MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA: JE, KIZAZI HUATHIRIKAJE NA NINI HUSABABISHA?

Tendo la ndoa halipaswi kuwa na maumivu. Hata hivyo, karibia wanawake watatu kati ya wanawake wanne katika maisha yao wanaweza kupatwa na maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Maumivu wakati wa tendo la ndoa(dyspareunia) yanaweza kuingiliana na kupata ujauzito. Kwa mwanamke mmoja, maumivu wakati wa tendo la ndoa yanaweza kuashiria ugonjwa ambao unaweza kuathiri kizazi chako.  

NUKUU: Pili, maumivu wakati wa tendo la ndoa yanaweza kumfanya mwanamke kupata ujauzito kwa shida mno na hata wakati mwingine akakosa kabisa. Kama hutaweza kuvumilia maumivu wakati wa tendo la ndoa, hasa wakati wa kipindi cha yai kupevuka, hutaweza kuwa tayari kupata ujauzito. Jifunze nini kinachokuwa cha kawaida na kisichokuwa cha kawaida inapofika wakati wa maumivu wakati wa tendo la ndoa, ni magonjwa gani yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa, na nini unapaswa kufanya unapokumbana na tatizo hili.

Je, Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa Ni Jambo La Kawaida?

Usumbufu wakati mara kwa mara wakati wa tendo la ndoa unaweza kuwa ni kawaida. Kwa mfano, mara ya kwanza wakati mwanamke anapoanza kushiriki tendo la ndoa anaweza akapata baadhi ya masumbufu. Hii inaweza kuwa hivyo, kwasababu ya kutokuwa na uzoefu kwa wote wawili. Hata hivyo, wapenzi wawili wanapokutana mara ya kwanza ili kushiriki tendo la ndoa hawapaswi kuumizana.

Dhana ya kwamba tendo la ndoa kwa mara ya kwanza linapaswa kuwa na maumivu na kutokwa na damu kwa kawaida sio sahihi. Kumbuka hata kama ni mara ya kwanza ndio umeanza kukutana na mwanaume ili kushiriki tendo la ndoa unaweza kujisikia raha kabisa.

Sababu nyingine ya kushiriki tendo la ndoa kwa maumivu makali ni kushiriki tendo la ndoa kwa mtindo au style isiyofaa. Mitindo au style inayoruhusu uume kuzama kwa kina inaweza kupelekea shingo au mlango wa kizazi kuguswa, hali ambayo inaweza kusababisha maumivu. Kubadirisha sytle au kuachana na style mojawapo inaweza kutatua tatizo hili kwa urahisi. Kwa mfano, style nzuri ya mwanamke wakati anaposhiriki tendo la ndoa humruhusu yeye aweze kujiongoza na uume unapoingia.

Chanzo kingine kinachomfanya mwanamke kuwa na masumbufu wakati wa tendo la ndoa ni pale anapokuwa hajaandaliwa vizuri. Viungo vya uzazi kwa kawaida husisimka wakati mwanamke anapopandwa na nyege. Shingo ya kizazi hupanda na kushuka pale unapogeuzwa, nah ii hali ya shingo ya kizazi kupanda na kushuka humfanya mwanamke kujisikia raha anapofanya tendo la ndoa.

Maumivu yanayokuzuia usijisikie raha wakati wa tendo la ndoa ni ishara ya matatizo katika kizazi chako.

Je, Chanzo Cha Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa Ni Nini?

Maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa yanaweza kuwa ni dalili za magonjwa. Baadhi ya magonjwa hayo yanaweza kuathiri kizazi au kukufanya ushindwe kabisa kupata ujauizto.

Kuna sababu nyingi mbalimbali za maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa ambazo pia zinaweza kuathiri kizazi chako, nazo ni kama hizi zifuatazo:

  • Michubuko kwenye ndani ya tumbo la uzazi
  • Vivimbe kwenye kizazi
  • Uvimbe wa fibroid kwenye kizazi
  • Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID
  • Uke kuwa mkavu

Je, Inakuwaje Wakati Maumivu Makali Wakati Wa Tendo La Ndoa Yanapofanya Mwanamke Kushindwa Kupata Ujauzito?

Wakati mwingine, chanzo cha maumivu wakati wa tendo la ndoa, huwa haiathiri kizazi moja kwa moja, bali ukweli kwamba maumivu ya tendo la ndoa humfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito. Mwanamke anapata maumivu wakati wa tendo la ndoa katika sehemu mbili, kwanza kwenye mashavu ya uke, pili kwenye maeneo ya mlango wa uke. Maumivu yanaweza kuwepo muda wote, wakati mwingine, au wakati anapoguswa tu.

Ndugu msomaji makali yetu inaishia hapa, tutaonana katika makala ijayo. Nikaribishe kipindi cha maswali na maoni.

Pia unaweza ukatuma namba yako ya Whatsap ukaweza kuunganishwa ili uweze kuendelea kujifunza masomo yetu mazuri ya afya katika Group letu la WHATSAP.

Unahitaji huduma, unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda.

Karibuni sana.