JE, NINI MAANA YA UKE KUWA MKAVU?

Ukavu wa uke huwa ni dalili za maumivu yanayoathiri ubora wa maisha ya mtu. Unaweza kusababisha maumivu wakati unakaa, au unafanya mazoezi au unapokojoa na hata wakati unapofanya tendo la ndoa. Kwa kawaida, sehemu ya ndani ya uke huwa ni yeneye unyevunyevu wenye majimaji yanayosaidia kuufanya uke uweze kuvutika.

Vaginal dryness: 'Women, please report symptoms,' urge experts

NUKUU: Ukavu wa uke hutokea pale tishu zinazokuwa ukeni zinapokauka, na hazina unyevunyevu kabisa. Hali hii hupelekea mwanamke kuwa na masumbufu, hasa anapokuwa akishiriki tendo la ndoa.

Hali ya uke kuwa mkavu hutokea katika umri wowote. Ni hali ya kawaida kwa wanawake au watu waliofikia katika ukomo wa hedhi pale viwango vya homoni ya estrogen vinapopugua. Homoni ya estrogen husaidia kuufanya uke kuwa na unyevunyevu na wenye afya. Kiwango kidogo cha homoni ya estrogen husababisha kuta za uke kuwa nyembamba na kavu. Hii ni hali ya kawaida kwa wanawake waliofikia umri wa kukoma hedhi.

Lakini matibabu ya asili yapo kwa ajili ya uke unapokuwa mkavu.

Je, Nini Husababisha Uke Kuwa Mkavu?

Kama nilivyoeleza hapo awali kwamba, hali ya uke kuwa mkavu hutokea pale kiwango cha homoni ya estrogen kinapopungua. Hii hutokea kwa asili kabisa kulingana na umri wako au unapofikia ukomo wa hedhi.

Kukoma hedhi ni pale vipindi vyako vya hedhi vinapokoma na huwezi kuwa mjamzito tena. Wakati homoni ya estrogen inapopungua, ngozi na tishu za mashavu ya uke huwa nyembamba mno na huvutika kidogo sana, na uke wako unaweza kuwa mkavu.

8 Possible Causes of Vaginal Dryness and What Could Happen If You Don't  Treat It

NUKUU: Magonjwa mbalimbali au madawa kwa ajili ya kutibu magonjwa yanaweza pia kusababisha uke kuwa mkavu. Hali ya uke kuwa mkavu inaweza kutokana na mambo  haya yafuatayo:

  • Kunyonyesha
  • Utumiaji wa madawa ya uzazi wa mpango
  • Kisukari
  • Kuondolewa kwa vifuko vya mayai au kufungwa kwa mirija ya uzazi
  • Kukosa kinga mwilini
  • Kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa
  • Utumiaji wa sabuni ukeni zenye marashi makali

Je, Uke Unakuwaje Pale Unaposhiriki Tendo La Ndoa?

Ukavu wa uke mara nyingi huwa wazi dhahiri kabisa wakati uume unapoingia ukeni. Pasipokuwa na uteute wa kutosha ukeni, basi michubuko ukeni wakati wa tendo la ndoa inaweza kusababisha masumbufu kwa mwanamke.

Intercourse Shouldn't Be Painful: The Well for Health: Health and Wellness  Center

NUKUU: Hakikisha unachukua muda wa kuamsha hisia za tendo la ndoa ili ute upatikane. Fanya kuchezacheza na kushikashika kisimi unapokuwa na mwenzi wako, hii inaweza kukusaidia pia kuamsha hisia na kuleta ute ukeni. Kwa bahati mbaya, maumivu makali wakati wa tendo la ndoa hupelekea mwanamke kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa na kumchukia mwenzie.

Je, Uke Mkavu Unaonekanaje?

Ukavu wa uke husababisha maumivu na masumbufu ukeni mwako, hasa wakati wa tendo la ndoa. Uke mkavu unaweza pia kusababisha mambo haya yafuatayo;

  • Kuhisi muwasho ukeni au hali ya kuwaka moto
  • Kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa kwasababu michubuko
  • Vidonda kwenye mashavu ya uke
  • UTI ya kujirudiarudia au fangasi ya muda mrefu
  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa kabisa.

3 Herbs for Vaginal Dryness Examined by Science - Chiavaye

NUKUU:Uteute mchache ukeni husababisha unyevunyevu kukosekana kwenye mashavu ya uke. Hii inamaanisha kwamba unaweza kujisikia ukavu au muwasho wakati unapovaa nguo ya ndani au unapotembea au unapokaa.

Je, Tatizo La Uke Kuwa Mkavu Linapimwaje?

Madaktari hupima hali ya ukavu ukeni kwa kufuatilia historia ya tatizo lako. Ili kupata chanzo cha tatizo hili, daktari atakuuliza juu ya dalili na madawa uliyoliyokuwa ukitumia. Madaktari wanaweza kufanya vipimo vifuatavyo:

  • Kupima via vya nyonga ili kuona matatizo yaliyomo ndani
  • Kipimo cha damu ili kubaini viwango vya homoni au magonjwa mengine
  • Uchafu unaotoka ukeni mwako.

Napenda niishie hapa katika makala yetu, tutaonana kipindi kijacho. Niwakaribishe tu wote wenye maswali na maoni, karibuni sana.

Je, Unahitaji huduma? Wasiliana nasi katika namba hizi: 0752389252/0712181626.

Pia James Herbal Clinic tuna darasa letu zuri katika WHATSAP, unaweza ukatuma namba yako tu na ukaunganishwa na darasa hilo ili uweze kujifunza kwa uendelevu maswala ya afya.

Karibuni san!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *