Je, kukosa choo ni nini?
Kukosa choo maana yake ni kutokuwa na uwezo wa kwenda haja kubwa kutokana na kinyesi kukusanyikana sehemu moja tumboni na kuwa kigumu na kushindwa kutoka.
Kwa kawaida kinyesi tumboni kinapaswa kutoka kila siku kila baada ya kupata mlo, iwe ni mlo wa asubuhi, mchana au jioni. Hivyo, kila mtu anapaswa apate choo mara 2-3 kila siku. Lakini hali hii inapokosekana, vitu vibaya au vichafu pia huanza kusafiri taratibu na kuingia katika utumbo mpana.
NUKUU: Utoaji kinyesi huwa wenye maumivu sana pindi muhusika anapoenda chooni kujisaidia, na hivyo sumu hunyonywa tena na kurudi tumboni, na kusababisha mzigo mkubwa katika utendaji kazi wa ini na figo. Na ieleweke kuwa, uchafu wote katika mwili wa mwanadamu unapaswa uondolewe ndani ya masaa 18-24 tu!!
Napenda kila mmoja wetu tuelewe kuwa, matatizo mengi ya magonjwa mbalimbali mara nyingi yamekuwa yakisababishwa na hali ya kukosa choo kutokana na milo yetu, kwa mfano:
- Kutokwa na harufu mbaya mdomoni,
- Mwili kutoa harufu, tumbo kujaa gesi, kichwa kugonga, mshipa wa ngiri,
- Mwili kuwa mnene,
- Kukosa usingizi, maumivu ya kiuno, mwili kuchoka,
- Chakula kushindwa kurudiwa kumeng’enywa mara ya pili, na ulimi kuwa na utando mweupe.
- Mishipa ya damu kuwa migumu na kusababisha shinikizo la juu la damu na miguu au mikono kufa ganzi,
Sumu inayonyonywa mara ya pili kutoka kwenye kinyesi kinachoshindwa kutoka tumboni, inaweza pia kusababisha hali ya kipanda uso, tumbo kujaa gesi mara kwa mara na kulifanya kuunguruma na hivyo kujamba hewa yenye harufu mbaya, homa ya uti wa mgongo au vimbe wa tando za uti wa mgongo na ubongo, nk.
Je, Nini Husababisha Kukosa Choo?
Kwa kawaida tatizo hili mara nyingi husababishwa na ulaji wa vyakula aina zifuatazo:
- Chips mayai na juisi,
- Nyama nyekundu(mishikaki, supu, nk)hasa inapoliwa kwa mfululizo)
- Vyakula vilivyosindikwa
- Vyakula vilivyokobolewa kama vile, ugali wa sembe, unga wa ngano (maandazi, chapati, nk)
NUKUU: Hali ya kukosa choo yaweza kuwa ya kawaida kwa mama mjamzito, nitaeleza baadaye pia kuhusu hali hii kwa mjamzito.
Watu wenye umri mkubwa au wazee mara nyingi hupatwa na tatizo la kukosa choo kutokana na mazoea ya kutokunywa maji mengi kwa siku.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kwa kawaida dalili za tatizo hili huwa ni nyingi mno lakini nitaonyesha hizi zifuatavyo:
- Mchafuko wa tumbo
- Mwili kuishiwa nguvu
- Kichwa kugonga
- Kukosa hamu ya kula
- Maumivu ya kiuno.
- Kinyesi kuwa kigumu, kikavu na sio cha mara kwa mara
Je, Nini Madhara Ya Kukosa Choo?
Wengi huona kama jambo la kawaida kwao, lakini ni hatari baadaye, na ndio maana madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu huwa kama hivi ifuatavyo:
- Kukosa hamu ya kula
- Ini na figo kushindwa kufanya kazi vizuri
- Miguu au mikono hasa vidole kufa ganzi
- Kupatwa na magonjwa ya kisukari
- Kukosa hisia ya tendo la ndoa, nk
- Kupungukiwa nguvu za kiume
- Mishipa ya damu kukakamaa au kuwa migumu na kusababisha matatizo ya moyo.
- Kuota nyamanya sehemu za njia ya haja kubwa, yaani bawasiri(haemorrhoid).
NUKUU: Unataka kujua zaidi juu ya bawasiri, bonyeza hapa: Mambo 7 Yanayosababisha Bawasiri
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya kukosa choo. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Unahitaji Huduma? Basi, unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!