FAHAMU KABISA KWAMBA VIVIMBE KWENYE VIFUKO VYA MAYAI VINAWEZA KUSABABISHA UGUMBA KWA MWANAMKE.

Baadhi ya vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) vinaweza kuambatana na kupungua kwa uwezo wa kupata ujauzito.Hata hivyo, hutegemeana na aina ya uvimbe ulionao kwenye kifuko cha yai.

Vivimbe Vya Mayai Kwenye Kifuko Cha Yai Vinavyoweza Kuathiri Uwezo Wa Kupata Ujauzito Ni Pamoja Na:

  1. Endometriomas

 

Hivi ni vivimbe vinavyosababishwa na endometriosis, hali ambayo tishu zinazokuwa ndani ya ukuta wa mfuko wa uzazi(endometrium) huota na kutokeza nje ya mfuko wa uzazi(uterus).

NUKUU: Vivimbe hivi kwenye vifuko vya mayai vinaweza kuambatana na matatizo ya uzazi.

  1. Vivimbe Vingi Kwenye Kifuko Cha Mayai(Polycstic Ovary Syndrome)

 

Polycystic ovary syndrome ni hali inayojitokeza kwenye vifuko vya mayai yenye vivimbe vingi vidogo vidogo, vipindi vya hedhi kubadirika pamoja na viwango mbalimbali vya homoni kupanda juu.

NUKUU: Vivimbe vingi kwenye vifuko vya mayai huambatana na hali mayai kutokupevuka kila mwezi, hali ambayo inaweza kuchangia matatizo ya kutokupata ujauzito kwa baadhi ya wanawake.

Je, Ni Aina Gani Za Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai Ambavyo Haviathiri Uwezo Wa Mwanamke Kupata Ujauzito?

Aina za vivimbe kwenye vifuko vya mayai ambavyo haviathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito ni kama ifuatavyo:

  1. Uvimbe Wenye Majimaji Kwa Ndani(Functional cyst)

 

Je, Functional Cyst Ni Nini?

Huu ni uvimbe wenye ngozi nyembamba unaokuwa na majimaji kwa ndani ambao hujijenga juu ya kifuko(ovary) cha yai la mwanamke wakati au baada yai kupevuka. Uvimbe huu huzuia yai lililokomaa. Kwa kawaida uvimbe huu hutoweka baada ya yai kuachiliwa. Kama yai lisipoachiliwa, au kama uvimbe ukisogea kabla yai halijaachiliwa, basi uvimbe huu hutuna sana ukiwa umejaa majimaji kwa ndani.

NUKUU: Uvimbe huu hujengeka wakati wa mzunguko wa kawaida wa hedhi, wala hausababishi au kuchangia kuwepo kwa hali ya kutokupata ujauzito. Kusema kweli, uvimbe huu huashiria kwamba kazi muhimu zinazomfanya mwanamke kupata ujauzito kuwa zinafanyika.

  1. Uvimbe Aina Ya Cystadenomas Kwenye Vifuko Vya Mayai:

 

Hivi ni vivimbe vinavyojitokeza juu ya vifuko vya mayai. Ingawa ni vivimbe vinavyohitaji matibabu, lakini haviwezi kuathiri uwezo wa mwanamke kupata ujauzito.

  1. Vivimbe Aina Ya Dermoid Cyst

 

Vivimbe hivi vigumu huwa vina tishu au nyama nyama, kama vile ngozi, nywele badala ya majimaji. Uvimbe huu haumbatani na hali ya kutokupata ujauzito. Kama ukipima vifuko vya mayai na ukaonekana kuwa unakaribia kupata ujauzito, yafaa uongee na daktari wako. Daktari atakuelekeza dawa ya kutumia inayoweza kuboresha uwezo wako wa kupata ujauzito.

  1. Vivimbe Aina Ya Dermoid Cyst

 

Vivimbe hivi vigumu huwa vina tishu au nyama nyama, kama vile ngozi, nywele badala ya majimaji. Uvimbe huu haumbatani na hali ya kutokupata ujauzito. Kama ukipima vifuko vya mayai na ukaonekana kuwa unakaribia kupata ujauzito, yafaa uongee na daktari wako. Daktari atakuelekeza dawa ya kutumia inayoweza kuboresha uwezo wako wa kupata ujauzito.

 

Je, Unahitaji Huduma?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa visababishi vya vivimbe kwenye vifuko vya mayai.

Kwa mawasiliano tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626-Arusha Mbauda.

Pia kama unahitaji kuwa katika darasa letu la afya, basi unaweza kutuma namba yako ya WHATASAP au TELEGRAM ili tukuunganishe na JUKWAA(GROUP) letu uweze kujifunza masomo ya afya.

 

Neno La Kufariji: Msiogope enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. Luka 12:32

 

Karibuni sana wapendwa, na Mungu awabariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *