Uvimbe kwenye kizazi ni ugonjwa wa kawaida kabisa kwenye tumbo la uzazi ambao wanawake wengi wamekuwa wakiupata kwa kasi sana kuliko kawaida. Takribani asilimia 70%-80% ya wanawake wamekuwa wakipatwa na uvimbe wa fibroid mara moja au zaidi katika maisha yao hata wafikiapo umri wa miaka 50. Hata hivyo, uvimbe wa fibroid hauhusiani na salatani lakini bado unaweza kujionyesha wenyewe ndani ya mwili wa mwanamke.
NUKUU: Lakini nipende kutoa ushauri huu, James Herbal Clinic tunalo suluhisho la tatizo hili, kwani tuna dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuyeyusha uvimbe na kuuondoa kabisa. Uonapo dalili nitakazozitaja hapo chini, unapaswa ufike hospitali haraka kufanya vipimo na ukisha hakiki kwamba una uvimbe wa fibroid, basi unaweza kufika katika kituo chetu na ukaanza kupata tiba bila kuchelewa.
- Kutokwa Na Damu Nyingi Ya Hedhi
Wanawake wengi wana mzunguko wa hedhi wa kawaida, na kiwango cha damu cha kawaida ambacho hutoka kila mwezi. Ndio maana dalili hii hutambulika kwa urahisi sana. Kusema kweli, idadi kubwa ya wanawake wanaokuwa na matatizo ya uvimbe wa fibroid huanza kujitahidi kutafuta suluhisho la tatizo hilo baada ya kuona wakitokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi. Mbali na damu ya majimaji ile ya kawaida, uvimbe wa fibroid una tabia ya kuifanya damu kuganda. Unaweza kuiona hali hii kwa urahisi sana wakati wa kutokwa na damu ya hedhi.
NUKUU: Dalili yoyote ya uvimbe wa fibroid ni sababu tosha ya kuweza kumuona daktari. Damu nyingi wakati wa hedhi inaweza kutoka kwa muda mrefu zaidi ya siku 7-14, na kuendelea.
- Shinikizo La Kibofu Cha Mkojo
Unaweza ukauhisi uvimbe wa fibroid kwenye kibofu cha mkojo kutokana na ukaribu wa viungo hivyo viwili. Vivimbe vidogo vya fibroid vinaweza kusababisha shinikizo dogo. Uvimbe mkubwa wa fibroid unaweza kumfanya mgonjwa kuhisi kukojoa mara kwa mara au maumivu maeneo ya tumbo la chini. Katika dalili za aina hii, yafaa sana kutambua kwamba damu yoyote kwenye kibofu cha mkojo ni ishara tosha ya uvimbe mkubwa.
NUKUU: Kesi hizi ni nadra sana, lakini kumekuwa na matukio ambapo kibofu cha mkojo huharibiwa. Mpasuko wa maeneo hayo unaweza kusababisha mkojo kuvujia ndani mwilini pote, hali ambayo ni hatari sana.
- Shinikizo Kwenye Njia Ya Haja Kubwa
Uvimbe wa fibroid husababisha uharibifu maeneo hayo. Shinikizo linalokuwa kwenye njia ya haja kubwa ni ufunuo mwingine kabisa unaoonyesha jinsi uvimbe ulivyofikia ukubwa wake. Aina ya shinikizo kwenye njia ya haja kubwa inaweza kukudhihirishia kabisa ukubwa wa uvimbe huo. Uvimbe mdogo unaweza kuonyesha kiwango kidogo cha shinikizo kwenye utumbo mkubwa.
NUKUU: Uvimbe mkubwa hata hivyo, unaweza kuziba kabisa utumbo na kusababisha hali ya kukosa choo. Hali hii usipoitambua mapema au kama hautajali, dalili hii inaweza kuharibu moja kwa moja njia ya umeng’enyaji chakula(utumbo mdogo na mkubwa). Hali hii inaweza kupelekea ukafanyiwa upasuaji.
- Kuhisi Tumbo Limejaa Muda Wote Na Kukosa Hamu Ya Kula
Muda mwingine unaweza kujisikia tumbo limejaa hata kama hujala kitu chochote. Uvimbe mkubwa wa fibroid unaweza kushikiza juu tumboni, na kukufanya ujihisi tumbo limejaa kwasababu ya kuzibwa kwa nafasi ya usagaji chakula tumboni.
NUKUU: Hali inapozidi kuwa mbaya zaidi, unaweza kupungua uzito kwa haraka tu kutokana na kutokula chakula au hamu ya kula. Uonapo dalili hizi, yafaa sana kuwa hospitalini kwenda kupima na kuanza kupata matibabu.
- Kiuno Kuwa Kikubwa
Wengi wetu tunapenda kujiangalia kwenye vioo kila siku, na mabadiriko hutokea kwa urahisi sana tena kwa muda mfupi. Hii yaweza kuwa njia mojawapo ya kukufanya ujitambue kuwa wewe ni mgonjwa wa fibroid. Mabadiriko ya nje huonekana na kutoweka, yakiwamo na mengine kama vile muongezeko wa damu kwenye mishipa ya damu au misuli ya tumbo kutengana.
