ZIJUE SABABU ZA UGONJWA SUGU WA FIGO, DALILI ZAKE, MADHARA YAKE NA TIBA ZAKE.

Ugonjwa sugu wa figo, pia unaitwa hali sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo, inahusisha figo kupoteza polepole utendaji kazi wake. Figo zako huchuja uchafu na majimaji kutoka kwenye damu, ambao huondolewa kweye mkojo wako. Ugonjwa sugu wa figo unaweza kusababisha viwango vya hatari vya majimaji, pamoja na uchafu viweze kujengeka mwilini mwako.

Chronic Kidney Disease Treatment in India | Renal Failure

Katika hatua ya awali ya ugonjwa sugu wa figo, lazima unaweza kuwa na dalili chache. Unaweza usitambue kuwa una ugonjwa wa figo mpaka pale hali itakapokuwa mbaya.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili za ugonjwa sugu wa figo hutokea muda wote ikiwa kama ikianza kuharibika polepole. Kupotea kwa uwezo wa figo kufanya kazi kunaweza kusababisha matatizo ya majimaji au uchafu mwilini. Hutegemeana na jinsi ilivyo sugu, kupotea kwa uwezo wa figo kufanya kazi kunaweza kusababisha mambo haya:

  • Kuhisi kichefuchefu
  • Kutapika
  • Kukosa hamu ya kula
  • Mwili kudhoofika na kuchoka
  • Matatizo ya kutokupata usingizi
  • Kukojoa sana au kidogo tu
  • Uwezo wa ubongo kupungua
  • Misuli kuuma
  • Miguu kuvimba
  • Ngozi kukauka, na kuwahsa
  • Shinikizo la juu la damu ambalo huwa ni vigumu kulithibiti
  • Kushindwa kupumua vizuri ikiwa majimaji yakiwa yamejaa kwenye mapafu
  • Kifua kuuma, ikiwa majimaji yakiwa yamejaa maeneo ya moyo

NUKUU: Dalili na ishara za ugonjwa wa figo mara nyingi huwa sio maalum sana. Hii inamaanisha kwamba zinaweza pia kusababishwa na maradhi mengine. Kwakuwa figo zako zipo tayari kuweza kufidia utendaji kazi uliopotea, basi unaweza usiendelee kuona dalili mpaka pale uharibifu usioweza kurekebishwa ukitokea.

Je, Muda Gani Unapaswa Kuonana Na Daktari?

Hakikisha unafika hospitali kuonana na daktari ikiwa una dalili za ugonjwa wa figo. Uchunguzi unapofanyika mapema unaweza kukusaidia kuzuia ugonjwa wa figo usiendelee na kusababisha figo ushindwe kufanya kazi.

Kama una magonjwa ambayo yanaongeza vihatarishi vya ugonjwa wa figo, basi daktari wako anaweza kuchunguza shinikizo la damu na utendaji kazi wa figo pamoja na vipimo vya mkojo na damu wakati unapofika hospitalini. Muulize daktari wako ikiwa kama vipimo hivyo ni vya muhimu sana kwako.

Je, Vyanzo Vyake Ni Nini?

Ugonjwa sugu wa figo hutokea wakati ugonjwa au hali inadhoofisha utendaji kazi wa figo, na kusababisha figo kuharibika na kuwa mbaya kwa muda wa miezi au miaka kadhaa.

Ugonjwa na maradhi ambayo yanasababsiaha ugonjwa wa figo ni pamoja na:

  • Kisukari cha kupanda na cha kushuka
  • Ugonjwa wa moyo(shinikizo la juu la damu) au presha ya kupanda
  • Kuvimba kwa kipimo cha figo kinachopima uchafu
  • Kuvimba kwa mirija ya figo
  • Vivimbe vidogovidogo kwenye figo
  • Kuziba kwa mirija ya mkojo kwa muda mrefu kutokana na maradhi kama vile kuvimba kwa tezi dume, mawe ya figo na baadhi ya magonjwa ya saratani.
  • Uvimbe ambao husababisha mkojo kurudi ndani
  • Maambukizi kwenye figo uliyoyapa muda huo(pyelonephritis).

Matibabu kwa ajili ya ugonjwa sugu wa figo huzingatia sana kupunguza kasi ya uharibifu wa figo, mara nyingi ni kudhibiti visababishi vyake. Lakini hata kudhibiti vyanzo vyake kunaweza kuzuia uharibifu wake usiendelee. Ugonjwa sugu wa figo unaweza kuendelea na kuishia kwenye figo kushindwa kufanya kazi, ambalo ni tatizo baya zaidi hata bila kutumia chujio bandia au kupachika figo bandia.

Ubarikiwe sana ndugu msomaji napenda niishie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.

Hivyo unaweza pia ukatuma namba yako ya WHATsAP tukakuunganisha na darasa letu ili uweze kujifunza zaidi masomo ya afya mbalimbali na utapata ushauri pia.

Je, Unahitaji Huduma?

Wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *