RANGI YA UTE AU UCHAFU UNAOTOKA ILI KULINDA MAENEO YA UKE

Ni kawaida kushangaa endapo kama rangi au uchafu unatoka mara kwa mara ukeni kuwa ni wa kawaida au unahitaji kuchunguzwa. Uchafu utokao ukeni unaweza kuwa na rangi nyingi, na viashiria mbalimbali ili kuonyesha kuwa mwili una afya.

Katika makala hii tunaenda kujifunza ili tujue je, ute unalinda maeneo ya uke unakuwa na rangi gani?

 

 

Je, Uchafu Unaotoka Ukeni Huwa Ni Kitu Gani?

 

Uchafu utokao ukeni huwa ni majimaji fulani yanayotengenezwa kutoka kwenye tezi ndogo zinazokuwa ukeni na kwenye mlango wa kizazi. Maji maji haya huvuja kutoka ukeni kila siku ili kuondoa seli zilizochoka pamoja na mabaki, ili kuufanya uke pamoja na njia ya mfumo wa uzazi uwe katika hali yenye afya nzuri.

Image result for image of a healthy woman

Kiwango cha uchafu unaotoka ukeni kinaweza kutofautiana kwa kila mwanamke. Rangi, uzito, na kiwango vinaweza pia kubadirika kila baada ya siku, kutegemeana na mazingira ya mwanamke anapokuwa hedhini:

 

 

  • Siku ya 1-5

 

Mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi, uchafu unaotoka ukeni mara nyingi huwa mwekundu au wenye damudamu, kadiri mwili unavyotumia nguvu kuliondoa gamba laini linalokuwa juu ya ukuta wa mfuko wa kizazi.

 

  • Siku ya 6-14

 

Kipindi cha hedhi kinachofuata, mwanamke anaweza kuona damu kidogo ikitoka ukeni kuliko kawaida. Yai linapoanza kukua na kukomaa, basi ute utelezi unaokuwa kwenye mlango wa kizazi utabadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu au mweupe au wa njano. Unaweza ukawa mzito.

 

 

  • Siku ya 14-25

 

 

Siku chache baada ya yai kupevuka, ute utelezi hubadirika na kuwa mwepesi wenye kuteleza, kama ute wa yai la kuku vile. Baada ya yai kupevuka, ute hubadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu, mweupe au wa njano, na wenye kunata.

 

 

 

  • Siku ya 25-28:

 

Ute utelezi unaokuwa kwenye shingo ya kizazi hubadirika na kuwa mwepesi, na mwanamke anaweza kuuona kidogo tu, kabla hajaingia kwenye kipindi kingine cha hedhi.

 

 

  1. Uchafu Wenye Rangi Nyekundu

 

 

Uchafu huu mwekundu unaweza kutofautiana, kwani unaweza kuwa wenye rangi yenye kung’aaa au nyekundu sana. Uchafu mwekundu huwa ni matokeo ya damu ya hedhi kuanza kutoka.

Damu ya hedhi hutokea, kwa wastani, kwa kila mzunguko wa siku 28, ingawa kiwango cha kati huwa ni siku 21 na 35. Hedhi huwa ni ya siku 3-5.

 

Related image

NUKUU: Mwanamke yeyote anayepata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja, anapaswa afike hospitali mapema ili kumuona daktari. Ingawa kuna visababishi vingi hafifu vya kumfanya mwanamke apate hedhi mara mbili kwa mwezi, lakini navyo vinaweza wakati mwingine kuwa viashiria vya matatizo mabaya baadaye.

Mwanamke yeyote aliyefikia hali ya kukoma hedhi na kutokuona hedhi kwa takribani mwaka mmoja, anapaswa amuone daktari mapema ikiwa kama anapatwa na hali ya kutokwa na damu ukeni. Hii yaweza kuwa ni dalili ya salatani.

 

  1. Uchafu Mweupe

 

 

Uchafu mweupe unaweza kuongezeka, unaweza ukawa kama maziwa vile au wa njanonjano kwa mbali. Endapo mwanamke hatakuwa na dalili zingine, basi uchafu mweupe unaweza kuwa kiashiria kabisa cha kilainishio kizuri chenye afya ukeni mwake. Utakuta uke wake uko katika hali nzuri hata anapokutana kimapenzi na mwezni wake hakutakuwa na shida yoyote zaidi ya kufurahia tendo la ndoa.

Image result for image of white vagina discharge

NUKUU: Hata hivyo, endapo kama uchafu mweupe utakuwa mzito kama maziwa mtindi vile na kuwa na harufu mbaya, basi hii yaweza kuwa dalili za maambukizi. Muhusika anapaswa afike hospitali haraka bila kuchelewa ili kumuona daktari wa vipimo.

