Mrija ya uzazi inaweza kupatwa na magonjwa mbalimbali na hivyo kupelekea kuvimba au kuziba. Leo nitapenda kuzungumzia juu ya kuvimba kwa mrija au mirija ya uzazi.
Kuvimba kwa mrija wa uzazi kitaalamu tunaita “salpingitis”. Karibia matatizo yote katika mfumo wa uzazi husababishwa na maambukizi ya bakteria, hususani magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na pangusa. Uvimbe husababisha kutengenezeka kwa majimaji au hata usaha na hivyo kukusanyika ndani ya mrija wa uzazi. Maambukizi kwenye mrija mmoja kwa kawaida hupelekea na mrija mwingine kupata maambukizi, kwakuwa bakteria huhama kupitia mishipa iliyokaribu na mrija mwingine.
Kuvimba kwa mrija au mirija ni moja wapo wa visababishi vya ugumba wa mwanamke. Usipofanya matibabu haraka, ugonjwa unaweza kuharibu daima mrija wako wa uzazi kiasi kwamba mayai yanayoachiliwa kila mwezi katika mzunguko wa hedhi hayataweza kuzifikia mbegu za mwanaume. Majeraha na kuziba kwa mirija ya uzazi ni madhara ya moja kwa moja yatokanayo na maambukizi ya PID. Hata hivyo ugonjwa wa PID maana yake ni kuwa na maambukizi katika mfumo wa uzazi kama vile mfuko wa uzazi Pamoja na vifuko vya mayai.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kwa hali ya wepesi, mrija kuvimba unaweza usionyeshe dalili. Hii inamaanisha mirija ya uzazi inaweza kuharibika bila mwanamke kufahamu kwamba alikuwa na maambukizi. Dalili za mrija kuvimba zinaweza kuwa kama hivi ifuatavyo:
- Kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni wenye rangi na harufu mbaya
- Kutokwa na matone ya damu ukeni mara kwa mara ndani ya mwezi mmoja
- Maumivu makali wakati wa hedhi
- Kuhisi maumivu wakati yai linapopevuka
- Kuhisi maimivu wakati wa kujamiiana
- Kuhisi homa
- Kuhisi maumivu ya tumbo la chini pande zote mbili
- Kuhisi maumivu ya kiuno
- Kukojoa mara kwa mara
- Kuhisi kichefuchefu na kutapika
- Dalili kwa kawaida huonekana baada ya kipindi cha hedhi.
Je, Kuna Aina Ngapi Za Kuvimba Kwa Mirija Ya Uzazi
Kuvimba kwa mrija kumegawanyika katika makundi mawili, mrija kuvimba papo hapo na kurudi katika hali yake ya kawaida au kuendelea kuvimba moja kwa moja. Katika kuvimba papo kwa hapo, mirija ya uzazi hubadirika na kuwa myekundu na hivyo kutuna, na hutengeneza majimaji mengi kiasi kwamba ukuta wa ndani wa mirija mara nyingi hugandamana.
Mirija inaweza pia kugandamana karibu na viungo vingine kama vile utumbo mkubwa na mdogo. Wakati mwingine mrija unaweza kufura ukatuna na kujaa usaha. Kwa nadra sana mrija hupasuka na kusababisha maambukizi kwenye tumbo la uzazi. Uvimbe sugu wa mrija wa uzazi mara nyingi hufuatia shambulia baya.
Maambukizi huwa ni ya kawaida, hukaa kwa muda mrefu na yanaweza kuonyesha dalili.
Je, Vyanzo Vyake Ni Nini?
Katika magonjwa 10 ya kuvimba kwa mirija, ugonjwa 1 unaweza kusababishwa na bakteria. Visababishi vikuu vya kuvimba kwa mrija ni Pamoja na:
- Pangusa
- Kisonono
- Mycoplasma
- Staphylococcus
- Streptococcus
NUKUU: Fahamu Madhara 6 Ya Ugonjwa Wa Pangusa (Chlamydia) Kwa Mwanamke.
Bakteria lazima wapate njia ya kupita na kuingia kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke kupitia maambukizi. Bakteria wanaweza kutambuliwa kwa njia mbalimbali ikiwa Pamoja na:
- Ngono
- Mimba kuharibika
- Kutoa mimba
- Kujifungua, nk
Je, Nini Madhara Ya Kuvimba Kwa Mrija Wa Uzazi?
Bila kufanya matibabu haraka, basi kuvimba kwa mrija wa uzazi kunaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa Pamoja na:
- Maambukizi kusambaa mpaka kwenye viungo vingine vya uzazi
- Kumuambukiza mwenzi wako
- Vifuko vya mayai kuvimba
- Mimba kutunga nje ya uzazi
- Kutokupata ujauzito kabisa.
Je, Utatumia Nini Ili Kupima Na Kujua Kuwa Mrija Umevimba?
Upimaji wa mrija uliovimba hutokana na idadi mbalimbali za vipimo ikiwa Pamoja na:
- Kupimo cha jumla ili kuona mrija uliovimba
- Kupima mambukizi ya PID
- Kupima damu
- Kupima uteute unaotoka ukeni
- Kupima mirija ya uzazi
Nipende kuishia hapa ndugu msomaji katika makala yetu hii, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana.
Pia tunakukaribisha katika Group letu la WHATsAP unaweza kutuma namba yako ya Whatsap tukakuunganisha ili uweze kujifunza masomo mbalimbali ya afya ya uzazi na magonjwa mengine.
Unahitaji kupata huduma? Basi wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626,
Arusha-Mbauda.
Karibu sana!