ZIJUE TOFAUTI KATI YA KISONONO NA KASWENDE

Je, Kisonono Nini?

Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaojulikana katika jamii. Pia ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria ambao wanaweza kuletwa na mwenzi wako kupitia uke, njia ya haja kubwa au mdomoni wakati mnapofanya tendo la ndoa.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kisonono mara nyingi huwa hakisababishi dalili. Wanawake wenye maambukizi ya kisonono wanaweza kufikiri huenda wana maambukizi ya UTI. Lakini dalili za kisonono huwa kama hivi:

  • Kutokwa na uchafu wa njano ukeni
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kukojoa
  • Kupata hedhi mara mbili wakati wa hedhi
  • Kutokwa na damu sehemu ya njia ya haja kubwa
  • Kutokwa na uchafu au kuhisi maumivu makali ukeni
  • Kutokwa na vipele vyenye muwasho ukeni.
  • Kutokwa na usaha kwenye uume

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Ugonjwa huu usipotibiwa, basi unaweza kumfanya mwanaume au mwanamke kuwa na madhara ya muda mrefu kama vile PID, pamoja na utasa.

Je, Kaswende Ni Nini?

Kaswende husababishwa na bakteria. Bakteria wanaosababisha kaswende kuingia mwilini kupitia kidonda kwenye ngozi au kujamiiana na mwenzi wako bila kinga. Kwakuwa vidonda hivi huonekana kwenye mashavu ya uke, uke, njia ya haja kubwa, au uume, kaswende mara nyingi husambazwa kwa kwa njia ya ngono. Vidonda katika sehemu za siri vilivyosababishwa na kaswende pia humfanya muhusika kuweza kupata maambukizi ya HIV kwa urahisi mno. Kaswende pia inaweza kuambukizwa kwa njia ya kugusana ikiwa kama una jeraha au kidonda.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Ugonjwa wa kaswende dalili zake hutofautiana kutokana na hatua ya ugonjwa unavyozidi kukua bila matibabu, nazo huwa kama hivi:

  1. Ugonjwa wa Kaswende ya awali(primary syphilis):

Aina hii hutokea kidonda kidogo cha mviringo ambacho bakteria wameingilia na hutokea kati ya siku 10 hadi miezi mitatu(yaani kuanzia wiki 2 hadi 6) baada ya mtu kupata maambukizi ya kaswende.

Kidonda hiki kinaweza kutokea sehemu ya njia ya haja kubwa, shingo ya kizazi(cervix), mdomoni, kwenye uume, ulimi, kwenye uke, pamoja na sehemu zingine mwilini.

NUKUU: Kwa kawaida kidonda huwa hakiambatani na maumivu na kwa kuwa kinaweza kujitokeza katika sehemu zilizojificha kama vile kwenye shingo ya kizazi, na ndio maana huwa sio rahisi mtu kutambua kuwa ana ugonjwa wa kaswende. Robo tatu ya wagonjwa wa kaswende wanaposhindwa kupata tiba mapema huishia kwenye kundi la kaswende ya hatua ya pili(second syphilis).

2. Hatua Ya Pili Ya Kaswende(Second Syphilis)

Hatua hii hutokea wiki 4-10 baada ya mtu kupata kaswende ya awali. Dalili ya aina hiyo ya kaswende huwa ni pamoja na uchovu, kuumwa kichwa, homa, kunyofoka nywele, vidonda vya koo, kuvimba kwa matezi mwili mzima, Maumivu ya mifupa au kupungua uzito.

NUKUU:  Kaswende ya aina hii huwa inakuwepo kwa wiki kadhaa na hupotea bila hata kupata tiba kwa mtu aliye athirika.  Pia inaweza kujirudiarudia katika kipindi cha mwaka mmoja na mtu huingia kwenye kundi la hatua ya ugonjwa wa kaswende iliyojificha(Latent Syphilis)

3. Kaswende Iliyojificha(Latent Syphilis):

Aina hii ya kaswende hujulikana kama kaswende ambayo inaweza kuthibitika tu kwa kutumia vipimo vya maabara(serological test). Nayo imegawanyika katika makundi mawili; (1). Kaswende iliyojicha ya awali(early latent syphilis) ambayo hutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya mwathirika kuona kaswende aina ya pili(secondary syphilis) kama nilivyoeleza hapo juu mwanzo.

NUKUU: Aina hii huwa na dalili zinazojirudiarudia  kama ilivyo kaswende aina ya pili…..Mgonjwa anapokuwa na kaswende aina hii huwa hapati dalili zozote na uwezo wake wa kuambukiza mtu mwingine unakuwa chini au hawezi kumwambukiza mtu mwingine ugonjwa huo.

4. Kaswede Ya Baadaye(Tertiary syphilis):

Asilimia ya wagonjwa wa kaswende ambao hawakupata tiba hapo awali huingia kwenye kundi hili kuanzia miaka 15-30 baada ya maambukizi ya kaswende hapo awali. Aina hii inaweza kuathiri viungo vya mwili kama vile macho, ubongo, mishipa ya fahamu(neurosyphilis), viunganishi vya mifupa(jointi), uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu, na hivi vyote husababisha madhara makubwa kama vile, upofu wa macho, magonjwa ya moyo, magonjwa ya akili, kuwa kiziwi, kupungukiwa kumbukumbu na hatimaye kifo. NUKUU: Aina hii ya kaswende pia inaweza kuathiri mfumo wa usagaji chakula, mfumo wa upumuaji, na mfumo wa uzazi.

5. Kaswende Ya Kurithiri(Congenital Syphilis):

Aina hii ya kaswende hutokea baada ya ujauzito au baada ya mtoto kuzaliwa. Robo mbili ya watoto wanaozaliwa huwa hawaonyeshi dalili zozote. Nusu ya watoto wenye maambukizi ya kaswende hufariki muda mfupi kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa. Dalili za aina hii ya kaswede kwa mtoto mchanga zinaweza kutokea baada ya kuzaliwa au wiki 2 hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa, nazo huwa kama ifuatavyo:

  • Kushindwa kukaa ama kupungua uzito
  • Kuhisi homa
  • Kupatwa na hasira haraka
  • Kutochongoka kwa pua au pua kuwa bapa.
  • Kupatwa na vipele mdomoni, sehemu za siri au njia ya haja kubwa
  • Kutokwa na majimaji puani
  • Ini au bandama kuwa kubwa
  • Ngozi kuwa ya njano na kupatwa na upungufu wa damu mwilini.

Dalili za ugonjwa wa kaswende kwa mtoto mkubwa huwa zipo ni nyingi nazo huwa ni kama hivi ifuatavyo:

  • Kuathirika kwa meno,
  • Maumivu ya mifupa,
  • Upofu wa macho,
  • Kupungua kwa uwezo wa kusikia ama kuwa kiziwi.
  • Kupatwa na ukungu kwenye mboni za macho,
  • Kupatwa na vidonda sehemu ya njia ya haja kubwa au sehemu ya uke,
  • Ngozi kuwa na mabaka meusi kwenye midomo, sehemu za siri au njia ya haja kubwa,
  • Maumivu kwenye mikono au miguu na kuvimba kwa viunganishi vya mifupa.

 

Nikushukuru sana ndugu msomaji wa makala hii, naomba niishie hapa nikaribishe kipindi cha maswali.

Pia tunatoa masomo yetu ya afya kupitia WHATSAP, hivyo unaweza kutuma namba yako ukaunganishwa na darasa letu.

Unahitaji huduma, basi tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Arusha-Mbauda Maua.

Karibuni sana!