Uvimbe maji ni mfuko wa majimaji yasio ya kawaida, kama vile malengelenge, ambayo yanaweza kujengeka katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwa ni pamoja kwenye ngozi, sehemu za siri na viungo vya ndani vya uzazi. Uvimbe unaweza kutofautiana kuanzia ukubwa mdogo hadi kuwa mfuko mkubwa wenye lita nyingi za majimaji.
Vivimbe maji ni vifuko iliyojaa majimaji ambavyo vinaweza kukua kwenye tishu katika sehemu yoyote ya mwili. Vivimbe hivi ni vya kawaida, na kuna aina nyingi mbalimbali. Maambukizi, uvimbe, vimelea, na majeraha yanaweza kusababisha vivimbe maji. Mara nyingi huwa havina madhara, lakini wakati mwingine vinaweza kuwa saratani.
Baadhi ya vivimbe maji ni kama hivi hapa chini:
- Vivimbe maji vinavyokuwa nyuma ya magoti(Baker’cysts)
- Uvimbe maji unaokuwa kwenye mashavu ya uke(Bartholin cyst)
- Uvimbe maji kwenye matiti(Breast cyst)
- Vivimbe maji kwenye figo(kidney cysts)
- Vivimbe maji kwenye vifuko au ovary ya mayai(ovarian cysts)
- Vivimbe maji vinavyokuwa kwenye vifundoni mwa vidole au miguu(ganglion cyst)
Uvimbe maji usipotibiwa, unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na: Maambukizi, kivimbe hujaa bakteria na usaha, na kuwa kama jipu. Kama jipu likipasukia ndani ya mwili, kuna hatari ya damu kuchafuka, hali ambayo inaweza kusababisha shida kubwa sana kwa muhusika kama mgonjwa.
Vyanzo vya kawaida vya uvimbe maji kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) huwa ni pamoja matatizo ya homoni. Pia vinaweza kusababishwa na madawa uliyokuwa ukitumia kwa ajili ya kupevusha au kukomaza mayai.
Kwa namna hiyo basi, unaweza kuwa na:
- Maumivu kwenye nyonga, nayo yanaweza kuanza taratibu baadaye yakawa makali sana
- Maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa
- Kushindwa kukojoa na kumaliza mkojo wote kwenye kibofu
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, vipindi vya hedhi kubadirikabadirika, au kutokwa na damu nyepesi kuliko kawaida,
- Tumbo kuvimba au kuwa kubwa
Uvimbe maji huwa kama kifuko(kipochi) ndani ya tishu, ambacho kwa kawaida huwa hakipaswi kuwa mahali hapo. Kinaweza kujaa majmaji, damu damu, tishu, nywele, mfupa, mwili tofauti, nk. Nimesema hapo juu kuwa kama kifuko hiki kikijaa usaha, kinakuwa kifurushi fulani ambacho tunaita jipu. Kwahiyo uvimbe maji unaweza kujitokeza mahali popote, ndani au nje ya mwili wako.
NUKUU: Fungua pia link hii: Fahamu Aina Ya Vivimbe Maji Kwenye Vifuko Vya Mayai (Ovarian Cysts), Dalili Zake Na Madhara Yake.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili za uvimbe maji kwenye vifuko vya huwa kama hivi ifuatavyo:
- Tumbo kuwa kubwa
- Kuhisi maumivu wakati unapojisaidia haja kubwa
- Maumivu kwenye nyonga muda mfupi kabla au baada ya hedhi
- Maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndoa
- Maumivu kwenye nyonga
Dalili za kawaida za uvimbe maji kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) ni pamoja na:
- Maumivu ya kiuno
- Maumivu maeneo ya tumbo la chini
- Maumivu ya kuchoma hasa unapokuwa ukifanya shughuli zako
- Tumbo kuunguruma, au kuhisi tumbo kujaa
- Kuhisi kichefuchefu na kutapika
Vivimbe maji kwenye vifuko vya mayai (ovarian cysts) vinaweza kuathiri uwezo wako wa kuzaa, navyo ni pamoja na: Endometriomas. Endometriomas ni uvimbe unaosababishwa na ugonjwa wa endometriosis, hali ambayo tishu za mfuko wa uzazi huota nje ya mfuko wa uzazi na hivyo kukua. Vivimbe maji hivi kwenye vifuko vya mayai vinaweza kuambatana na tatizo la kutokupata ujauzito kabisa(ugumba).
Hivyo basi, uvimbe maji kwenye vifuko vya mayai hausababishi mimba kutoka. Lakini kama ukipasuka, unaweza kusababisha damu kuvuja ndani kwa ndani na kusababisha mimba kuharibika na kisha kutoka.
Kusema kweli uvimbe maji kwenye vifuko vya mayai husababisha maumivu ya kiuno kwa asilimia 45% kwa wanawake. Uvimbe maji kwenye kifuko cha mayai unapokuwa mkubwa unaweza kusababisha maumivu ya kiuno. Hii ni kwasababu uvimbe maji mkubwa husababisha mgandamizo kwenye tishu na viungo vingine vya uzazi, na kupelekea masumbufu kwenye kiuno chako.
Uzoefu wa kawaida, uvimbe wa ovari kwa kawaida huwa hauna madhara wala dalili. Uvimbe wa ovari lazima usababishe tumbo kuunguruma, na tumbo kuuma lakini huwa hauambatani na kuwa na uzito mkubwa.
Uvimbe maji unaweza kukufanya ukahisi tumbo kujaa hata bila kuvimba. Kunaweza kuwa na maumivu makali ya kiuno, au maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa. Wakati mwingine uvimbe unaweza kupasuka, na kusababisha maumivu makali ya ghafla. Uchafu wenye rangi ya kahawia ukeni unaweza kutoka.
Tahadhari:
Epuka vyakula vilivyojaa mafuta na kolesteroli nyingi, vyakula vyenye wingi wa mafuta hali ambayo hupelekea kuwa na magonjwa ya moyo. Vyakula vilivyojaa mafuta ni pamoja na nyama, bidhaa za maziwa yenye mafuta, nk.
Je, Ni Vyakula Gani Unapaswa Kutumia Wakati Unapokuwa Na Uvimbe Maji?
Chakula cha mwanamke mwenye uvimbe maji kwenye vifuko vya mayai ni pamoja na hivi vifuatavyo:
- Mboga za majani
- Viazi
- Kabeji
- Bilinganya
- Njugu mawe
- Tikiti maji
- Machungwa
- Mapera
- Mapapai
- Parachichi nyingi,
- Ndizi,
- Zabibu
Naomba niishie hapa wapendwa wanagroup, naomba nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yenu. Pia unaweza kutuma namba yako ya whatsAp ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya uvimbe maji kwenye kizazi. Je, unahitaji hudumua? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712 181 626,
Arusha-Mbauda.
Karibuni sana!