JE, NINI HUSABABISHA TEZI DUME KUVIMBA? NINI MADHARA YAKE?

Tezi dume ni tezi ndogo ambayo husaidia kutengeneza manii, nayo ipo chini kibofu cha mkojo. Mara nyingi tezi hii hupanuka na kubwa kadiri unavyozidi kuwa mzee.

Tezi dume iliyovimba inaweza kusababisha dalili ambazo zinaweza kukusumbua, kama vile kuziba kwa njia ya mkojo kwenye kibofu cha mkojo. Inaweza pia kusababisha matatizo ya kibofu cha mkojo, njia ya mkojo au figo.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Wagonjwa wengi wenye tatizo hili wanapoanza kuugua mara nyingi hali hii huwachanganya sana hata kuja kuifahamu. Lakini huwa ni rahisi mno pale dalili zake zinapoanza kujitokeza, nazo huwa kama hizi zifuatazo:

  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara
  • Kukojoa sana hasa mida ya usiku
  • Shida pale unapoanza kukojoa
  • Mkondo wa mkojo kuwa dhaifu, na hivyo kuzuia mkojo usitoke
  • Mkoko kutoka kidogo kidogo sana pale unapomalizia kukojoa
  • Mkojo kushindwa kutoka wote kwenye kibofu

Lakini pia bado zipo dalili ambazo huwa sio za kawaida kabisa, na humfanya mgonjwa kusumbuka sana, nazo ni hizi zifuatazo:

  • Maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)
  • Kushindwa kukojoa
  • Damu kwenye mkojo

Dalili za uvimbe wa tezi dume huelekea kuwa mbaya polepole. Lakini wakati mwingine dalili hubaki vilevile au hata kupona kwa muda Fulani.

Ukubwa wa uvimbe wa tezi dume mara nyingi huwa haubainishi jinsi gani dalili zilivyo mbaya. Baadhi ya watu wenye uvimbe mdogo wa tezi dume wanaweza kuwa na dalili mbaya sana. Wengine ambao wana uvimbe mkubwa sana wanaweza kuwa na matatizo kidogo tu. Na baadhi ya watu wenye uvimbe mkubwa wa tezi dume huwa hawana dalili zozote hata kidogo.

Je, Visababishi Vyake Ni Nini?

Baadhi ya matatizo ya kiafya yanaweza kupelekea dalili ambazo ni kama zile zilizosababishwa na kupanuka kwa tezi dume. Sababu hizo ni Pamoja na:

  • Maambukizi katika njia ya mkojo yaani UTI
  • Kusinyaa kwa mrija wa mkojo unaobeba mkojo mwilini na kuutoa nje
  • Makovu kwenye shingo ya kibofu cha mkojo kutokana na upasuaji
  • Mawe kwenye figo au kibofu cha mkojo
  • Matatizo kwenye neva zinazodhitibi kibofu cha mkojo
  • Saratani ya tezi dume au kibofu cha mkojo
  • Tezi kuvimba

Baadhi ya madawa pia yanaweza kusababisha dalili zinazofanana na kuziba kwa njia ya mkojo. Nayo ni kama haya:

  • Madawa yanayotuliza maumivu, nayo yanaitwa opioids
  • Madawa kwa ajili ya baridi au aleji
  • Dawa za zamani kwa ajili ya matatizo ya moyo, nazo zinaitwa “tricyclic antidepressants.”

Je, Unapaswa Ufanyeje?

Nikushauri ufike hospitali bila kuchelewa unapoona dalili hizo, hata kama hazikusumbui. Ni vyema kugundua mapema kama kuna visababishi ambavyo vinaweza kutibiwa. Bila matibabu, hatari ya kuziba kwa njia ya mkojo inaweza kuibuka. Kama mkojo hautoki, pata matibabu haraka sana.

Je, Mambo Hatarishi Yakoje?

Mambo hatarishi yanayopelekea mwanaume kupatwa na tatizo la kupanuka kwa tezi dume ni kama haya yafuatayo:

  • Umri kuwa mkubwa
  • Ugonjwa wa kisukari
  • Ugonjwa wa moyo
  • Mitindo mibaya ya ulaji au unywaji.

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Maradhara ya ugonjwa huu huwa ni makubwa mno, na ndio maana muhusika anapaswa kupata tiba mapema bila kuchelewa. Madhara yake ni kama haya yafuatayo:

  • Kushindwa kukojoa kabisa
  • Kupatwa na maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)
  • Mawe kwenye kibofu cha mkojo
  • Kibofu cha mkojo kuharibika
  • Figo kuharibika

Nipende kuishia hapa katika makala hii nikaribishe kipindi cha maswali kwa yeyote anayehitaji kuuliza na kutoa maoni.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATsAP ukajiunga na group letu ambalo unaweza kujifunza mambo mengi juu ya afya.

Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kupitia namba zetu hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha Mbauda

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *