukuza nyumbani, nk.

 

 

Kilele cha ushindi wa Ibilisi ni pale nchi(dunia) inapofikia hatua ya kutunga sheria za kuwaua watoto kabla ya kuzaliwa. Na pengine Ibilisi anahusisha vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watoto na vuguvugu la wanawake kudai haki zao; wakisema kuwa wana haki juu ya miili yao au ni uhuru wa uchaguzi kwao. Vilevile Ibilisi amempatia binadamu maneno na lugha tamu ili kuhalalisha vitendo hivyo viovu – haki ya afya ya kizazi, uzazi wa mpango. Hayo yanafanyika ili kujenga uhalali wa binadamu kuvikubali vitendo ambavyo kwa asili yake ni viovu. Ndivyo hivyo Ibilisi anavyofanya ili kujipatia mawindo yake. Kwa hiyo kuna uhusiano mkubwa kati ya utoaji mimba na nguvu za kishetani zinazochochea vitendo hivyo. Ndugu wapendwa mabinti wote na hata wanawake pia napenda kuwashauri kuwa ni vyema tukauogopa uwepo wa Mungu na sheria zake. Kitendo cha utoaji mimba kinaweza kusababisha laana mbalimbali katika maisha yako, kama vile kukosa amani katika ndoa yako baadaye kwasababu Mungu kazuia usipate ujauzito tena, au ukaandamwa na mateso kama vile magonjwa katika tumbo lako la kizazi, nk.

 

Nashukuru sana wapendwa kwa kunisikiliza, Mungu awabariki sana.

Je, unahitaji huduma kutoka James Herbal Clinic? Tupigie simu hizi: 0752389252 au 0712181626

 

 

Karibuni sana