Mambo 6 Yanayomfanya Mwanaume Kupata UTI.

Njia yako ya mkojo inajumuisha sehemu za mwili wako zinazotengeneza mkojo na kuutoa nje ya mwili wako.

Kwa wanaume, sehemu hizi ni pamoja na figo zako, kibofu cha mkojo, mirija ya mkojo, na njia ya mkojo. Mirija ya mkojo ni mirija pacha inayosafirisha mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu chako. Mrija wako wa mkojo ni mrija mmoja unaosafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo kupitia kwenye kibofu chako hadi ncha ya uume wako.

Ikiwa bakteria wabaya hujilimbikiza mahali popote kwenye njia yako ya mkojo, hii inaweza kusababisha maambukizi.

Ingawa maambukizo ya kwenye mfumo wa mkojo (UTIs) ni ya kawaida zaidi kwa wanawake, lakini na wanaume pia wanaweza kupata. Wanaume wenye umri mdogo hupata UTI mara chache sana. Huwapata zaidi wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50. Takriban 12% ya wanaume hupata UTI wakati fulani.

Aina Za UTI Kwa Wanaume

  1. Maambukizi ya njia ya chini

Maambukizi ya njia ya chini ni yale yanayotokea kwenye kibofu, tezi dume, au njia ya mkojo. Aina ya kawaida ya UTI ni maambukizi ya kibofu. Hali hiyo pia inaitwa cystitis. Aina nyingine ya maambukizi ya njia ya chini ni kuvimba kwa njia ya mkojo (urethritis).

  1. Maambukizi Ya Njia Ya Juu

Maambukizi ya njia ya juu hutokea kwenye mirija ya mkojo (ureters) au figo. Aina moja maalum inaitwa pyelonephritis. Hayo ni maambukizo ya figo zako, kwa kawaida ambayo yanakuwa yameenea kwenye njia yako ya mkojo.

Dalili Za UTI Kwa Wanaume

Kulingana na eneo la UTI yako, unaweza kuwa na moja au zaidi ya dalili hizi:

  • Kukojoa mara kwa mara
  • Muda wote kuhisi kama unataka kukojoa
  • Kuhisi maumivu wakati unapokojoa au unapomaliza kukojoa
  • Kuhisi maumivu maeneo ya tumbo la chini
  • Kulowanisha kitanda
  • Mkojo mchafu au wenye harufu
  • Damu kwenye mkojo
  • Kuhisi homa
  • Kuhisi kichefuchefu
  • Kuhisi maumivu upande wa kulia na kushito au mgongoni

Wanaume wengine huwa hawapati dalili zozote.

Je, Nini Kinachosababisha UTI Kwa Waanaume?

Kwa kawaida wanaume hupatwa na maambukizi kwenye njia ya mkoto kutokana na mambo haya yafuatayo:

  • Maambukizi Ya Magonjwa Ya Zinaa: Pangusa (Chlamydia na kisonono ni magonjwa mawili ya zinaa ambayo yanaweza kusababisha UTI. Magonjwa ya zinaa pia ndio chanzo cha kawaida cha UTI kwa wanaume wenye umri mdogo.
  • Matatizo Ya Tezi Dume: Kuvimba kwa tezi dume ni kawaida kwa wanaume hasa wazee, na hali hii inaweza kuzuia mtiririko wa mkojo. Hali hii inaweza kuongeza uwezekano wa kuwa na bakteria na kusababisha UTI.
  • Ugonjwa Wa Kisukari: Hali hii na masuala mengine ya kiafya yanayoathiri mfumo wako wa kinga pia yanaweza kukufanya uweze kupata UTI.
  • Mawe Kwenye Figo: Unapokuwa na mawe kwenye figo, kuziba kunaweza kusababisha mkojo kujaa kwenye kibofu chako. Hiyo huongeza uwezekano wa kupata UTI.
  • Utumiaji Wa Mipira (Cathethers): Mipira ambayo ni mirija nyembamba iliyoingizwa kwenye kibofu, huruhusu watu ambao hawawezi kukojoa waweze kutoa mkojo kutoka kwenye  kibofu chao. Unaweza kuwa na mpira mmoja hospitalini kwa sababu umepooza, au kwa sababu una hali ya neva ambayo huathiri uwezo wako wa kukojoa. Mirija hii pia huongeza hatari ya kupata UTI.
  • Upungufu Wa Maji Mwilini: Ikiwa mwili wako haupati maji ya kutosha, mkojo wako hujilimbikiza zaidi na unaweza kutoka taratibu sana. Hali hiyo inaweza kuunda matatizo ya UTI.

Je, Vipimo Vya UTI Vinafanyikaje Kwa Wanaume?

Daktari wako atakuuliza kuhusu dalili zako. Pia watauliza kuhusu historia yako ya ngono kwa sababu ngono inaweza kuongeza hatari yako ya UTI.

Vipimo vya mkojo vinaweza kuthibitisha kama una UTI. Ikiwa daktari wako anafikiri kuwa tatizo linaweza kuwa linahusiana na tezi dume, unaweza kupata uchunguzi wa tezi dume. Mara chache, unaweza pia kuhitaji kupata kipimo cha X-ray au ultrasound ili daktari wako apate kuangalia vizuri njia yako ya mkojo.

Je, Tiba Yake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa maambukizi ya UTI kwa wanaume na wanawake pia. Je, unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya ya kila siku.

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *