Vyakula vyote vyenye viini lishe vinavyodhibiti ongezeko la oksijeni, kama vile matunda na mboga za majani, uwezo wa kumbukumbu kwenye ubongo wako.
Sehemu Ya Utunzwaji Wa Kumbukumbu
Viini lishe katika rojorojo hii vinaonyesha kuboresha kumbukumbu na uwezo wa akili, kutokana na majaribio yaliyofanywa kwa wanyama na wanadamu. Maembe huboresha uwezo wa kukumbuka na kuchochea kazi za ubongo, kwakuwa yana viinilishe vinavyodhibiti ongezeko la oksijeni.
Tufaa(apple) na zabibu mbichi au kavu huboresha uwezo wa kumbukumbu na kuboresha utendaji kazi wa ubongo pia, na hupunguza msongo wa mawazo. Maziwa ya nazi, huupatia mwili mafuta maalumu (medium chain triglycerides), ambayo hulinda neva pia, na yanafaa kutumiwa kama mtu ana shida ya kusahau, kama inavyokuwa katika ugonjwa wa Alhzheimer.
Kwa kuzingatia maelezo ya hapo juu. Rojorojo iboreshayo kumbukumbu imethibitika kuwa na viini lishe vya kutosha na ladha nzuri. Yafaa wakati wa staftahi, au kama asusa ya katikati ya alasiri kwa vijana au wazee wanaotaka kuboresha uwezo wa kumbukumbu na akili.
VIUNGO
Kwa Milo Mitatu Ya Milimita 250
- Embe ½ (kama gram 168)
- Tufaa (apple) 1 (kama gram 161), likiwa na maganda yake
- Vijiko viwili vya zabibu kavu(zisizo na mbegu ni bora zaidi) kila kijiko kimoja ni kama gram 15 hivi,
- Kikombe 1 cha maziwa ya nazi (kama milimita 226)
- Majani ya mnanaa(kila kimoja ni kama gram 0.05)
MAANDALIZI
- Menya na katakata embe na tufaa
- Changanya viambata vyote.
Basi, blendi ili upate juisi. Baada yapo, unaweza kunywa juisi yako vizuri kabisa.
Hakikisha unatumia glasi 1 mara mbili au mara moja kwa siku.
Neno La Faraja: Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa….Mithali 10:14
Ndugu msomaji, makala yetu inaishia hapa, tunakaribisha kipindi cha maswali na maoni yako.
Je, unahitaji huduma? Basi, wasiliana nasi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Arusha.