ZIJUE SABABU 7 ZINAZOMFANYA MWANAMKE KUCHELEWE KUPATA HEDHI NA KUMFANYA ASHINDWE KUPATA UJAUZITO.

Wakati mwingine kipindi cha hedhi kinapochelewa, humfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito. Zipo sababu nyingi zinazopelekea kipindi cha hedhi kuchelewa, ikiwa pamoja na kutokuwa na uwiano sawa wa vichocheo(hormonal imbalance) au mabadiriko katika taratibu zako za mazoezi.

Vipindi vya hedhi vya  kucheleweshwa vinaweza kuwa na shida na wakati mwingine  hupelekea wanawake kuamini kwamba wana ujauzito. Lakini kipindi cha hedhi kikichelewa kinaweza kusababishwa na mambo mengi yasiyohusiana na ujauzito.

 
NUKUU: Kwa namna nyingine, kipindi cha hedhi kinapochelewa  inaweza kuwa ni ishara ya maradhi mengine ya kiafya. Kwakweli kama kipindi cha hedhi kikichelewa kinakufanya wewe ufanye utaratibu wa kufika hospitali haraka ili uweze kupata vipimo.
 
Leo napenda kukupa sababu 7 kwanini kipindi chako cha hedhi kinachelewa? Fuatilia vizuri somo hili ujue sababu zinazomfanya mwanamke kuchelewa kupata hedhi.
 
2.   Una Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai
 
Mwanamke anapokuwa na tatizo la vivimbe kwenye vifuo vya mayai, mayai yake wakati mwingine hushindwa kuendelea kukua. Hii ni kwasababu hali husababisha kutokuwa na uwiano sawa wa vichocheo(hormonal imbalance) ambayo huharibu vifuko vya mayai. Kama matokeo, basi yai kupevuka na hedhi vyote vinaweza kucheleweshwa.
 
Mbali na vipindi vya hedhi kubadirikabadirika, ishara au dalili zingine za kawaida za vivimbe kwenye vifuko vya mayai ni pamoja na chunusi, nywele kunyonyoka na mwili kuwa mzito au kuwa mnene. Maradhi haya yana tiba, lakini utakapotumia tiba za asili ili kurekebisha vipindi vya hedhi, tatizo hutoweka.
 
Inafaa sana kufanya uchunguzi na vipimo hospitali ikiwa kama unaonyesha dalili zozote kama nilizotaja hapo juu.

3. Uzito Wako Umekuwa Ukibadirika

Vifuko vya mayai pamoja na seli za mafuta mwilini pote huzarisha homoni ya estrogen. Hii inamaanisha kuongezeka au kupungua kwa ghafla kwa uzito kunaweza kubadirisha kipindi chako cha hedhi.

Pia vipindi vya hedhi kubadirikabadirika huenea zaidi kwa wanawake wanene sana au wembamba sana.

4. Kukosa Usingizi

Miili yetu huhitaji usingizi kwasababu nyingi mbalimbali ikiwa pamoja na kurekebisha joto letu na kuhakikisha viungo vyetu vya mwili vinafanya kazi kwa kawaida kabisa. Kwakuwa mfuko wa uzazi wenye ni kiungo, basi inaonyesha kwamba hali ya kukosa usingizi kunaweza kuharibu utendaji kazi wake.

5. Utumiaji Wa Madawa Ya Mpango Wa Uzazi

Unapotumia madawa ya mpango wa uzazi pasipofuata ushauri wa daktari wako, kunaweza kusababisha kipindi cha hedhi kuchelewa au kukosa hedhi kabisa.

Hata hivyo, ikiwa kama kipindi chako cha hedhi kitachelewa zaidi ya wiki 1 na ulikuwa umetumia mpango wa uzazi, basi unashauriwa ufike hospitali haraka ili uweze kupata ushauri na vipimo kutoka kwa daktari wako.

6. Kukoma Hedhi Kabla Ya Muda Wako

Moja ya dalili za kukoma hedhi ni kutokuona kabisa mzunguko wa hedhi kwa muda wa zaidi ya mwaka mzima. Wanawake wengi wanaopata hedhi hutarajia kwamba watapata hali ya kukoma hedhi wafikishapo umri wa miaka 40 au 50. Lakini kwa baadhi yao, hali ya kukoma hedhi hutokea mapema sana.

Kukosa hedhi huwa ni hatua za muda tu kabla hali ya kukoma hedhi kabisa haijatokea. Wakati huo, vifuko vya mayai huanza kuzarisha vichocheo kidogo vya estrogen kuliko kawaida, hali ambayo humsababisha mwanamke kupata hedhi mara chache sana au wakati mwingine kukosa hedhi mwezi mmoja au na kuendelea.

7. Kuwa Na Msongo Wa Mawazo

Kule kujisikia kuwa na msongo wa mawazo kunaweza kuchelewesha kipindi chako cha hedhi. Kwakweli, unapokuwa na mashaka au wasiwasi juu ya hedhi yako kunaweza kuongeza viwango vya msongo wa mawazo na kuchelewesha kipindi cha hedhi hata zaidi.

Kwahiyo mpendwa msomaji naomba makala yetu iishie hapa, tutakutana kipindi kijacho, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu kwa njia ya WHATSAP ili uweze kujifunza zaidi masomo yetu bora ya afya.

Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Arusha Mbauda.

Karibuni sana!