Madhara 5 Ya Kutoshika Mimba (Ugumba) Unayopaswa Kuyafahamu

Ugumba au inamaanisha mwanamke kutokuwa na uwezo wa kushika ujauzito licha ya kufanya tendo la ndoa bila kutumia kinga kwa Zaidi ya mwaka mmoja. Ugumba unaweza kusababishwa na mambo mengi mbalimbali. Kutegemeana na mambo yanayosababisha ugumba, bado kuna uwezekano wa kutibu ugumba kwa njia mbalimbali hususani tiba za asili. Matibabu kwa ajili ya ugumba yana mafanikio makubwa sana kupitia tiba za asili kiasi kwamba, mwenza(mgumba) yupo tayari kubeba mimba ndani ya miaka miwili bila kusumbuka.

Ni vyema kukumbuka kwamba ugumba hauwaathiri wanawake tu. Kwa namna nyingine iko hivi, mwanamke anaweza asibebe mimba kwasababu ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kumbebesha mimba.

Je, Ugumba Unatokeaje?

Kama nilivyosema hapo awali kwamba ugumba husababishwa na mambo mengi. Kitu cha kawaida Zaidi miongoni mwa mambo hayo ni tatizo la upevushaji. Hii ni uachiliaji wa yai kwenye vifuko vya mayai. Huku kutokupevusha mayai au upevushaji wa mayai wa kubadirikabadirika mara nyingi husababishwa na mvurugiko wa homoni(hormonal imbalance). Visababishi vingine vya ugumba ni:

  • Kuziba kwa mirija ya uzazi
  • Kuwepo kwa makovu kwenye vifuko vya mayai pamoja na mirija ya uzazi
  • Kuvurugika kwa homoni(hormonal imbalance)
  • Matatizo ya mlango wa kizazi
  • Kuwepo kwa uvimbe maji au uvimbe wa fibroid kwenye kizazi
  • Kizazi kuwa tofauti

Je, Nani Ambaye Anayeweza Kupata Ugumba Kwa Urahisi?

Unaweza kuwa katika hatari ya kuendelea kuwa mgumba ikiwa kama:

  • Unateseka na uvimbe maji(ovarian cysts)
  • Una umri Zaidi ya miaka 30
  • Unavuta sigara kila mara
  • Ni mnene sana au mwembamba sana
  • Unakunywa pombe nyingi
  • Una magonjwa ya zinaa.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje? Je, Mgumba Anapimwaje?

Mara nyingi huwa hakuna dalili au ishara zinazoonekana kwa nje kuhusu ugumba. Wanawake wengi wanapimwa na kukutwa na ugumba baada tu wanaposhindwa kubeba ujauzito kwa Zaidi ya mwaka mmoja. Kulingana na ugumba uliosababishwa na kutokupevuka kwa mayai, mwanamke anaweza kuona mzunguko wa hedhi wenye kubadirikabadirika au kukosa hedhi kabisa. Mzunguko wa hedhi unaobadirikabadirika humaanisha mzunguko kuwa mfupi Zaidi ya siku 21 au mrefu Zaidi ya siku 35.

Je, Vipimo Vinafanyikaje?

Vipimo kwenye ugumba hulenga hasa chanzo cha tatizo. Hii huanza na kipimo cha mwili na inaweza kuambatanisha idadi ya vipimo kadha wakadha kama vile kipimo cha upevushaji wa mayai(ovulation testing), kipimo cha kuziba kwa mirija ya uzazi(Hysterosalpingography), kipimo cha vifuko vya mayai, nk. Kwa hiyo, hata kama kuna vipimo hivi, bado daktari anaweza kushindwa kuhakikisha chanzo cha ugumba.

Je, Nini Madhara Ya Ugumba?

Madhara yaliyosababishwa na ugumba mara nyingi yana athari za kijamii na kihisia. Haya yanaweza kuwa ni pamoja na:

  • Matatizo ya kimahusiano
  • Msongo wa mawazo
  • Matatizo ya kiakili
  • Mashaka
  • Unyanyasi wa kijamii

Mpendwa msomaji Makala yetu ndio inafikia mwisho hapa, naomba nikaribishe tu kipindi cha maswali, karibu sana!

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuunganishwa na darasa letu uweze kujifunza Zaidi mambo ya afya.

Je, Unahitaji huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *