Kisonono ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria wanaoitwa Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hawa husambazwa wakati unaposhiriki tendo la ndoa kwa njia ya uke, njia ya haja kubwa au mdomo. Mwanamke mjamzito pia humuambukiza mtoto wake wakati anapojifungua.
Mtu yeyote mwenye ugonjwa wa kisonono anaweza kumuambukiza mtu hata kama hajaonyesha dalili. Tiba ni njia pekee ya kuepukana na maambukizi haya.
NUKUU: Kuwa na maambukizi ya kisonono hakuwezi kukuzuia wewe kupata maambukizi ya magonjwa mengine baadaye. Muonekano mpya wa kisonono utasababisha maambukizi kuwa yanajirudia tena. Hali hii inaweza kutokea hata kama ulitibiwa na ukapona kabla.
Je, Dalili Za Kisonono Zinakuwaje?
Ni kawaida kabisa kwa ugonjwa wa kisonono kushindwa kuonyesha dalili, hasa kwa wanawake. Kipindi cha kupevusha mayai, kuanzia muda maambukizi yanapoanza kuingia mpaka dalili zinapojitokeza, kwa kawaida huwa ni siku 5. Lakini wakati mwingine dalili zinaweza zisionekane mpaka siku 30.
Kisonono kinaweza kisisababishe dalili mpaka pale maambukizi yatakaposambaa katika maeneo mengine ya mwili. Unaweza kusambaza kisonono hata kama huna dalili. Utaendelea kuambukiza wengine tu mpaka utakapopata matibabu.
Je, Dalili Za Kisonono Kwa Wanawake Zinakuwaje?
Kwa wanawake, dalili za awali wakati mwingine huwa ni za kawaida tu ambazo unaweza kupima ikaonekana kama maambukizi kwenye njia ya mkojo, yaani UTI au maambukizi ya fangasi sehemu za siri, na mtu anahangaika muda mrefu anatumia dawa za magonjwa aliyopima akayaona na tatizo lisitibike kwasababu bado hajapata tiba za ugonjwa wenyewe uliopo. Tatizo ni kisonono lakini anatumia dawa za UTI au Fangasi sehemu za siri, nk. Bila shaka kina dada na kina mama mumenielewa ninachokielezea.
Dalili zinaweza kuwa kama hivi:
- Maumivu au kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Muwasho sehemu ya njia ya haja kubwa
- Kujisikia usumbufu mwilini
- Kutokwa na damu ukeni au uchafu
- Kutokwa na damu ukeni wakati wat endo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
- Kupata hedhi mara mbili kwa mwezi mmoja
- Kuhisi muwasho sehemu ya mashavu ya uke
- Vipindi vya hedhi kubadirika
- Kuhisi maumivu maeneo ya tumbo la chini
- Kuhisi homa
- Tezi zinazokuwa maeneo ya uke kuvimba
- Maumivu wakati wat endo la ndoa
- Vidonda kooni(japo dalili hii hutokea mara chache sana)
Je, Kwa Wanaume Dalili Zinakuwaje?
Kwa wanaume dalili mara nyingi huwa ziko wazi Zaidi. Wanaume wengi hutibiwa kabla matatizo mengine hayaanza kutokea. Lakini baadhi ya wanaume huwa na dalili kidogo tu au wasiwe na dalili kabisa. Hii inamaanisha kwamba wanaweza kuambukiza wapenzi wao na wasijue tatizo hili. Dalili zinaweza kuwa Pamoja na:
- Kutokwa na ute usio wa kawaida kwenye uume. Mwanzoni ute huu unaweza kuwa kama ute way ai au kama maziwa. Baadaye unaweza kuwa wa njano, mzito au wenye damu kidogo.
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Mrija wa mkojo kuvimba
- Kuhisi muwasho kwenye njia ya haja kubwa
- Kujisikia usumbufu mwili wote.
Je, Dalili Zingine Zinakuwaje?
Kusambaa kwa bakteria wa gonococcal hutokea pale maambukizi ya kisonono yanaposambaa kwenye maeneo mengine ya mwili. Maeneo hay ani Pamoja na maungio ya mifupa(jointi), Ngozi, moyo, au damu.
Dalili zake huwa kama hivi:
- Harara kwenye Ngozi
- Maumivu kwenye maungio ya mifupa
- Kuvimba kwa tishu za misuli
Kwa wanawake, ugonjwa wa kisonono usipotibiwa unaweza kupelewa kuwapo kwa maambukizi katika via vya uzazi(Pelvic Inflammatory Disease) au PID. Haya huwa ni maambukizi kwenye mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi(uterus), na shingo ya kizazi. Kama maambukizi hayatatibiwa, basi PID inaweza kusababisha uharibifu daima kwenye viungo vya uzazi, hali ambayo hupelekea mwanamke kuwa mgumba kabisa. Pia yanaweza kusababisha maumivu ya nyonga yasiyokuwa na mwisho.
Wanaume wenye kisonono ambacho hakijatibiwa wanaweza kuwa na ugonjwa unaoitwa epididymitis(yaani kuvimba kwa mirija midogomidogo iliyojisokota inayokuwa nyuma ya korodani ambayo kazi yake ni kubeba shahawa au mbegu za mwanaume na kuzisafirisha). Ugonjwa huu hujulikana kama kuvimba kwa mirija kwenye korodani. Dalili zake zinaweza kuwa ni kuhisi homa, maumivu kwenye korodani, na kuvimba kwa korodani.
Kwa mara chache sana, bakteria wa kisonono wanaweza kuingia kwenye mkondo wa damu na kuambukiza sehemu zingine kama vile Ngozi, maungio ya mifupa, au viungo vya ndani. Dalili zinaweza kuwa pamaoja na homa, uvimbe, maumivu kwenye maungio ya mifupa, harara na vidonda kwenye Ngozi.
Naomba niishie hapa mpendwa msomaji katika makala hii, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.
Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHAsAP ili tukuunganishe na darasa letu uweze kupata masomo ya afya kila siku.
Je, Unahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda,
Karibuni sana!