PID inaweza kumfanya mwanamke kupata ujauzito kwa shida sana, na mwanamke 1 kati ya wanawake 10, anaweza kuwa mgumba kabisa kutokana na maambukizi hayo. Bakteria ambao huenea hata kufika kwenye mirija ya uzazi wanaweza kupelekea kuwapo uvimbe ambao husababisha makovu kujengeka. Na makovu hayo yanaweza kuunda vizuizi kwenye mirija ya uzazi ambavyo hufanya mbegu na yai kuwa vigumu kukutana.
NUKUU: Hata tishu kidogo tu za kovu zinaweza kufanya kuwa vigumu mwanamke kupata ujauzito. Lakini wanawake wengi wenye tatizo la PID bado wanaweza kupata ujauzito kwa msaada wa matibabu hasa ya dawa za asili.
PID kwa kawaida huwa haionekani haraka, na ndio maana dalili zake zinaweza kumsumbua muhusika kwa muda mrefu akifuatilia vipimo lakini asitambue kwa urahisi. Dalili zake zinaweza kuwa kidogo tu lakini kadiri ugonjwa unavyozidi kujirudia mara kwa mara, ndipo unaweza kuonda dalili kama hizi zifuatazo;
- Maumivu ya tumbo la chini
- Homa au baridi
- Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu mbaya
- Kupata hedhi yenye damu nyingi kuliko kawaida
- Kupata hedhi ya muda mrefu
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa, nk
NUKUU: Dalili za PID mara nyingi huendelea taratibu, lakini pia zinaweza kutokea kwa haraka, vilevile bila kujulikana zinatoka wapi. Hata hivyo, unapaswa kufika hospitali haraka sana pindi uonapo dalili hizo. Kadiri tatizo la PID linapofanyiwa vipimo mapema na kuanzishiwa matibabu mapema bila kuchelewa, ndivyo kunakuwa na uwezekano mdogo sana wa kusababisha ugumba(kutokupata ujauzito) au matatizo mengine makubwa.
Je, Jinsi Gani Ugonjwa Wa PID Unavyoathiri Au Kuharibu Ujauzito?
PID inaweza kumfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito kwa sehemu ya kwanza. Inaweza pia kuongeza viahatarishi vya mimba kutunga nje ya kizazi, ambapo yai lililorutubishwa linapojipachika nje ya tumbo la uzazi.
NUKUU: Kovu zinazohusiana na PID zinaweza kulifanya yai lililorutubishwa lishindwe kusafiri kupita kwenye mirija ya uzazi, hivyo, badala yake linaweza kuishia kukulia ndani ya mrija wa uzazi. Mimba zinazotunga nje ya kizazi hazifai kamwe na zinaweza kumuweka mwanamke katika hatari ya kutokwa na damu nyingi.
Je, Vipi Wanaume Kuhusu Ugonjwa Wa PID?
Wanaume wanaweza kubeba bakteria wanaosababisha ugonjwa wa PID bila kuwa na dalili zozote kama vile kutokwa na uchafu kwenye uume au kuhisi maumivu wakati wa kukojoa, hivyo wanaweza kupeleka maambukizi haya kwa wenza wao pasipokujua. Lakini wanapofanya vipimo vya magonjwa ya zinaa kunaweza kuwasaidia sana.
NUKUU: Kama mwanaume ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa yanayofahamika kusababisha ugonjwa wa PID kama vile kisonono au pangusa, basi anaweza kuchukua hatua ya kujiepusha kabisa kushiriki tendo la ndoa na mwenza wake hata kama ni kwa kutumia kondom, ni vyema akaanza matibabu ili ugonjwa utoweke kabisa.
Kwahiyo naomba niishie hapa wapendwa wasomaji katika makala hii, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni kwa atakayepitia makala hii.
Lakini pia tunakukaribisha katika darasa letu endelevu katika Group la WHATSAP ambapo utapata masomo mbalimbali juu ya matatizo ya afya. Hivyo unaweza kutuma namba yako ili uweze kuunganishwa na darasa.
Unahitaji huduma au ushauri? Unaweza kuwasiliana nasi katika namba hizi: 0752389252/0712181626.
Arusha Mbauda.
Karibuni sana!