JE, KUTOKWA NA UCHAFU WENYE MAJIMAJI UKENI WAKATI WA UJAUZTO NI JAMBO LA KAWAIDA?

Wanawake wajawazito hupatwa na msongo wa mawazo sana kwa vitu vidogo vidogo tena vya kawaida mno.  Zipo sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea kutokwa na uchafu wenye majimaji ukeni wakati wa ujauzito. Baadhi ya sababu hizi ni za kawaida kabisa wala hazina madhara, lakini zingine zipo zinaweza kuonyesha viashiria vya hatari, nawe unapaswa uwahi kufika hospitali mara uonapo hali dalili kama hizo.

 

Image result for image of pregnant woman

 

Anapendeza kweli mama mjamzito pale tumbo linapozidi kukua, kama unavyoona hapo juu kwenye picha.

 

Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo hutokana na kutokwa na uchafu wenye majimaji ukeni wakati wa ujauzito:

 

  1. Utoko Mweupe

 

 

Kwa upande mwingine naweza nikasema hivi, utoko ni kitu cha kawaida kabisa; lakini kinaweza kuwa kibaya kwa mwanamke anapokiona kinatokea wakati wa ujauzito wake.

Related image

Lakini nipende kukufahamisha kuwa, viwango vya homoni ya estrogen huongezeka sana kadiri mimba inavyozidi kukua, na hali hii husababisha huongeza mtiririko wa damu kuelekea ukeni, na matokeo yake ndio utaona uchafu wenye majimaji ukitoka ukeni.

NUKUU: Uchafu huwa ni wa kawaida kabisa tena mzito na wenye rangi nyeupe. Mara nyingi hali hii inapojitokeza kwa mama mjamzito humpa wasiwasi sana, na imani yake huja mara tu pale anapopata maelezo kutoka kwa daktari.

 

 

  1. Ute Utelezi

 

 

Jambo lingine ni hili hapa, napenda niwajulishe kina mama wajawazito kuwa, unapobeba ujauzito, mlango wa kizazi(Cervix) huvimba na kuwa mnene kwa ajili ya kutengeneza mlango au uwazi. Ikiwa kama ungebaki katika hali hiyo, basi yaweza kuwa hiyo ndio ingekuwa njia ya kupitia bakteria kwenda kwenye mji wa mimba(uterus). Lakini mwili hauwezi kuruhusu hali hiyo ijitokeze kwa kiumbe kinachkuwa tumboni.

 

Related image

NUKUU: Hivyo basi, chini ya mlango au uwazi huo hutengenezwa ute ute mwingi, nao huzuia aina ya bakteria yoyote asiweze kuingia kwenye mfuko wa uzazi(uterus).  Mwanamke anapokaribia kujifungua, uteute huondoka na hivyo husababisha kuwepo kutokwa na uchafu wenye majimaji ukeni na unaweza ukashuka mpaka mapajani mwake. Lakini hatua hii ya ujauzito, wanawake wengi wameizoea kama hali ya kutokwa na uchafu ukeni.

 

 

  1. Mkojo

 

 

 

Kadiri tumbo la mama mjamzito linavyozidi kuwa kubwa, bila shaka huleta habari mpya kwa mama au mume anayetarajia mtoto.  Naamini kila siku inapopita lazima mama akutane na miujiza mipya.

 

Tambua leo hili kuwa, tumbo linapozidi kuwa kubwa pia husababisha msukumo hasa maeneo ya kibofu cha mkojo. Mjamzito anapokohoa, au kucheka, mara nyingi vinaweza vikashuka vitu kama majimaji ukeni. Lakini cha kushangaza ni kwamba, huu huwa ni mkojo tu.

 

  1. Kujifungua Kabla Ya Muda

 

 

Uonapo uchafu wa majimaji wenye rangi ya kahawia au nyekundu wakati wa ujauzito ukitoka ukeni, unapaswa kuwa makini sana. Yawezekana ni dalili za kujifungua kabla ya muda wake, na unapaswa kukimbia hospitali mapema ili kuonana na daktari.

Related image

Unaweza ukavua nguo ya ndani ukashangaa unaona uchafu kama huo hapo kwenye nguo ya ndani

 

 

  1. Bakteria Ukeni

 

 

Bakteria ukeni huzaliana kama matokeo ya kutokuwa na uwiano sawa wa bakteria wa asili ukeni. Uonapo dalili za uchafu wa njano au ukijivu vile ukitoka ukeni tena wenye harufu mbaya kama shombo ya samaki, basi hizi ni dalili zinazoonyesha kuwa una bakteria ukeni, na unapaswa uwe na tahadhari kubwa sana ili kuweza kupata matibabu kwa ajili ya kuzuia madhara yoyote kwa kiumbe kilichomo tumbini.

Related image

Unaweza kukutana na uchafu kama huo mama mjamzito kwahiyo unapaswa uwe makini sana.

 

 

  1. Magonjwa Ya Zinaa

 

 

Utafiti unaonyesha kwamba wanawake wajawazito wanapenda kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, sijui kama madai haya ni ya kweli au la. Lakini ni kweli kabisa kuwa wanawake wengi wajawazito hushindwa kuvumilia wanapokuwa peke yao bila mwanaume.

 

Image result for image of a pregnant woman doing sexual intercourse with her husband

NUKUU: Mwanamke mjamzito unapopatwa na maambukizi ya zinaa wakati wa ujauzito, dalili zinazokupata huwa ni kutokwa na uchafu wa njano wenye harufu mbaya ukeni.

 

 

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba zetu hizi: 0752389252 au 0712181626.

 

 

Arusha-Mbauda

 

 

Karibuni sana.