NUKUU: Kama hutaweza kuona dalili yoyote kwa nje, basi mavazi au nguo unazovaa zinaweza kuwa ishara tosha za uvimbe wa fibroid. Kama gauni lako unalopenda kulivaa utalihisi linakubana au halikutoshi, basi unaweza kuwa na uvimbe mkubwa wa fibroid ambao unasababisha tumbo kuwa kubwa. Uonapo dalili kama jitahidi sana kufika hospitali ili kuweza kupata huduma ya vipimo na kuanza matibabu mapema.
- Kushindwa Kupata Ujauzito
Hali ya ugumba kitaalamu tunaweza kuifafanua kama kutokuwa na uwezo wa kubeba mimba baada ya mwaka mmoja kuisha huku ukiwa katika ndoa. Sasa, hii inaweza kuwa ni kweli na ni dhahiri ikiwa kama hakuna kisababishi chochote kingine cha ugumba. Visababishi vya ugumba huja kutokana na utoaji mimba, mbegu za mwanaume kuwa chache, pamoja na utumiaji wa madawa mbalimbali bila ushauri wa daktari.
NUKUU: Baada ya kukamilisha vipimo vingine vyote na kuhakiki kabisa kuwa kila kitu kiko vizuri, basi uvimbe wa fibroid unaweza kuwa chanzo cha uharibifu. Unapaswa umwambie daktari wako kuwa una uvimbe wa fibroid.
- Kutokwa Na Damu Ya Hedhi Mara Mbili Kwa Mwezi
Hii ni dalili mojawapo ngumu kuionanisha na uvimbe wa fibroid, kama mambo mengine yanaweza kuusababisha. Unapaswa ujue kabisa kwamba hakuna makosa mengine katika lishe yako au afya yako.
Lazima upitie vipimo vingi, ili kuweza kugundua visababishi vya uvimbe wa fibroid. Kama ilivyo kwa kila dalili nyingine, daktari anahitaji kufanya uchunguzi ili kuweza kuona matatizo mengine yanayoendana na tatizo la uvimbe. Uvimbe unaweza kuzidi kukua na kufikia saizi kubwa kwasababu wanawake wengi huogopeshwa na dalili za uongo.
- Matatizo Ya Nyonga Yanayogunduliwa Wakati Wa Kipimo Kingine
Ugunduzi wakati wa vipimo vingine ni moja ya njia mojawapo ya kupima uvimbe wa fibroid. Hiyo ndio faida ya kufanya vipimo mapema.
NUKUU: Wanawake wanaokuwa na juhudi ya kufanya vipimo mara kwa mara na kujali miili yao wana uwezo mkubwa wa kuweza kugundua uvimbe wa fibroid mapema. Kama daktari anagundua vivimbe hivi mapema huku vikiwa bado vidogo, mgonjwa anapaswa ajiandae kupata matibabu haraka iwezekanavyo.
- Vipindi Vya Hedhi Kubadirika Badirika
Vipindi vya hedhi kubadirika ni dalili tosha ya kutokwa na damu nyingi au kutokwa na damu ya hedhi mara mbili kwa mwezi. Uvimbe wa fibroid unaweza kuharibu vifuko vya mayai(ovaries) na mfumo wote wa uzazi mwilini. Unapotambua kuwa una uvimbe kunaweza pia kumsaidia daktari kuweza kufanya suluhisho la tatizo hili.
NUKUU: Kukosa hedhi yaweza kuwa ishara nzuri kwamba tumbo la uzazi(uterus) pamoja na vifuko vya mayai(ovaries) vina matatizo. Wakati mwingine, hali hii inaweza kutokea kwasababu ya msongo wa mawazo, lakini kama ikiendelea, basi yaweza kuwa ni uvimbe wa fibroid.
- Kuharisha
Uvimbe wa fibroid unaweza kusababisha kuharisha, japokuwa sio kawaida. Sio asilimia kubwa ya wanawake wanaopatwa na hali hii, bali inategemeana na unyeti wa tumbo.
NUKUU: Habari njema ni kwamba, unaweza kuona hali ya kuharisha pamoja na dalili zingine. Kwa kawaida huonekana katika baadhi ya hatua za awali za tatizo hili, ili kuweza kukupa nafasi ya kutambuwa kuwa ni uvimbe wa fibroid. Kama unafahamu vizuri juu ya aina ya vyakula unavyotumia kila siku, basi kutambua dalili ya kuharisha inaweza isikupe tatizo.
Nashukuru sana msomaji wa makala hii, napenda kuisha hapa.
Je, unahitaji huduma kutoka James Herbal Clinic? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626-Arusha Mbauda.
Pia tunatoa masomo ya afya mazuri kwa njia ya mtandao wa TELEGRAM na WHATSSAP, hivyo unaweza kutuma namba yako ya whatssap ukaunganishwa na darasa letu.
Karibuni sana.