Fahamu Mambo 6 Yanayosababisha Miguu Na Mikono Kufa Ganzi.

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.

Mwili wa binadamu hutawaliwa na mifumo ya neva au kwa kitaalamu Nervous System, ambapo katika mifumo hii kuna mfumo mkuu, central nervous system (ubongo na uti wa mgongo) na pia kuna mfumo wa pembezoni ambao ni kazi za mwili mbali na ubongo na uti wa mgongo (peripheral nervous system), mfumo huu wa pembezoni hujumuisha kazi za misuli, mapigo ya moyo, mmeng’enyo wa chakula tumboni, uwezo wa kuhisi baridi au joto, kugusa vitu na kujua ukali wa ncha ya kitu na kadhalika.

Chemotherapy Induced Peripheral Neuropathy - CIPN - Symptoms and Management  | PatientsEngage

NUKUU: Matatizo haya ya kiafya (miguu au mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu huwa ni nyingi mno, nazo kama hizi zifuatazo, naomba kila mmoja azifuatilie:

  • Mtu kuhisi ganzi
  • Maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni au mikononi,
  • Kuhisi kama umevaa soksi au gloves wakati hujavaa,
  • Kuhisi kama kuna kitu cha ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole,
  • Kushindwa kushika au kunyanyua kitu,
  • Kuchoka kwa misuli na kadhalika.

Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo naomba uyafahamu kuanzia sasa:

  1. Kupungua Kwa Virutubisho Mwilini

Katika hili tunamaanisha mwili kutokuwa na vitamini vya kutosha na hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).

  1. Matumizi ya madawa ya vidonge

Mtu kuwa katika matumizi ya baadhi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi huweza kumsababishia mtumiaji matatizo ya neva.

  1. Uzito Mkubwa Wa Mwili

Hali hii hupelekea maumbile ya viungo vya mwili mfano umbile la uti wa mgongo lionekane tofauti na ilivyo kawaida. Kubadilika huku husababisha baadhi ya neva katika uti wa mgongo zikandamizwe zaidi na misuli au uzito wa mwili na hivyo kusababisha neva hizo zishindwe kufanya kazi vizuri, matokeo yake ni wewe kuanza kuhisi maumivi au kufa ganzi kwa miguu.

  1. Ugonjwa wa kisukari

Mtu mwenye tatizo la kisukari huwa hatarini zaidi kuugua au kupata matatizo ya neva, (diabetic polyneuropathy).

  1. Shinikizo la damu

Mtu kuwa na shinikizo la juu la damu (High blood pressure) pia ni kihatarishi kinachoweza kumfanya apate ugonjwa huu wa neva.

115 Black Man Having Stroke Stock Photos - Free & Royalty-Free Stock Photos  from Dreamstime

NUKUU: Baadhi ya vitu hatarishi vinavyoweza kumfanya mtu apate matatizo haya, vinaweza kuepukika kwa mtu kuyabadili maisha yake mfano, kama ulikuwa hufanyi mazoezi ya mwili, basi ujitahidi kuupa mwili wako mazoezi ili kupunguza uzito wa mwili, kuepuka magonjwa ya kisukari na kuepuka kuwa na shinikizo kubwa la damu. Hivyo nakushauri pata vyakula vyenye virutubisho vya kutosha.

 

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James & Ferdinand Herbal Clinic tuna dawa nzuri aina mbalimbali  ambazo hushughulika na kuondoa tatizo hili kwa uhakika kabisa. Unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu ili upate masomo ya afya kila siku.

Je, unahitaji huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *