Fahamu Dalili Na Madhara Ya Uvimbe Wa Utando Wa Ukuta Wa Ndani Wa Mfuko Wa Uzazi (Endometritis)

Endometritis ni kuvimba au kuharibika kwa utando au ukuta wa ndani wa tumbo la uzazi (uterus).Endometritis husababishwa na maambukizi kwenye mfuko wa uzazi. Inaweza kuwa kutokana na pangusa (chlamydia), kisonono (gonorrhea), au mchanganyiko wa bakteria wa kawaida ukeni. Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea baada ya kuharibika kwa mimba au unapojifungua. Pia ni kawaida zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji.

Hatari ya endometritis ni kubwa baada ya kuingiziwa vifaa kwenye kupitia mlango wa kizazi. Vifaa hivi ni kama vile vinavyotumika kwa ajili ya:

  • Kupanua mlango wa kizazi
  • Kuchukua sampuli ya tishu (Endometrial biopsy)
  • Upasuaji mdogo kwenye mfuko wa uzazi (Hysteroscopy)
  • Mpango wa uzazi kwa kufunga mirija ya uzazi
  • Kujifungua kwa upasuaji

Endometritis inaweza kutokea wakati huo huo na maambukizi mengine katika via vya uzazi (PID)

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili zake zinaweza kuwa kama hizi zifuatazo:

  • Kuvimba kwa tumbo
  • Kutokwa na damu au uchafu ukeni
  • Kushindwa kupata choo
  • Kuhisi kuugua
  • Maumivu ya tumbo la chini au maeneo ya nyonga
  • Maeneo ya mapaja kuuma

Je, Vipimo Vinafanyikaje?

Mtoa huduma wako wa afya atafanya vipimo ili kuchunguza viungo vya uzazi. Mfuko wa uzazi na mlango wa kizazi wako unaweza kuwa mororo na mtoa huduma wako huenda asisikie sauti zozote za tumbo kuunguruma. Kunaweza kukawa na kutokwa na uchafu kwenye mlango wa kizazi.

Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika:

  • Kupima mlango wa kizazi kama kuna bakteria wa pangusa au kisonono na vimelea wengine
  • Kuchukua sampuli ya uchafu unaotoka ukeni
  • Kupima kiwango cha chembe nyeupe za damu
  • Kupima aina ya uchafu unaotoka ukeni

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Madhara ya ugonjwa huu yanaweza kuwa kama haya yafuatayo:

  • Kushindwa kupata ujauaizto
  • Uvimbe kwenye maeneo ya viungo vya uzazi
  • Majipu kwenye maeneo ya mfuko wa uzazi
  • Damu kuchafuka

Je, Suluhisho Lkae Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa chanzo na amdhara ya ugonjwa huu. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tukuunganishe kwenye darasa letu la masomo ya afya.

Je, unahitaji huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda

Karibu sana!

2 thoughts on “Fahamu Dalili Na Madhara Ya Uvimbe Wa Utando Wa Ukuta Wa Ndani Wa Mfuko Wa Uzazi (Endometritis)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *