Je, Fibroid Ni Nini?
Fibroid ni tishu ndogo ambazo huanza kuota ndani ama nje ya tumba la kifuko cha uzazi la mwanamke. Na ieleweke kuwa, wakati mwingine uvimbe huu hukua na kuwa mkubwa zaidi na kusababisha Maumivu makali ya tumbo la chini na kutokwa na damu muda mrefu kipindi cha hedhi. Tatizo hili linapoanza wakati mwingine unaweza usione dalili zozote. Uvimbe wenyewe huwa sio Saratani.
Kwa kawaida, vivimbe mbalimbali huanza kujitokeza katika maeneo tofauti ndani na nje ya mfuko wa uzazi(uterus): Uvimbe wa Fibroid umegawanyika katika makundi matatu kulingana na maeneo ambapo uvimbe hujitokeza, nayo yako kama ifuatavyo:
- Intramural Fibroid: Ni uvimbe ambao huonekana katikati ya misuli ya ukuta wa kizazi(uterus).
- Subserosal Fibroids: Ni uvimbe ambao hujitokeza nje ya tumbo lako la uzazi(uterus), ambazo hujulikana kwa jina la serosa.
- Submucosal Fibroids : Ni uvimbe ambao hujitokeza katika tabaka la kati la ukuta wa kizazi.
- Pedunculated fibroid: Ni uvimbe usio na saratani kwenye tumbo la uzazi ambao umeunganishwa kwenye ukuta wa tumbo la uzazi na muundo unaofanana na kikonyo unaoitwa peduncle. Peduncle imetengenezwa kwa misuli laini sawa na fibroid na inaweza kuwa na ukubwa kuanzia milimita 5 mm hadi sentimita 10 kwa kipenyo.
- Intracavitary Fibroid: Ni uvimbe usio wa saratani ambao unakua karibu kabisa ndani ya uwazi wa tumbo au mfuko wa uzazi (uterus). Ni aina ya fibroid inayokuwa kwenye mfuko wa uzazi, ambayo ni uvimbe unaoweza kuendelea kukua ndani au nje ya mfuko wa uzazi.
Je, Nani Hupata Uvimbe Wa Fibroid?
Wanawake wote wapo katika hatari ya kupatwa na uvimbe wa Fibroid. Uvimbe wa fibroid huwa ni wa kawaida kwa wanawake. Hali hii hujitokeza asilimia 20-25 kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa. Uwepo wa uvimbe wa fibroid unaweza kupelekea mwanamke kuondolewa kizazi ikiwa kama hautatibiwa ukaondoka. Kwa nyongeza napenda niseme hivi, wagonjwa wengi wa uvimbe wa fibroid hupata dalili lakini hushindwa kuzitambua. Kwa kuwa uvimbe wa fibroid unaweza kumpata mwanamke akiwa katika umri wa miaka 20, lakini wengi wao hushindwa kuhisi dalili zozote mpaka wanapokuwa wamefikisha umri wa miaka 30-40.
Je, Nini Husababisha Fibroid Mayoma?
Vyanzovyakekwakawaidahuwanivingikidogo, navyohuwakamahiviifuatavyohapa;
- Mwanamke kufikisha umri wa miaka 28-33 bila kupata ujauzito
- Ugumba wa muda mrefu
- Matumizi ya pedi zisizokuwa na uthibitisho wa madaktari.
- Kutoa mimba
- Mapungufu ya lishe mwilini, nk.
- Kutoshiri kitendo la ndoa muda mrefu(yaani dada ama mama anapofikia umri wa miaka 25-30 bila kushiriki tendo la ndoa)
Je, DaliliZakeZinakuwaje?
Uvimbe katika kizazi cha mwanamke ukiwa mdogo unaweza usiwe na dalili zozote, na dalili hutegemea sehemu ulipo kwenye mfuko wa uzazi na pia ukubwa wake.
Hata hivyo dalili za ugonjwa huu huwa kama ifuatavyo:
- Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
- Kupata hedhi mara mbili kwa mwezi.
- Maumivu makali wakati wa hedhi.
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu,
- Hedhi zisizokuwa na mpangilio
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
- Kutotunga mimba au kuharibika kwa mimba
- Kukosa choo ama tumbo kujaa gesi na kumfanya muhusika kuwa ana jamba jamba mara kwa mara.
- Maumivu makali wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma uvimbe huo.
- Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ama usio kuwa na harufu lakini mwingi.
Je, Uvimbe Huu Unapozidi Kuwa Mkubwa Husababisha Dalili Gani?
Kwa kawaida uvimbe huu unapokuwa mkubwa husababisha dalili kama hizi zifuatazo;
- Kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe hukandamiza kibofu cha mkojo.
- Mkojo kubaki kwenye kibofu cha mkojo.
- Choo kuwa kigumu ama kukosa choo.
- Kupungukiwa na damu kwasababu fibroid hunyonya damu
Je, Nini Madhara Ya Uvimbe Wa Fibroid?
Uvimbe wa fibroid usipotibiwa huendelea kukua na kuwa mkubwa, na hivyo baadaye husababisha madhara makubwa kwa muhusika nayo huwa kama hivi ifuatavyo;
- Hukandamiza mirija ya kupitishia mayai kutoka katika kiwanda cha mayai yanakozarishwa yaani ovary.
- Uvimbe aina ya Submucosal huzuia yai lililorutubishwa lisijishikishe kwenye kizazi.
- Kushindwa kupata choo au kutoa kinyesi kigumu
- Ugumba
- Mwisho kabisa, huzuia mfuko wa kizazi kusukuma mbegu za mwanaume kwenda kwenye mirija ya mayai.
NUKUU: Unataka kujua zaidi juu ya madhara ya uvimbe wa fibroid, bonyeza hapa: Haya Ndio Madhara 4 Ya Uvimbe Wa Fibroid Kwenye Tumbo La Uzazi.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya vivimbe katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Rafiki, makala yetu inaishia hapa, sasa nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili tueweze kukuunganisha uweze kujifunza zaidi.
Je, Unahitaji Huduma? Basi, wasiliana nasi kwamba hizi: 0768 559 670 au 0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!