Kwa kawaida uvimbe wa fibroid huota ndani au nje ya mfuko wa kizazi chako. Vivimbe hivi huanza kama seli moja, ambayo baadaye hukua na kuzaliana kwa wingi. Hatimaye, uvimbe wa fibroid huongezeka ukubwa, mahali popote ukianza kuwa na ukubwa wa peasi na hata kufikia ukubwa wa tikitiki maji. Pia vivimbe vya fibroid hubadirika katika umbo.
Vivimbe vingi vya fibroid huonekana nje ya ukuta wa mfuko wa kizazi chako au ndani ya msuli wa tishu wenyewe, lakini kwa namna nyingine, uvimbe wa fibroid unaweza kuchomoza na kurefuka kwa ndani ya uwazi wa kizazi chako.
Ujauzito wenyewe unawezekana ikiwa kama una uvimbe wa fibroid, lakini baadhi ya magonjwa yanaweza kusababisha kutokushika ujauzito (ugumba).
Uvimbe Wa Fibroid Na Kutokuwa Na Uwezo Wa Kupata Ujauzito(Ugumba).
Kutegemeana na ukubwa wa vivimbe vya fibroid na mahali vilipoota, basi vinaweza kuathiri uwezo wako wa kupata mimba na ujauzito wako kwa njia zifuatazo:
- Kuzuia mbegu za mwanaume zisiweze kukutana na yai
- Kuzuia kiinitete kisiweze kujipachika
- Kusababisha kushindwa kuhimili ujauzito
- Kuathiri nafasi na ukuaji wa mtoto
Ukubwa Na Eneo Vinahusiana Na Uvimbe.
Vivimbe vya fibroid vinavyojionyesha juu ya ukuta wa nje wa mfuko wa kizazi kwa kawaida huwa havisababishi ugumba au uwezo wa kutopata ujauzito. Vivimbe ambavyo vinazuia ujauzito kwa kawaida huwa vinapatikana ndani ya mfuko wa kizazi (uterus) au ndani ya msuli wa ukuta.
Ugumba au uwezo wa kutokupata ujauzito ni tatizo lenye utata mkubwa, na vivimbe vya fibroid mara nyingi huwa ndio visababishi. Kusema kweli, karibia asilimia 5-10% ya wanawake wasiokuwa na uwezo wa kupata mimba(wagumba) wana uvimbe wa fibroid. Lakini pale vivimbe vya fibroid vinapochangia kwenye ugumba, mara nyingi ni kwasababu ya ukubwa wake. Uvimbe wowote wenye ukubwa zaidi ya sentimita 6 unaweza kusababisha tatizo tumboni.
Uvimbe Wa Fibroid Kwenye Mlango Wa Kizazi.
Ingawa vivimbe vya fibroid huonekana sehemu ya juu ya mfuko wako wa kizazi, wakati mwingine vinaota mizizi kwenye eneo la chini, juu au kuzunguka shingo au mlango wa kizazi chako, ambao ndio mlango wa mji wako wa mimba. Hii pia ndio mahali ambapo mbegu za mwanaume huingia kwenye kizazi ili kurutubisha yai. Kama uvimbe wa fibroid ulio kwenye mlango wa kizazi ukibadirisha umbo la mlango wa kizazi chako au kuuziba mlango, basi mbegu hazitaweza kuingia na kukamilisha mchakato wa urutubishaji.
Mabadiriko Ya Umbo La Tumbo Lako La Uzazi
Uvimbe wa fibroid mkubwa au ulio na matawi zaidi ya mawili(multiple fibroid) unaweza kubadiri umbo na ukubwa wa mfuko wako wa kizazi, na hivyo kuwa vigumu kabisa kiinitete kujipachika kwenye ukuta wa kizazi. Hata kama mbegu za mwanaume zingeweza kurutubisha yai na kuingia kwenye mfuko wa kizazi, kama halitaanzisha makazi, basi ujauzito unaweza kuharibika.
Mirija Ya Uzazi Kuziba
Kama vile vivimbe vya fibroid vinavyofunika mlango wa kizazi na kuzuia mbegu kushindwa kuingia kwenye kizazi, vilevile vinaweza kuziba mirija yako ya uzazi. Wakati wa utungaji wa mimba, mirija ya uzazi huwa ndio sehemu ya kukutania mbegu za mwanaume pamoja na yai la mwanamke. Ikiwa kama hakutakuwa na upenyo, basi hakuna makutano tena, na hakuna ujauzito.
Uvimbe Wa Fibroid Na Mtoto Tumboni
Vivimbe vya fibroid vinaweza kuathiri ukuaji wa mtoto wako, au hata uwezo wako wa kubeba mtoto katika miezi yote tisa, kulingana na jinsi vivimbe vya fibroid vilivyofanya wakati wa ujauzito. Asilimia 12% ya wanawake wanaokuwa na uvimbe wa fibroid wakati wa ujauzito, na mara nyingi huwa hakuna madhara. Lakini kama uvimbe wa fibroid ukiendelea kukua, mara nyingi hutokea wakati wa miezi ile mitatu ya mwanzo.
Wakati uvimbe wa fibroid ukizidi kukua, unahitaji kulishwa damu nyingi, hali ambayo husababisha damu kuisha kwenye tumbo la uzazi, na mtoto wako anayekua, naye huhitaji virutubishi vingi na hewa nyingi ya oksijeni. Hali hii inaweza kusababisha mimba kuharibika.
Uvimbe mkubwa wa fibroid unaweza pia kuathiri sehemu ya mtoto wako alipo na unaweza kusababisha kujifungua kwa njia ya oparesheni.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya uvimbe tumboni. Pia unaweza kutuma namba zako za WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu uweze kupata masomo ya afya kila siku.
Je, Unahitaji Huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!