Uchafu mweupe wenye kunata, na wenye harufu mbaya mara nyingi huwa ni wenye maambukizi ya fangasi, ambao pia unaweza kusababisha muwasho ukeni.

 

 

  1. Uchafu Wenye Rangi Ya Njano Na Ukijani

 

 

Kama uchafu una rangi ya njano njano, inaweza isiashirie tatizo kwako. Hali hii hasa inaweza ikasababishwa kubadirika kutokana na vyakula unavyotumia.

 

Image result for image of yellow and green vagina discharge

Uchafu ambao ni wa njano kabisa, unjano wenye ukijani, au kijani yenyewe, mara nyingi huwa ni dalili za bakteria au maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Jitahidi kumuonda daktari mapema endapo kama uchafu ni mzito na wenye harufu mbaya.

 

  1. Uchafu Wenye Rangi Ya Pink

 

 

Uchafu unaweza kuwa wenye rangi ya pinki kwa mbali au kabisa. Mara nyingi huwa unakuwa na damudamu kidogo. Uchafu wenye rangi ya pinki kwa kawaida  hujitokeza huku ukiwa na matone ya damu damu kabla ya kipindi cha hedhi kuwadia. Hata hivyo, inaweza pia kuwa ishara ya damu kutoka pale yai linapojipachika kwenye ukuta wa tumbo la uzazi ujauzito unapoingia.

Image result for image of pink vagina discharge

NUKUU: Baadhi ya wanawake hutokwa na matone ya damu damu baada ya yai kupevuka, hali ambayo pia inaweza kusababisha kutokwa na uchafu wa pink. Uchafu unaweza kuwa wenye rangi ya pink baada ya kufanya tendo la ndoa, endapo kama tendo lenyewe limesababisha maumivu kidogo au muwasho ukeni au maeneo ya mlango wa kizazi.

 

  1. Uchafu Msafi

 

 

Uchafu wa kawaida huwa ni msafi mweupe. Unaweza kuwa mwepesi au ukawa na uzito kama ute wa yai vile. Mwanamke anaweza akatokwa na uchafu mweupe msafi, mwepesi kabla yai halijapevuka, au wakati hisia au nyege zinapompanda, au anapopata ujauzito.

 

Related image

  1. Uchafu Wenye Rangi Ya Ukijivu

 

 

 

 

 

Uchafu unaotoka ukeni huku ukiwa na rangi ya kijivu huwa sio mzuri, na inaweza kuwa dalili za maambukizi ya bakteria wajulikanao kama, “Bacterial Vaginosis(BV)”.

 

Bakteria hawa kwa kawaida husababisha dalili zingine ukeni kama vile;

 

 

  • Muwasho

 

  • Hali ya kama moto ukeni

 

 

  • Harufu mbaya ukeni

 

  • Hali ya wekundu maeneo ya mashavu ya uke au mlango wa uke

 

 

NUKUU: Mwanamke yeyote anayetokwa na uchafu wenye rangi kama ukijivu pamoja na dalili zake hizo anapaswa kufika hospitali haraka sana bila kuchelewa.

 

Je, Ni Lini Unapaswa Kumuona Daktari?

 

 

Nakushauri umuone daktari ikiwa kama uchafu una harufu au muonekano usi wa kawaida . Mwanamke napaswa pia kutafuta tiba endapo kama anapatwa na dalili kama zifuatazo:

 

  • Muwasho

 

  • Maumivu au kutojisikia raha

 

 

  • Uchafu mzito kama maziwa ya mgando

 

 

  • Kutokwa na damu mara mbili kwa mwezi au baada ya hedhi kukoma

 

  • Kutokwa na damu baada ya kufanya tendo la ndoa

 

 

  • Kutokwa na damu kila mara baada ya kufanya tendo la ndoa

 

  • Kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano, ukijivu, au kijani

 

 

  • Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya

 

  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kukojoa

 

urine sample for bence jones protein test

NUKUU: Daktari atapima maeneo ya nyonga. Pia anaweza kuchukua uchafu kidogo ili kufanya vipimo.

