ZIJUE SABABU NYINGI ZINAZOPELEKEA WANAWAKE WENGI KUTOKUSHIKA UJAUZITO?

Mwanamke kutokushika mimba kumegawanyika katika makundi makuu mawili.

Kwanza ni hali inayoitwa “Primary infertility” ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili, kuna hali inayoitwa Sekondari infertility, hapa mwanamke anayo historia kama aliwahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa ama iliharibika.

6,770 Woman Infertility Stock Photos, Pictures & Royalty ...

NUKUU: Matatizo ya kutoshika mimba kitaalamu tunaita ‘infertility’ ama ugumba. Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu, nayo ni haya:

  • Maambukizi katika viungo vya uzazi
  • Hali duni ya lishe
  • Magonjwa sugu ambayo huathiri hali ya mfumo wa uzazi wa mwanamke.

Je, Nini Chanzo Chake?

Tatizo hili husababishwa na mambo mengi yanayomsumbua mwanamke, nayo huwa kama hivi ifuatayo:

  • Mayai kushindwa kupevuka
  • Mirija ya uzazi kuziba, kutanuka, kutunga usaha au maji
  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID
  • Mirija kufanyiwa upasuaji kutokana na mimba kutunga nje ya kizazi
  • Utoaji mimba mara nyingi
  • Magonjwa ya zinaa
  • Uvimbe kwenye mfuko wa kizazi
  • Mabadiriko ya homoni(hormonal imbalance)

Je, Mwanamke Mgumba Au Asiyeweza Kupata Ujauzito  Hupatwa Na Dalili Gani?

Kwa kawaida mwanamke mwenye hali ya ugumba au kutoshika ujauzito hupatwa na dalili kama hizi zifuatazo:

  • Kukosa hedhi ndani ya miezi kadhaa
  • Hedhi kupishana,
  • Hedhi kutoka kidogo sana,
  • Hedhi kutoka nyingi sana,
  • Maumivu makali ya tumbo wakati au kabla au baada ya hedhi
  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
  • Kutokupata hedhi au hedhi kuruka miezi au kujirudia ndani ya mwezi ×2
  • Kuhisi mara kwa mara hali ya ujauzito na kila ukipima ni negative
  • Kutopata hamasa ya tendo la ndoa (si wote)

Je, Ni Madhara Gani Anayoyapata?

Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito mara nyingi hupatwa na madhara ya kuwa na:

  • Mashaka,
  • Wasiwasi,
  • Msongo wa mawazo,
  • Amani katika ndoa kutoweka na hatimaye ndoa kuvunjika.

Understanding Grief After Abortion - South Avenue Women's Services

NUKUU: Utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija ya mayai. Matatizo ya mirija husababisha ugumba kwa kiasi kikubwa ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.

Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro  katika tabaka la ndani la kizazi ambapo linatoka kwa nje badala ya kuwa ndani. Hali hii kitaalam inaitwa ‘Endometriosis, ’ nitakujakulielezea baadaye katika makala nyingine. Sio tatizo linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini linaathiri baadhi ya wanawake. Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo na huwa makali wakati wa hedhi na kusababisha damu ya hedhi kutoka kidogokidogo, na mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.

Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki, pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambapo humuathiri mwanamke. Mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri, anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa.

Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto, kwahiyo ni vyema naye kufanyiwa uchunguzi endapo wanatafuta mtoto au ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.

Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina inaonekana mume wala mke hana tatizo, hali hii kitaalamu inaitwa ‘Unexplained infertility’

Je, Uchunguzi Unafanyikaje?

Matatizo ya ugumba yanazidi kuwa makubwa sana, nayo yanazidi kuumiza watu wanaotafuta ujauzito. Tunaziona sababu kuu za ugumba lakini pia mapungufu ya lishe mwilini nayo ni mojawapo ya visababishi.

Napenda kuwashauri tu wapendwa wasomaji wenye matatizo haya kuwa ni vyema kabisa kufanya uchunguzi kwa madaktari wa magonjwa ya kina mama na matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa au Wilaya. Yafaa sana kupata vipimo vya damu ili kuangalia homoni, pia vipimo vya Ultrasound ili kuangali mirija ya uzazi.

Ndugu msomaji, nipende kusema kwamba makala yetu inaisha hapa, hivyo nakaribisha kipindi cha maswali na maoni yako.

Je, Unahitaji Huduma?

Ikiwa wewe umeshawahi kupata vipimo na kupewa majibu, basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626.

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATASAP ukaunganishwa kwenye GROUP letu ili uweze kujifunza zaidi juu ya afya.

 

Karibuni sana!

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *