Zijue Sababu Zinazofanya Uke Kutoa Sauti Wakati Unaposhiriki Tendo La Ndoa

Uke kutoa sauti ni pale hewa inapopita na kuingia ndani ya uke. Hewa inapopita, baadaye hutoka ukeni na inaweza kusababisha sauti sawa na kujaa gesi tumboni na kutoka kwenye njia ya haja kubwa(kujamba). Kwa kawaida ni tukio la kawaida, na huwa ni hali inayojitokeza kwa nadra sana.

Hata hivyo inaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa ambao utahitaji kutibiwa.  Ngoja tuangalie vyanzo vyake na ni wakati gani unapaswa kufika hospitali kuweza kupata matibabu.

Je, Visababishi Vyake Ni Nini?

Kuna mambo mengi mbalimbali yanayoweza kusababisha uke kutoa sauti. Ni vyema kufahamu vyanzo mbalimbali, kwani mengine yanahitaji kushughulikiwa na mtaalamu wa matibabu. Baadhi ya vyanzo hivi ni kama hivi vifuatavyo;

  1. Kushiriki Tendo La Ndoa

Tendo la ndoa ni chanzo cha uke kutoa sauti. Mwendo wa uume unapoingia ndani na kutoka nje wakati mwingine unaweza kusababisha hewa kuingia na kisha kuzuiwa. Wakati misuli ya uume inapotuna kutokana na kumwaga shahawa au pale uume unapotolewa nje, basi hewa nayo hutolewa nje.Hii inaweza kusababisha sauti ya mlio kama unajamba.

Kuna baadhi ya wanaume hawajui kushiriki tendo la ndoa, hivyo wanatabia ya kufanya kama wanavyofanya wanyama bila kutumia ufundi na utaalamu mzuri kwenye uke wa mwanamke na hivyo kusababisha gesi ukeni au uke kutoa sauti. Lakini pia ikiwa tatizo lipo kwa mwanamke linaweza kusababisha hewa endelevu ukeni.

  1. Uwazi Wa Uke Usio Wa Kawaida

Uwazi wa uke usio wa kawaida huwa ni tundu au shimo lisilo la kawaida kati ya uke pamoja na viungo vingine vya ndani kwenye nyonga. Ni kisababishi cha gesi au sauti ukeni ambayo haitokani na tendo la ndoa. Zipo aina mbalimbali za uwazi au tundu la uke ambazo sio za kawaida. Hali hii inapaswa kufanyiwa uchunguzi na mtaalamu wa mambo ya uzazi.

Je, Dalili Za Uwazi Wa Uke Kuwa Mkubwa Zinakuwaje?

Gesi ukeni ni moja ya dalili ya uke kuwa na uwazi mkubwa. Dalili zingine hutegemeana na saizi na aina ya uwazi wa uke ulionao, lalini hapa kuna baadhi ya dalili unazopaswa kuzitambua:

  • Kinyesi kinachovuja kwenye mkojo
  • Uchafu au mkojo unaotoka ukeni wenye harufu mbaya
  • Maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)
  • Kuharisha
  • Maumivu ukeni au kwenye njia ya haja kubwa
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kichefuchefu
  • Maumivu maeneo ya tumbo la chini

Je, Unawezaje Kuzuia Uke Usitoe Sauti?

Hakuna mambo mengi unayoweza kufanya ili kuzuia uke usitoe sauti unaposhiriki tendo la ndoa. Mara nyingi huwa ni dalili magonjwa mengine au tukio la asili tu wakati unaposhiriki tendo la ndoa. Hata hivyo, yapo matibabu na njia za upasuaji ambazo zinaweza kurekebisha chanzo. Hata gesi inapotoka unaposhiriki tendo la ndoa, kunaweza kuwapo pia matibabu ya kawaida tu pasipokufanyiwa upasuaji na hali hiyo inaweza ikatoweka kabisa.

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili ambazo zinaweza kuondoa chanzo cha uke kutoa sauti wakati wa kushiriki tendo la ndoa.  Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tuweze kukuunganisha kwenye darasa letu upate masomo ya afya kila siku.

Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *