ZIJUE TOFAUTI ZA MANII NA SHAHAWA

Mwili wa mwanaume umebeba maajabu mengi mno kama ulivyo mwili wa mwanamke tu. Lakini maswali ya kawaida na ya ajabu ni yale yanayohusiana na manii. Wote tunafahamu kwa uhakika kwamba manii huwa zina mbegu lakini ni nini kilichomo zaidi humo ndani? Kwanini zinaonekana na zinaweza kutoa harufu inayotofautiana wakati mwingine? Na je, inawezekana kweli ikasaidia kuzuia mimba isitoke? Ili kujua majibu katika maswali haya juu ya manii, basi naomba ufuatilie makala hii vizuri kabisa.

  1. Fahamu Kuwa Manii Sio Mbegu

 

Manii na shahawa au mbegu huwa sio kitu kimoja. Mbegu ni seli zinazoonekana kwa kutumia darubini ambazo ni sehemu ya manii. Kazi ya shahawa au mbegu ni kurutubisha yai ndani ya mwili wa mwanamke. Ili shahawa ziweze kufika huko zinapaswa zibebwe na uteute ambao huzarishwa na viungo mbalimbali vya uzazi uzazi vya mwanaume. Mirija miwili inayokuwa kwenye nyonga ambayo kitaalamu tunaita, “Seminal Vesicles” hutoa aina ya sukari fulani ambayo huipatia shahawa au mbegu  nishati au nguvu ya kuweza kuogelea na kulifikia yai.

NUKUU: Uteute unaokuwa kwenye tezi huwa unakuwa na kemikali ambazo huzifanya manii kuwa za majimaji kiasi kwamba mbegu huweza kuogelea kwa uhuru kabisa bila shida. Vitu vyote hivi hutengeneza manii.

 

  1. Mbegu Zina Virutubishi

 

Mbegu za mwanaume zina Vitamini B12, C, madini ya Calcium, ascorbic acid, citric canid, lactic acid, sukari, Zinki, Magnesium, potassium, mafuta, sodium na protin kwa wingi. Lakini kiwango cha virutubishi hivi kwakweli huwa ni kidogo sana.

 

  1. Mbegu Kidogo Hutoka Kuliko Unavyofikiri

 

Kiwango cha manii kinachotolewa na mwanaume wakati wa kufika kileleni huwa kati ya milimita 2-5, ambacho sawa na ujazo wa kijiko 1 cha chai. Lakini utashitushwa utakapofahamu kuwa kuna takribani ya mbegu milioni 15-200 katika kiwango cha shahawa(mbegu) ulizotoa baada ya kufika kileleni.

  1. Ubora Wa Mbegu Za Mwanaume Hubadirika Kutokana Na Umri

 

Wanaume wanaweza kutoa shahawa au mbegu maishani mwao mwote lakini sio mara zote kuwa ni bora kuliko. Kutokana na utafiti inaonyesha kwamba, shahawa au mbegu wanazotoa wanaume wenye umri wa miaka zaidi ya 52 zinaonyesha kuwa sio nzuri sana kama zilizvyo shahawa za vijana wenye umri mdogo. Uzarishaji wa mbegu kwa mwanaume huwa ni mkubwa sana pale anapokuwa na umri kuanzia miaka 20. Na Uzarishaji nao unaweza kuanza kupungua taratibu pale anapovuka umri wa miaka 20.

 

  1. Ute Unaomtoka Mwanaume Anapokuwa Na Nyege Sana Huwa Ni Tofauti

 

Uteute huo huwa hauna mbegu ndani yake. Utafiti unaonyesha kwamba uteute unaotoka kwenye uume pale mwanaume anapokuwa amedindisha akiwa amepandwa na hisia kubwa au hamu ya tendo la ndoa, huwa hauna mbegu hata kidogo ndani yake. Mbegu zinazoonekana humo huwa hazina uwezo wa kutembea au kuogelea. Uteute huu haumfanyi mwanamke kuwa mjamzito. Kazi ya uteute huo huwa ni kama kilainishio cha asili pale uume unapoingia ukeni. Uteute huu huzarishwa na tezi zinazoitwa “Cowper”.

 

  1. Manii Huzifanya Mbegu Ziweze Kudumu Kwa Muda Mrefu

 

Mbegu za mwanaume zinaweza kuishi kwa muda wa siku 5 ndani ya uke wa mwanamke, huku zikisubiri kurutubisha yai mara tu lipojitokeza. Lakini manii haziwezi kudumu kwa muda mrefu huku zikiwa nje ya mwili. Kama zikiwekwa kwenye maji vuguvugu, zinaweza kukaa kwa dakika chahche tu kisha zinakufa. Lakini kama zikiwekwa hewani au sehemu yoyote ngumu, basi zinaweza kuishi mpaka zinakauka kabisa.

 

Nipende kuishia hapa ndugu msomaji, na karibu sana katika darasa letu la kila siku kupitia mtandao wa TELEGRAM na WHATSSAP.

 

Je, Unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712 181 626,

 

Arusha-Mbauda.

Unahitaji kujiunga na darasa, unaweza kutuma namba yako ya WHATSSAP katika makala hii.

 

Karibuni sana!

9 thoughts on “ZIJUE TOFAUTI ZA MANII NA SHAHAWA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *