Wanaume wasiokuwa na mbegu kwenye manii wana ugonjwa unaoitwa, “azoospermia”. Ni hali inayotokea kwa asilimia 1% kwa wanaume wote na asilimia 15% kwa wanaume tasa au wagumba.
Hakuna dalili halisi yoyote unayoweza kuiona, lakini huenda umekuwa ukijaribu kumpatia ujauzito mwenza wako lakini usifanikiwe, hivyo huu ugonjwa inaweza kuwa ndio chanzo.
Je, Nini Visababishi Vyake?
Unaweza ukawa na tatizo ambalo huzifanya korodani zako kushindwa kutengeneza mbegu au kusababisha mbegu kushindwa kutoka. Zipo aina tatu za ugonjwa wa kutokuwa na mbegu kwenye manii:
- Korodani Kushindwa Kuchochewa Na Homoni
Korodani zako zinaweza kuwa za kawaida kabisa, lakini mwili wako unashindwa kuchochea homoni kwa ajili ya kutengeneza mbegu. Hali hii inaweza kutokea kwasababu ya kiwango kidogo cha homoni au baada ya kupigwa miyonzi. Aina hii ya ugonjwa hutokea mara chache sana.
2. Korodani Kushindwa Kutengeneza Mbegu
Uharibifu kwenye korodani huzifanya korodani kushindwa kuetengeneza mbegu kwa kawaida. Inaweza kutokea hali hiyo kwasababu ya:
- Maambukizi kwenye mirija ya kusafirishia mbegu au mkojo
- Ugonjwa wa utotoni kama vile kuvimba kwa korodani moja au zote
- Saratani au matibabu yake kama vile miyonzi, nk
3. Mbegu Kushindwa Kutoka Kwenye Korodani
Korodani zako hutengeneza mbegu za kawaida, lakini kuna kitu fulani kinachozizuia zisitoke, kama vile;
- Kuziba kwa mirija inayobeba mbegu kutoka kwenye korodani mpaka kwenye uume. Kitaalamu tunaita, “ obstructive azoospermia.”
- Kufanyiwa upasuaji kwenye mirija inayobeba mbegu
- Mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuingia kwenye uume(retrograde ejaculation) wakati unapofika kileleni
Je, Utafahamu Vipi Kama Una Tatizo La Kukosa Mbegu Kwenye Manii?
Kama umekuwa ukijaribu kumpatia ujauzito mwenza wako lakini ukashindwa kubahatika kumpatia, basi daktari wako lazima afanye uchunguzi juu ya hali hii. Kwanza, utampatia sampuli za manii, na maabara itazipima kupitia darubini yenye nguvu kubwa. Kama matokeo yataonyesha kuwa hakuna mbegu kwenye manii kwa vipindi viwili tofauti, basi utakuwa na tatizo la kutokuwa na mbegu kwenye manii.
Daktari wako baadaye atajaribu kutafuta chanzo cha tatizo hilo. Watakupatia vipimo kamili, pia watakuulizia juu ya historia ya ugonjwa wako, na kupima damu yako ili kupima kiwango cha homoni. Kama viwango vyako vya homoni viko kawaida, daktari wako anaweza kuagiza uende ukafanye kipimo cha ultrasound ili kuona kama kuna vitu vimeziba. Kama huna hali ya kuziba kwa mirija inayobeba mbegu, basi vipimo vya uzazi vinaweza kutambua kama una una tatizo kwenye kizazi chako.
Hivyo, napenda niishie hapa mpendwa msomaji, nikaribishe kipindi cha maswali na tutaonana katika makala zijazo.
Pia tunakukaribisha kwenye darasa letu katika Group la WHATSAP ambapo utapata masomo mbalimbali ya afya, hivyo unaweza ukatuma namba yako ya Whatsap ukaweza kuunganishwa na darasa letu.
Kwa mawasiliano tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!