JE, UNAJUA CHANZO CHA KIKOHOZI KIKAVU? JE, NINI DALILI NA MADHARA YAKE?

Kikohozi kikavu ni kikohozi ambacho hudumu kwa muda wa wiki nane au kwa muda mrefu mara kinapompata mtu mwenye umri mkubwa, au wiki nne kwa watoto wadogo.

Chronic Cough After Covid-19 Recovery | Post Covid Centers

NUKUU: Kikohozi kikavu ni hali ambayo inapompata mtu humfanya kukereka mno. Hali ya kikohozi kikavu inaweza kumfanya muhusika akakosa usingizi kabisa na akajisikia kuwa mchovu mara ifikapo mida ya asubuhi. Hali mbaya ya kikohozi kikavu inaweza kumfanya muhusika kuhisi kichefuchefu na kutapika, kichwa kugonga na hata mbavu kuuma.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kikohozi kikavu kinaweza kujitokeza kwa dalili zingine mbalimbali ambazo huwa tofauti ambazo ni kama hizi zifuatazo:

  • Mafua mepesi
  • Kuhisi kama kitu au majimaji yanapita kooni
  • Kuhisi muwasho mara kwa mara sehemu za koo au kuwa na vidonda
  • Sauti kupweleka
  • Kushindwa kupumua vizuri
  • Kuhisi kiungulia au ladha ya uchungu fulani kinywani mwako
  • Kukohoa makohozi ya damu muda mwingine

Je, Chanzo Chake Kinakuwaje?

Hali ya kikohozi kile cha rasharasha ambacho ni cha kawaida husaidia kuondoa uchafu kwenye mapafu na kuzuia maambukizi. Hata hivyo, hali ya kikohozi kinachoendelea kwa majuma kadhaa mara nyingi huwa ni matokeo ya matatizo ya matumizi ya madawa. Wakati mwingine zinaweza kuwapo sababu nyingine zaidi kama vile:

  • Kutokwa na mafua mepesi
  • Pumu
  • Maambukizi
  • Matumizi ya madawa ya shinikizo la juu la damu

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Mtu yeyote anapokuwa na hali ya kikohozi kigumu cha muda mrefu anaweza kujihisi kuchoka sana. Lakini pia anaweza akakosa usingizi na kusababisha madhara  kama haya:

  • Kichwa kugonga sana
  • Kuhisi kizunguzungu
  • Kutokwa na jasho
  • Mkojo kupita bila kujijua
  • Mbavu kuuma

Je, Tiba Yake Inakuwaje?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri kabisa ya asili yenye uwezo mkubwa wa kuondoa hali ya kikohozi kigumu pamoja na maambukizi mbalimbali katika mfumo wa hewa, nayo ni BEST GREEN POWDER.

 

Unahitaji Huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ukaweza kuunganishwa na darasa letu ili uweze kupata masomo mbalimbali juu ya matatizo ya afya.

Karibu sana!