Vivimbe vyote katika ya fibroid na ovarian cysts huwa ni kawaida kwa wanawake, hasa kabla ya kukoma hedhi.
Vivimbe kwenye mfuko wa uzazi huwa ni aina uvimbe mgumu ambao hujengeka kwenye msuli wa ukuta wa tumbo la uzazi(uterus). Kinyume chake, vivimbe maji kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) huwa ni vifuko vyenye majimaji ambavyo huendelea kukua ndani au juu ya vifuko vya mayai.

NUKUU: Na licha ya kutokea sehemu mbalimbali, dalili pekee zinaweza kukuacha ukashangaa kitu gani kibaya.
Hebu tuangalie mifano yake na tofauti kati ya vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids) na vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts). Tutaelezea pia kwanini ni muhimu sana kufanya vipimo.
Je, Dalili Za Uvimbe Wa Fibroid Na Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai Zinakuwaje?
Vivimbe vya fibroid na ovaria cysts mara nyingi huwa havisababishi dalili. Unaweza usitambue kama una vivimbe hivyo mpaka pale daktari akivigundua wakati atakapofanya vipimo. Kwa upande mwingine, kama una vivimbe vingi, au kama ni vikubwa, basi vinaweza kusababisha dalili nyingi.
Dalili Za Fibroid
Vivimbe kwenye tumbo la uzazi vinaweza kuwa vidogo kama mbegu za apple, au vinaweza kuwa vikubwa kama mzabibu. Dalili zinaweza kuwa kama hivi;
- Maumivu ya nyonga
- Tumbo la chini kuwa kubwa
- Kutokwa na damu nyingi ya hedhi
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Njia ya haja kubwa kubana
- Tumbo kuwa kubwa.
Uvimbe wa fibroid unaweza kuwa mkubwa mwanamke anapokuwa mjamzito na huonekana kusinyaa baada ya hedhi kukoma au kama utatumia dawa za asili kwa ajili ya kuondoa uvimbe huo.
Dalili Za Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai(Ovarian Cysts)
Vivimbe kwenye vifuko vya mayai hutofautiana ukubwa wake, lakini mara nyingi huwa ni nusu inchi hadi inchi 4 au vinawenaweza kuwa vikubwa zaidi na vinaweza kusababisha:
- Maumivu kupenya kwenye tumbo la chini, mara nyingi sehemu moja
- Tumbo la chini kuwa kubwa
- Maumivu kiunoni au kwenye mapaja
- Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
- Maumivu wakati wa hedhi
- Matiti kuuma
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara au hata huna mkojo
- Kutokwa na damu ukeni isiyo ya kawaida
- Matatizo katika njia ya haja kubwa
- Uzito wa mwili kuwa mkubwa
Uvimbe kwenye kifuko cha mayai unaweza kupasuka au kusababisha kifuko kujisokota kwenye umbo lake na kupelekea:
- Maumivu makali ya ghafla tumboni
- Homa au kutapika
- Kuhisi kizunguzungu au kuzimia
- Kupumua haraka haraka
- Kutokwa na damu nyingi ya hedhi.
Vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids) na vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) vinaweza kusababisha maumivu ya nyonga pamoja na tumbo la chini kuwa kubwa. Dalili mbili muhimu zinaweza kutoa ishara za aina moja ya uvimbe unaweza kuwa nao. Kwanza kabisa, maumivu kwenye tumbo la chini upande mmoja tu unaweza kusababishwa na vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) kuliko vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids). Badala yake, kuwa na matatizo ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi inaweza kutokana na vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids) kuliko vivimbe kwenye mayai(ovarian cysts).
Dalili nyingi hizi zinaweza kutokana na matatizo mengine ya kiafya pia. Hii ndio maana unapofika hospitali kuonana na daktari ili kujua nini kinasababisha, ni jambo jema mno kuliko kukaa na tatizo muda mrefu.
Je, Nini Husababisha Uvimbe Kwenye Tumbo La Uzazi(Fibroid) Na Kwenye Vifuko Vya Mayai(Ovarian Cysts)?
Vivimbe kwenye tumbo la uzazi au kwenye vifuko vya mayai vinaweza kutokea muda wowote. Vivimbe kwenye tumbo la uzazi kwa kawaida hutokea unapokuwa na umri wa miaka 40 hadi 50, na vinaweza kuota kwa makundi. Vivimbe vingi kwenye vifuko vya mayai huwa ni vivimbe ambavyo huendelea kwa wanawake ambao hawajafikia umri wa kukoma hedhi.
Je, Nini Husababisha Uvimbe wa Fibroid?
Inaonekana kwamba viwango vya homoni ya mwanamke vinaweza kuwa vyanzo vya tatizo hili. Na huongezeka sana baada ya kufikia umri wa miaka 30 anapokosa hedhi. Visababishi vyake ni kama hivi vifuatavyo;
- Mwanamke kufikisha umri wa miaka 28-33 bila kupata ujauzito
- Ugumba wa muda mrefu
- Matumizi ya pedi zisizokuwa na uthibitisho wa madaktari.
- Kutoa mimba
- Mapungufu ya lishe mwilini, nk.
- Mwili kuwa mnene sana
- Utumiaji wa vyakula vingi vya nyama
- Kutoshiriki tendo la ndoa muda mrefu(yaani dada ama mama anapofikia umri wa miaka 25-30 bila kushiriki tendo la ndoa)
Je, Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai(Ovarian Cysts) Husababishwa Na Nini?
Kwa kawaida visababishi vya vivimbe hivi huwa ni vingi mno navyo hutofautiana kama hivi ifuatavyo:
- Kufanya tendo la ndoa mwanamke akiwa hedhini,
- Kupungua kwa homoni ya estrogen
- Kuziba kwa mirija ya uzazi ambayo husababisha mkusanyiko wa majimaji
- Vimelea vya muda mrefu kama vile fangasi, nk.
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, pangusa, malengelenge au PID, nk.
Je, Vipimo Vya Vivimbe Kwenye Tumbo La Uzazi Au Kwenye Vifuko Vya Mayai Vinakuwaje?
Daktari anaweza kuhisi kuwa una uvimbe kwenye tumbo la uzazi au kwenye vifuko vya mayai kulingana na dalili zako pamoja na vipimo kwenye nyonga. Vipimo fulani vya kuzamisha vinaweza kutoa taarifa zaidi, endapo kama tumbo la chini linakuwa kubwa na hasa popote uvimbe ulipo. Vipimo hivi vinaweza kuwa kama hivi vifuatavyo:
- Kipimo cha kupima tumbo la chini(Abdominal Ultrasound)
- Kipimo cha kuzamisha ukeni(Transvaginal Ultrasound)
- MRI
Kama vivimbe hivi vikiwa ndani au juu ukuta wa tumbo la uzazi, vinaweza kuwa ni fibroid, ambavyo pia huitwa, “myomas au leiomyomas.”
Kama kuna uvimbe kwenye kwenye vifuko vya mayai, inaweza kuwa ni uvimbe maji. Kipimo cha ultrasound kinachozamishwa ukeni kinaweza kusaidia kubaini kama uvimbe ni mgumu au umejaa majimaji.
Ndugu msomaji naomba niishie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, tutaonana katika makala zijazo.
Pia unaweza kuungana nasi katika Group La WHATSAP ili uweze kupata masomo ya afya muda wote. Unahitaji kuungana nasi, tuma namba yako ya Whatsap ili uunganishwe na darasa.
Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626,
Arusha-Mbauda