 

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

Arusha Mbauda

 

Karibuni sana

78 thoughts on “RANGI YA UTE AU UCHAFU UNAOTOKA ILI KULINDA MAENEO YA UKE

  1. Nimefurahia sana hili somo maana nimemaliza siku zangu nikaona ute mweupe nikawa nahofu sana kumbe ni kawaida , asante kwa kutuelimisha

  2. Mimi nilimaliza period kama kawaida siku 5 and nikaanza kutokwa na ute mweupe na usionuka nikaogopa ila baadae nikajua ni kawaida but leo nimeingiliana na m2 wangu nilivyomaliza nikaona damu kidg imetoka so hiyo ni nn

  3. Mi niliingiliana na mume wangu siku ya 13 siku inayofata nimeanza kuona uchafu wa pink naogopa sana japo hauna harufu

  4. Nilivyoingia siku zangu za hatari nilitokwa ute mweupe mzito baada yakushiriki na mme wangu siku ya 3 ukaanza kutoka ute mweupe umechanganyikana na ule wamajimaji unavutika sijui nitatizo maana naogopa

    1. Hizo ndo zilikuwa siku za hatari bila shaka hujajua namna ya kutofautisha. Naomba utume namba yako ya whatssap

  5. Mimi ni mjamzito na natoka huo uchafu mweupe na siku kadhaa hapo nyuma umekuwa kama wa cream je nifanyajee,maan sijaona kama imeelezwa kwa wamama wajawazito.

  6. Mm natokwa na uchafu wa mgando Kama mtindi lakin siwashwi Wala kupat maumivu yeyote na uchafu huo hutoka kila Mara na kusambaa kwenye uke pande zote napata wasiwas unaweza kunambia una maana gani

  7. Habari nilipitiliza siku zangu mwezi mzima na haikuwa kawaida nilivyokuja kupata siku zang nikableed kwa mda wa siku kama kumi hiv baada ya hapo bado natokwa na ute wenye rangi nyeusi na mda mwingine wenye damu,haunuki na wala siwashwi hiyo itakuwa ni nini maana sio kawaida kwangu.

  8. Ninasiku ya 11 ila naona uchafu unaotok unadam dam pia naskia maumi kwa mbal ya tumbo je hii itakuwa n nn…naomb unijib kupitia no 0717778449

    1. Pole sana dada naomba ufuate data yako tayari nimeshakutumia link yetu, ingia ujifunze zaidi na utapata huduma

  9. Mim pia Nina shida ya kutokw na uchafu mweupe mzito hila haunuki Wala hauna miwasho na nilishaenda hospital wakasema uti na fungas nikatumia dawa lakin siponi hata

  10. Mimi ni mjamzito wa nilikua natoka uchafu mweupe mzito na harufu mbaya ukeni nkaenda hosptal nkapewa dawa za kuingiza znaitwa labesten na vidonge vya spotclav 625 asubuh nkiamka chupi inakua na rangi ya kijani au kam blue iv af bado harufu ni kali! Nina maumivu ya kiuno ya kwenye kibofu na nyonga pia yanakuja na kuondoka

  11. mimi nmepata uchafu wa pinki(spotting) sina uchungu wowote wakati wa kukojoa wala muwasho wowote sina. nimebakisha siku nane ili kuanza hedhi zangu jee hii ni sawa ama kuna shida

  12. Mm toka nimekaribia hedhi matiti yalikuwa yakiuma na kujaa had nimeingia period had nimemaliza nikakutana na mume wangu lkn bado matiti yamejaa na kuuma pia ,pia kuna damu damu inanitoka ila sio kama ya hedhi haina harufu sijui shida ni nn

    1. Pole sana dada hizo ni dalili za kuongezeka kwa homoni ya progesterone. Tuma namba yako ya whatssap uweze kuunganishwa na darasa

  13. Tunashukuru kwa maelezo mazuri maana nilianza kuogopa baada ya kuona Ute mweupe kumbe ni kawaida na uke upo katika Hali mzuri Asante

  14. Duh mm nimemaliza period yng ila nilikuwa na tatizo la kutopata ute kabisa nimetumia dawa za bf suma ila now nina karibia kumaliza mwezi nimeona ute mweupe mwepesi unavutika hiyo inaweza kuwa ni nini? Pia matiti ya mejaa na chuchu zinauma sana

  15. Habri, ikiwa umefanya mapenzi nawenza wako na baada ya hapo ukaona uchafu unatoka toka kila wakati na ukaendelea kwa siku. Za mbele je ni kawaida?

  16. Mimi nimekuwa nikitokwa uchafu mweupe umechanganyika na ule ute kama maji(ute wa hisia ama kilainishi). Je hiyo ni shida?

  17. Mimi natokwa na ute mweupe umechanganyikana na ule ute kama maji kisha baadae umetoka mweupe tu na hauna harufu ila unateleza mno
    Je kuna shida hapo

  18. Ninatokwa an ute mweupe mzito kama maziwa mtindi lakini siwashwi wala kutoa harufu Je kuna dalili zozote zisizo salama kiafya?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *