JE, JINSI GANI MIRIJA YA UZAZI ILIYOZIBA INAVYOATHIRI UWEZO WA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO?.

Unaweza kusikia watu wakizungumzia mirija iliyoziba pale wanapoelezea matatizo yao ya kutokupata ujauzito. Kama sehemu ya mwisho ya mrija wa uzazi ikiziba au kama mrija wa uzazi ukijaa majimaji kwa ndani, basi kitaalamu tunaita, “hydrosalpinx,” hali ambayo mara nyingi hupimwa kwa kufanyiwa uchunguzi mwanamke kama ana uwezo wa kupata ujauzito.

NUKUU: Ingawa baadhi ya wanawake hupatwa na dalili za kujaa majimaji kwa mirija, lakini wengine  hujifunza tu kuwa kuna tatizo pale wanapofanyiwa uchunguzi kama matokeo ya matatizo ya kutokupata ujauzito. Kama ukipenda kujifunza juu ya hali hii, na jinsi inavyoathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito, basi endelea kusoma makala hii.

Je, Nini Maana Ya Hydrosalpinx?

Mirija ya uzazi pia hufahamika kama salpinges. Neno hydrosalpinx hutumika kuelezea mirija iliyojaa majimaji hali ambayo hutokana na kuziba kwa sehemu ya mwisho ya mrija wa uzazi. Hali ya kujaa kwa majimaji kwenye mrija wa uzazi inaweza kusababisha maumivu ya tumbo au kutokwa na uchafu ukeni usiokuwa wa kawaida, lakini ni vigumu sana mwanamke kutambua kuwa ana tatizo hilo mpaka pale atakapofanyiwa uchunguzi katika tumbo lake la uzazi ya kwamba kwanini hapati ujauzito.

Je, Hali Ya Kujaa Majimaji Kwenye Mirija Inaweza Kuathiri Vipi Uwezo Wa Mwanamke Kupata Ujauzito?

Wakati wa yai kupevuka, kifuko cha yai huachilia yai ambalo hudakwa na vidole vya mrija wa uzazi ulio wazi na kuanza kusafiri ndani ya mrija wa uzazi na kushuka chini mpaka kwenye tumbo la uzazi ambapo linaweza kurutubishwa. Kama mirija ikiziba, basi huwa ni vigumu yai kusafiri na hivyo kusababisha matatizo ya uzazi.

Je, Ni Mambo Gani Hatarishi Yatokanayo Na Mirija Ya Uzazi Kujaa Majimaji?
Ingawa mtu yeyote anaweza akapatwa na tatizo hili, ni kawaida kabisa kwa wanawake kupatwa na tatizo hili ikiwa kama waliwahi kupatwa na magonjwa haya yafuatayo;
·        Endometriosis
·        Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
·        Maambukizi katika via vya uzazi au PID
·        Upasuaji katika nyonga

 

Je, Hali Ya Mirija Kujaa Majimaji Hupimwa Vipi?

Zipo njia mbalimbali nyingi ambapo vipimo vinaweza kufanyika, nazo ni kama ifuatavyo;
·        Vipimo vya Ultrasound
·        Vipimo vya Hysterosalpingogram(HSG)
 
·        Kipimo cha Laparoscopy

 

Dalili za mirija kujaa majimaji kwa kawaida huwa kama ifuatavyo:

  • Maumivu ya tumbo la chini
  • Maumivu ya nyonga
  • Kutokwa na uchafu ukeni usio wa kawaida

 

TIBA ZAKE

 

James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya vivimbe katika mfumo wa uzazi wa mwanamke, nazo ni REDEEMER, FRESH HERB na VITAMAKA.

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626,

Pia James Herbal tunatoa masomo kwa njia ya TELEGRAM na WHATSSAP, unahitaji kujiunga na darasa letu la kila siku, basi unaweza kutuma namba yako ya WHATSSAP ukaunganishwa na darasa letu.

 

Karibuni sana

2 thoughts on “JE, JINSI GANI MIRIJA YA UZAZI ILIYOZIBA INAVYOATHIRI UWEZO WA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO?.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *