Haya Ndio Madhara Ya Kutoa Mimba

Wanawake wengi wanaonyesha kuwa wasiri sana pale wanapokuwa wakifanya tabia ya utoaji mimba. Lakini hali zao baadaye hudhihirisha tu kile walichokuwa wakikifanya hapo awali. Wengi wao hufika hospitalini huku hali zao zikiwa tete kabisa pamoja na kwamba wanaweza kujitahidi kuficha historia ya mambo yao waliyokuwa wakiyafanya hapo awali.

Lakini wapo wengi ambao hufanya tabia ya kutoa mimba bila kushirikisha wataalam, nao hutumia vidonge vya kumeza au vya kuingiza ukeni. Wanaweza kufanikisha kutoa mimba mara ya kwanza na wasione madhara, na hivyo huendelea na tabia za kushiriki tendo la ndoa na baadaye mimba huingia bila kutarajia tena, na hivyo kuamua kutoa tmimba kwa njia ya kawaida tu kwa kutumia vidonge, nao hujipa moyo sana pale wanaposhindwa kuona madhara yoyote baada ya kufanikisha kutoa mimba ya pili. Hivyo huendelea na tabia ile ile wakitumaini kwamba hakuna madhara kabisa, huku wakijifananisha na wanawake wengine ambao hawajabeba mimba kabisa au hawajawahi kuzaa.

Leo nataka nikupe siri uijue vizuri tu kwamba nini kinachofuata baada ya kutoa mimba Zaidi ya mara mbili? Mwanamke anapokuwa na tabia ya kutoa mimba Zaidi ya mara mbili, madhara yanayompata huwa ni mabaya mno nayo ni kama haya yafuatayo:

  • kupata maambukizi katika viungo vya uzazi
  • kuharibika kwa mimba kila wakati kutokana na shingo ya kizazi kulegea
  • kupata msongo wa mawazo
  • uke kuuma sana wakati wa kushiriki tendo la ndoa(maambukizi)
  • kukosa furaha na kushindwa kufurahia tendo la ndoa
  • kupata ugumba
  • mimba kutunga nje ya kizazi
  • kuzaa watoto wasiokuwa na akili nzuri
  • kupata kansa ya shingo ya kizazi
  • kupata shida wakati wa kuzaa kwasababu shingo ya kizazi inakuwa imepata majeraha
  • kushindwa kupata mimba tena kutokana na maambukizi kwenye viungo vya uzazi

NUKUU: Mfuko wa uzazi una utando maalumu ambao hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija ya uzazi(fallopian tubes) kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mfuko wa uzazi, lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo ya uzazi na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia nje ya kizazi na matibabu ya tatizo hilo ni kukata mirija husika, hali ambayo husababisha kuongeza hatari ya ugumba.

Mwisho kabisa ni hili; wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya shingo ya kizazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba nah ii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutolea mimba, na mabadiriko ya ghafla ya homoni.

Je, Nini Kifanyike?

Mimi sintapendekeza kutoa mimba kwakuwa kutoa mimba ni kuua, na kuua ni dhambi kutokana na amri ya Mungu inavyosema. Kumbuka unapotoa mimba unaua, na pia damu hiyo itakulilia tu katika maisha yako. Ninachopenda kushauri ni kuzaa tu upate mtoto au watoto maana ndio mpango Mungu aliotupatia.

Mke mzuri na mwema yeye huolewa na kuwa na mji mzuri na kisha huzaa watoto na kutunza familia yake. Mwanamke au mke mbaya yeye atakuwa sio mwema, atakuwa muovu, muongo, mwenye jeuri, na hatimaye muuaji tena katili asiye kuwa na hofu.

Sasa wapi pakuponea? Njoo kwa Yesu, bila shaka atakuvua mzigo huo wa ubaya wote ulionao maana anasema hivi:

“Utatangatanga mpaka lini, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mumewe”. Yeremia 31:22

Njoo kwa Mungu, kwa maana hakuna njia nyingine ambayo utatumia ili kukwepa kuolewa na kuwa na mji au kuwa na mume na kufanya jukumu la kumlinda mumeo. Unapoenda kinyume na jinsi Mungu alivyoweka taratibu zake, maana yake una kiuka taratibu na maagizo yake, na matokeo yake ni ghadhabu za magonjwa mbalimbali yatayokupata katika maisha yako na mwisho wake huwa ni mateso na kifo.

Mungu akubariki sana mpendwa msomaji. Karibu sana kwa maswali yako na mchongo wako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Kwa huduma na ushauri, basi unaweza kutupigia kwa namba hizi: 0768559670/0712181626.

Mbauda-Arusha,

Karibu sana!

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *