Je, Ni Kiasi Gani Hali Ya Kuchelewa Kwa Hedhi Inaweza Kuwa Jambo La Kawaida?
Wasiwasi juu ya kuchelewa kwa hedhi, lakini unafahamu kwamba wewe sio mjamzito? Kukosa hedhi au hedhi kuchelewa ni hali ambayo hutokea kutokana na sababu nyingi mbali na ujauzito. Sababu za kawaida zinaweza kuanzia na kutokuwa na uwiano sawa wa vichocheo(hormonal imbalance) na madawa makali uliyotumia.
Pia kuna nyakati mbili ambapo ni kawaida kipindi chako cha hedhi kubadirika: wakati kipindi cha hedhi kinapoanza na wakati kinapoelekea kuanza kukoma. Mwili wako unapoelekea kubadirika, mzunguko wako wa hedhi unaweza kubadirika.

NUKUU: Watu wengi ambao hawajafikia ukomo wa hedhi mara nyingi wana kipindi cha hedhi chenye mzunguko wa siku 28. Hata hivyo, mzunguko wa hedhi wenye afya unaweza kuanzia siku 21 hadi 40. Kama mzunguko wako wa hedhi haendani na siku hizo, inaweza kusababishwa na moja ya sababu hizi zifuatazo:
1.Msongo Wa Mawazo
Msongo wa mawazo wa muda mrefu unaweza kuruga homoni zako, au kubadiri utaratibu wako wa kila siku, na hata kuathiri sehemu ya ubongo wako inayohusika na kurekebisha kipindi cha mzunguko wa hedhi(yaani tezi yako ya hypothalamus). Muda mwingine, msongo wa mawazo unaweza kusababisha maradhi au uzito wa mwili kuongezeka ghafla au kupungua ghafla, ambavyo vyote hivi vinaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi.
Kama ukifikiria kwamba msongo wa mawazo unaweza kuvuruga mzunguko wako wa hedhi, basi jaribu kutumia mbinu ya kutuliza mawazo yako na ubadirishe mtindo wa maisha yako.
Msongo wa mawazo wa muda mrefu unaweza pia kuathiri mambo mengine katika maisha yako, hivyo jitahidi kushughulikia mwenyewe swala hili au pata msaada wa mtaalamu wa matibabu, ni sehemu muhimu sana ya kujipatia tahadhali katika maisha yako.
2. Mwili Kuwa Mwembamba
Watu wenye matatizo ya kula kama vile kuogopa kuwa huenda mwili utakuwa mkubwa, wanaweza kupatwa na hali mzunguko wa hedhi kubadirika. Mwili unapopungua uzito sana kunaweza kusababisha vipindi vya hedhi kubadirika, na inaweza kufanya vipindi vya hedhi vikakoma kwa pamoja. Hii ni kwababu kutokuwa na mafuta ya kutosha mwilini kunaweza kuzuia kazi ya kupevusha mayai isifanyike.
Upatapo matibabu ili kutengeneza utaratibu wako wa ulaji na mwili wako ukapata mafuta tena, kunaweza kurejesha mzunguko wako wa hedhi kama ulivyokuwa awali.
Watu wanaofanya mazoezi sana kama vile kukimbia mbio za marathon, wanaweza pia kupatwa na hali ya mzunguko wa hedhi kubadirika pia.
3. Unene
Kama tulivyoona kwamba kuwa na mwili mwembamba kunaweza kusababisha mfumo wa homoni kubadirika, vile vile kuwa na mwili mnene unaweza pia kusababisha vipindi vya hedhi kubadirika. Homoni nyingi sana ya estrogen inaweza kusababisha vipindi vya hedhi kubadirika katika mizunguko yako, na inaweza hata kufanya vipindi vya hedhi kukoma kabisa.
Kama daktari wako amebaini kuwa tatizo la unene ni jambo linaloweza kuchelewesha vipindi vya hedhi au kukosa hedhi kabisa, basi anaweza kukushauri upunguze uzito wa mwili kwa kubadiri mitindo ya maisha yako, kama vile kuzingatia vyakula vya lishe visvyokuwa na mafuta sana na pia kufanya mazoezi.
