Kufunga kizazi, ni uzazi wa mpango wa kudumu. Wakati wa kufunga kizazi, mirija ya uzazi hukatwa, au kufungwa au kuzibwa kabisa ili kuzuia ujauzito daima.
Kufungwa kwa mirija ya uzazi huzuia yai lisiweze kusafiri kutoka kwenye vifuko vya mayai (ovaries), na huzuia mbegu za mwanaume zisisafiri na kufika mpaka kwenye mirija ya uzazi ili kulifikia yai. Nji yenyewe huwa haiathiri mzunguko wa hedhi.

NUKUU: Kufunga mirija ya uzazi kunaweza kufanyika muda wowote, hasa baada ya kujifungua au pamoja na upasuaji unapofanyika tumboni, kama vile kujifungua kwa njia ya upasuaji. Njia nyingi za kufunga mirija ya uzazi huwa hazibadirishwi. Kama ukijaribu kubadirisha, basi utahitaji upasuaji mkubwa sana na mara nyingi huwa haifai maana hakuna ufanisi wowote utakaoupata.
Je, Kwanini Njia Hii Inafanyika?
Kufunga mirija ya uzazi ni moja ya njia za kawaida zinatumiwa na wanawake kwa njia ya upasuaji. Njia ya kufunga mirija ya uzazi huzuia daima ujauzito, kwahiyo huhitaji kabisa aina yoyote ya uzazi wa mpango. Hata hivyo, njia hii haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Njia ya kufunga mirija ya uzazi pia inaweza kupunguza vihatarishi vya saratani ya vifuko vya mayai, hasa ikiwa kama mirija ya uzazi ikiondolewa.
Hata hivyo, njia ya kufunga mirija ya uzazi sio nzuri kwa kila mmoja. Ongea na daktari wako ili akueleweshe vizuri madhara na faida ya njia ya kufunga mirija ya uzazi.
Dakati wako pia anaweza kuongea na wewe juu ya njia zingine za uzazi wa mpango ikiwa pamoja na kupachika vijiti, nk.
Je, Nini Madhara Ya Kufunga Kizazi(Kufunga Mirija Ya Uzazi)?
Kufunga mirija ya uzazi ni upasuaji unaofanyika kwa kufanyiwa upasuaji maeneo ya tumbo la chini. Inahitaji ganzi. Madhara yanayoambatana na kufunga kizazi ni pamoja na:
- Uharibifu wa utumbo, kibofu cha mkojo na mishipa mikubwa ya damu
- Kuhisi maumivu
- Kidonda kutokupona vizuri au kuwa na maambukizi
- Maumivu ya nyonga au tumbo la chini yasiyokuwa na kikomo
- Kutokupata kabisa ujauzito baadaye baada ya mirija kufunguliwa
Mambo yanayokufanya uwe na madhara makubwa zaidi kutokana kufunga kizazi ni pamoja na:
- Uzito wa mwili kuwa mkubwa
- Ugonjwa wa kisukari
Je, Nini Kinachotokea Baada Ya Njia Hii Kufanyika?
Kama ni gesi ilitumika wakati wa kufunga mirija ya uzazi, basi itaondolewa baada ya mirija kufungwa. Unaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani masaa kadhaa baada ya kizazi kufungwa. Unapofungwa mirija ya uzazi haraka baada ya kujifungua kwa kawaida huwa haimfanyi muhusika akae hospitali kwa muda mrefu.
Unatapata masumbufu unapofanyiwa upasuaji. Unaweza pia kupata:
- Maumivu ya tumbo la chini
- Uchovu wa mwili
- Kizunguzungu
- Tumbo kuunguruma
- Maumivu kwenye bega
Je, Nini Matokeo Yake Baaaye?
Kufunga mirija ya uzazi ni njia salama ya uzazi wa mpango daima. Lakini njia hii huwa haifanyi kazi kwa kila mmoja. Wachache hupata ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada ya kufunga mirija ya uzazi. Njia hii inapofanyika ukiwa mdogo, kuna uwezo mkubwa mno wa yenyewe kushindwa kufanya kazi.
Kama ukipata mimba baada ya kufunga mirija ya uzazi, basi kuna hatari ya mimba kutunga nje ya mji wa mimba. Hii inamaanisha kwamba yai hujipachika nje ya mji wa mimba, mara nyingi kwenye mrija wa uzazi. Mimba kutunga nje ya kizazi huhitaji matibabu ya haraka sana. Ujauzito hauwezi kuendelea mpaka ukajifungua. Kama ukihisi muda wowote kwamba wewe ni mjamzito baada ya kizazi kufungwa, basi hakikisha unawasiliana na daktari wako haraka sana.
Kumbuka kwamba ingawa njia ya kufunga mirija ya uzazi inaweza kubadirishwa, lakini utaratibu wa kubadirisha huwa ni mgumu na hauwezi kufanyika. Kwahiyo unapaswa utakari kwanza kabla hujafanya maamuzi.
Mungu akubariki sana ndugu msomaji, ni kukaribishe kwa maswali na maoni yako.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ukaunganishwa na darasa letu la kila siku ili uweze kupata masomo mazuri ya afya na ushauri pia.
Je, Unahitaji huduma? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626.
Arusha-Mbauda Maua.
Karibu sana!