Happy Life 4 Baby ni unga safi uliotengenezwa kwa mchanganyiko wa vyakula vya asili vya nafaka, kunde pamoja na mbegumbegu. Mojawapo ya mchanganyiko wa vyakula hivi ni shayiri.
Kadiri mtoto anapofikia hatua ya kuacha kunyonya, na kuanza kula chakula kigumu, basi ni vyema kumchagulia chakula chake cha kuanza kutumia kwa uangalifu ili aweze kupata virutubisho anavyohitaji.
Pamoja na kwamba anaweza kutumia vyakula mbalimbali vya matunda na mbogamboga zilizo laini, lakini bado kuna unga safi wa lishe anaoweza kutumia mtoto vizuri kabisa kwakuwa una shayiri ndani yake.
NUKUU: Shayiri ni chakula chenye nguvu sana kwa watoto wadogo. Ni chakula kilichojaa virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwa ajili ya ukuaji wa mtoto.
Na pindi mtoto anapokuwa tayari kuanza kula chakula kigumu, anaweza kuanza kula chakula chenye mchanganyiko wa shayiri!
Lakini je, shayiri inamsaidiaje mtoto wako kukua akiwa na afya na nguvu tele? Hapa nitakupatia faida 12 za shayiri kwa mtoto wako:
1.Ina Wingi Wa Madini Ya Chuma Kwa Ajili Ya Afya Ya Ubongo
Ubongo wa mtoto pamoja na mfumo wa neva huhitaji madini ya chuma ili uweze kufanya kazi kwa ufasaha zaidi. Ili kutuma taarifa au ishara kutoka kwenye ubongo na sehemu zote za mwili, kuguswa na kuitikia mazingira baada ya ubongo kuyachakata, basi seli za neva huhitaji madini ya chuma.
Hii inamaanisha kwamba mtoto anahitaji madini ya chuma kwa ajili ya:
- Kujifunza
- Kukuza uwezo wa ubongo
- Kundeleza uwezo wa akili
- Muendelezo wa kuongea
- Utendaji kazi wote wa ubongo
Hivyo, mtoto ubongo wake hukua kwa kasi sana. Kwa bahati nzuri, shayiri ina wingi wa madini ya chuma, kwahiyo mtoto anapokunywa uji wa HAPPY LIFE 4 BABY, kwake huwa njia rahisi kupata afya ya ubongo.
2. Ina Wingi Wa Madini Ya Magnesium Yenye Nguvu
Magnesium ni madini mengine yenye nguvu sana yaliyo kwenye shayiri. Yanasaidia kazi nyingi mno kwenye mwili wa mtoto kama vile:
- Kuimarisha afya ya mifupa ya mtoto kwa kuwezesha madini ya calcium na vitamini D.
- Kufanya kazi pamoja na madini ya calcium ili kuifanya misuli iwe imara
- Kuboresha afya ya moyo
- Kusaidia mfumo kinga unapopambana na magonjwa
- Kumfanya mtoto aweze kupata usingizi mnono.
3. Ina Wingi Wa Vitamini B
Kwa nyongeza, shayiri ina vitamini B mbalimbali. Moja ya vitamini mashuhuri kabisa ni B1, pia hufahamika kitaalamu kama thiamine.
Vitamini B1 husaidia mwili wa mtoto kubadirisha wanga kwenye chakula na kuwa nishati. Pia husaidia seli kukua na kuweza kufanya kazi vizuri. Hivyo basi, husaidia pia chembechembe zenye nishati kuweza kuingia na kutoka kwenye neva na misuli ya mtoto kwakuwa chembechembe hizo zenye nishati huhitajika kwa ajili ya kuzifanya neva na misuli iweze kufanya kazi vizuri.
Vitamini B1 ina nguvu sana kwababu husaidia mifumo mingi ya mwili iweze kufanya kazi kwa ufasaha zaidi kama vile:
- Mfumo wa neva na ubongo
- Misuli
- Moyo
- Mfumo wa umeng’enyaji chakula(mfuko wa chakula pamoja na utumbo mdogo na mkubwa)
NUKUU: Pia Vitamini B1 huwa haihifadhiwi mwilini, kwahiyo mtoto anahitaji kula vyakula vyenye wingi wa vitamini B1 mara kwa mara pale anapoanza kula vyakula vigumu.
4. Husaidia Mtoto Kukua
Wote tunafahamu hatua nyingi anazopitia mtoto anapofikisha umri wa mwaka mmoja, na jinsi anavyokuwa kwa haraka.
Kama jinsi vilivyo vyakula vingine vya nafaka, Shayiri ina wingi wa madini ya magnesium yanayoboresha afya ya ukuaji wa mtoto. Protini pamoja na madini ya Zinc katika shayiri pia husaidia kuweka ukuaji wa mtoto kwenye mstari
5. Ina Wingi Wa Madini Na Vitamini Zingine Mbalimbali
Shayiri pia ni chanzo kizuri cha madini na vitamini mbalimbali, ambayo husaidia kufanya kazi muhimu mwilini.