4. Vivimbe Vidogovidogo Vingi Kwenye Vifuko Vya Mayai(PCOS)
Hii huwa ni hali ambayo husababisha mwili wako kuzarisha homoni nyingi za kiume(Polycystic Ovary Syndrome). Vivimbe huota kwenye vifuko vya mayai kama matokeo ya homoni imbalansi. Hali hii inaweza kufanya vipindi vya mayai kupevuka kubadirika au vikakoma kabisa na usione mayai yamepevuka.
Homoni zingine kama vile insulin, zinaweza kukosa uwiano. Hali hii inaweza kuambatana na kuota kwa vivimbe vingi kwenye kifuko cha mayai.
Matababu kwa ajili ya tatizo hili huwa ni pamoja na kutuliza dalili. Daktari anaweza kukushauri utumie madawa ya uzazi wa mpango au madawa mengine ili kusaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi.
5. Vidonge Vya Uzazi Wa Mpango
Unaweza kuona badiriko kwenye mzunguko wako wa hedhi unapoendelea kutumia uzazi wa mpango au unapoacha kutumia uzazi wa mpango. Vidonge vya uzazi wa mpango huwa vina vichocheo vya estrogen na progestin, ambavyo huzuia vifuko vyako vya mayai visitoe mayai. Inaweza kuchukua hadi miezi mitatu kwa mizunguko yako ya hedhi kuwa sawa tena baada ya kuacha kutumia vidonge vya mpango wa uzazi.
Aina zingine za uzazi wa mpango ambazo huingizwa au kuwekwa ndani ya mwili wako zinaweza kusababisha ukakosa vipindi vya hedhi pia.
6. Magonjwa Sungu
Magonjwa sugu, kama vile kisukari na mmeng’enyo wa chakula yanaweza pia kuathiri mzunguko wako wa hedhi. Mabadiriko ya sukari kwenye damu huambatana na mabadiriko ya homoni, ingawa ni mara chache, kisukari kisichodhibitiwa kinaweza kusababisha kipindi cha hedhi kubadirika.
Ugonjwa wa umeng’enyaji wa chakula husababisha uvimbe ambao hupelekea kuharibika kwa umbo mdogo, hali ambayo inaweza kuzuia mwili wako kufyonza virutubisho muhimu. Hali hii inaweza kupelekea vipindi vya hedhi kubadiri au kukosekana kabisa.
7. Mayai Kutokukomaa
Wanawake wengi huanza kukoma hedhi kati ya miaka 45 hadi 55. Wanawake wanaopata dalili kama hizo kuanzia umri wa miaka 40 au mapema kabisa wanaweza kuwa na tatizo la mayai kutokukomaa au kukoma hedhi mapema.
Kama unakosa vipindi vya hedhi na una umri wa miaka 40 au ukiwa bado mdogo sana, basi wasiliana na JAMES HERBAL CLINIC.
8. Tatizo La Tezi Ya Thyroid
Tezi thyroid kushindwa kufanya kazi au kufanya kazi zaidi ya uwezo wake inaweza pia kuwa sababu ya hedhi kuchelewa au kukosa kabisa.
Tezi ya thyroid hurekebisha joto la mwili wako, kwahiyo viwango vya homoni vinaweza kuathiriwa pia. Matatizo ya tezi ya thyroid yanaweza kutibiwa pia kupitia tiba za asili. Baada ya matibabu mizunguko yako ya hedhi itarudi kuwa kawaida kabisa kama ilivyokuwa mwanzo.
Ndugu msomaji makala yetu inaishia hapa, nipende kukaribisha kipindi chako cha maswali na maoni.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATsAP ili uweze kuunganishwa kwenye darasa letu uweze kuzidi kujifunza zaidi juu ya magonjwa mbalimbali ya uzazi.
Je, Unahitaji Huduma?
Basi wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!
Je kama ukiumwa UTI kali inaweza kupelekea kukosa kwa hedhi?
Ndiyo inaweza kusababisha mzunguko wa hedhi kuwa mbaya zaidi