Hapa nitatoa mfano mzuri wa vitamini na madini mengine yaliyo kwenye shayiri, na jinsi yanavyo utia nguvu mwili wa mtoto:
- Selenium: Husaidia kazi mbalimbali, ikiwa pamoja na afya ya ubongo na utendaji kazi wa mfumo kinga wa mwili,
- Phosphorus: Hufanya mifupa ya mtoto kuwa yenye afya
- Calcium: Huimarisha mifupa ya mtoto na husaidia misuli na moyo kufanya kazi kwa ufasaha
- Shaba:Husaidia katika afya ya moyo
- Zinc: Huboresha mfumo kinga wa mwili na husaidia vidonda kupona haraka
6. Ina Wingi Wa Protini
Shayiri ina protini nyingi sana kuliko vyakula vingine vya nafaka, kwa mfano ina protini inayoitwa, “Avenalin” ambayo nafaka zingine hazina.
Protini husaidia mifupa ya mtoto kuwa imara na yenye nguvu, na husaidia kurekebisha tishu za mwili ikiwa pamoja na misuli. Pia husaidia katika matengenezo yote na ukuaji wa mwili.
7. Ina Wanga Mwingi Na Mafuta Yenye Afya Bora
Shayiri ni chanzo cha ajabu sana katika nishati kwasababu ina wingi wa mafuta yenye afya pamoja na wanga mzuri. Mwili wa mtoto unatumia nishati kutokana na virutubisho hivi ili kuchochea kazi zake na kuufanya uwe imara.
8. Inamfanya Mtoto Kuyeyusha Chakula Haraka Tumboni
Shayiri ina wingi wa fiber(nyuzinyuzi), hivyo huufanya mfumo wa umeng’enyaji chakula wa mtoto kukua kwa urahisi na kuweza kuuhimili. Hiyo ndio sababu kwanini shayiri ni chaguo bora la chakula kigumu!
Mtoto atapata choo laini, wala hatasumbuka na matatizo ya bawasiri!
9. Huzuia Hali Ya Kukosa Choo Na Gesi Tumboni
Wingi wote wa nyuzinyuzi(fiber) huleta faida nyingine: haisababisha kukosa choo au kuwa na gesi tumboni. Fiber au nyuzinyuzi pia huifanya shayiri kuwa kama kilanishi fulani, na kumfanya mtoto apate choo(kinyesi) kilaini bila kuhangaika!
10. Humsaidia Mtoto Kujifahamu Anapokuwa Ameshiba
Shayiri ni njia bora inayomfanya mtoto kushiba. Inamsaidia mtoto kujisikia kushiba, hali inayoweza kumfanya kuzoea hisia hizo na kurekebisha hamu yake ya chakula.
Hii pia husaidia kumtayarisha mtoto kwa maisha yake yote ya baadaye kuwa na mazoea ya kula chakula chenye afya, kwani mtoto atakuwa na uwezo mkubwa wa kuchagua chakula hiki chenye virutubisho na kumfanya kushiba.
11. Husaidia Kuimarisha Mfumo Kinga Wa Mwili
Mfumo kinga wa mwili wa mtoto bado unaendelea kukua, na kumuacha mtoto katika hatari ya magonjwa. Kwa bahati nzuri, shayiri ina virutubisho mbalimbali vya kinga ya mwili.
Beta-glucans inayokuwa kwenye shayiri husaidia seli nyeupe za damu haraka kujibu na kushambulia maambukizi. Na Madini ya Zinc, magnesium na selenium pia husaidia kuimarisha mfumo kinga wa mwili wa mtoto.
12. Inaboresha Ulaji Wa Mtoto Kuwa Mzuri!
Inafahamika kwamba unapofahamu vyakula vizuri kama vile shayiri, na kuanza kuvitumia husaidia mwili wako kuufanya kuwa na virutubisho vingi.
Lakini kumzoesha mtoto kula chakula kilicho na mchanganyiko wa shayiri haitamfanya kuchagua chakula cha aina moja tu huko mbele katika maisha yake.
Unajua kwanini? Ni kwasababu shayiri ni chakula chenye afya kinachovitambulisha vyakula vingine vyenye afya hasa, matunda mbalimbali pamoja na mbogamboga.
Unga lishe mzuri wa HAPPY LIFE 4 BABY kutoka James Herbal Clinic umeandaliwa kwa mchanganyiko mzuri wa vyakula vya asili, kwa vipimo vizuri na mlinganyo mzuri.
Hivyo unaweza kujipatia unga huo kwa ajili ya afya ya mtoto wako mahali popote utakapokuwa!
Nipende kuishia hapa katika makala hii, niwakaribishe katika maswali na maoni yenu, tutaonana katika makala inayofuata!
Pia James Herbal Clinic tuna darasa letu katika Group La WHATSAP ambapo tunajifunza elimu ya afya kila siku, hivyo unaweza kutuma namba yako ya Whatsap ukaweza kuunganishwa na darasa letu.
Unahitaji huduma? Wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!