Fahamu Dalili 5 Za Kuvimba Kwa Mishipa Ya Korodani (Varicocele)

Je, Nini Maana Ya Varicocele?

Varicocele ni kutuna kwa mishipa ya ndani ya pumbu inayobeba korodani (scrotum). Mishipa hii husafirisha damu iliyopungukiwa na oksijeni kutoka kwenye korodani. Varicocele hutokea wakati damu inapoingia kwenye mishipa badala ya kuzunguka kwa ufanisi nje ya korodani.

Kwa kawaida varicoceles huanza wakati wa kubalehe na huendelea kukua. Kutuna kwa mishipa hii husababisha usumbufu au maumivu, lakini mara nyingi huwa haionyeshi dalili.

Ugonjwa huu unaweza kusababisha ukuaji duni wa korodani, uzalishaji mdogo wa mbegu au manii au matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha kabisa utasa.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa kwenye korodani (varicocele) kwa kawaida hutokea upande wa kushoto wa korodani na mara nyingi huwa hautoi dalili wala ishara. Lakini dalili zinapoanza kutokea zinaweza kujumuisha mambo haya yafuatayo:

  1. Maumivu: Maumivu makali, au kuwa na masumbufu zaidi wakati unapokuwa umesimama au wakati wa mchana. Kulala chini mara nyingi husaidia kupunguza maumivu
  2. Uvimbe Mkubwa kwenye korodani:Ikiwa mishipa kwenye korodani imetuna sana, basi inaweza kuonekana juu ya korodani. Mishipa ya korodani ikiwa imetuna kidogo sana inaweza kuonekana lakini kwa kugusa.
  3. Ukubwa tofauti wa korodani:Korodani iliyoathiriwa inaweza kuwa ndogo sana kuliko korodani nyingine.
  4. Matatizo Ya Uzazi:Ugonjwa wa varicocele unaweza kusababisha ugumu wa kumpatia mwanamke ujauzito, lakini sio kwamba mishipa ya korodani yote inapovimba  husababisha kutokuwa na uwezo wa kumpa mimba mwanamke (utasa).

Je, Nini Visababishi Vyake?

Tezi dume hupokea damu yenye oksijeni kutosha kutoka kwenye mishipa miwili ya ateri inayokuwa kwenye korodani. Vile vile, pia kuna mishipa miwili ya korodani ambayo husafirisha damu iliyopungukiwa na oksijeni na hivyo kuirudisha kwenye moyo. Ndani ya kila upande wa korodani, kuna mtandao wa mishipa midogo midogo kabisa ambayo husafirisha damu yenye oksijeni kutoka kwenye korodani hadi kwenye mshipa mkuu wa korodani.

Sababu halisi ya varicocele haijulikani. Sababu moja inayochangia inaweza kuwa ni kutokufanya kazi vizuri kwa vali ndani ya mishipa ambayo inakusudiwa kuweka damu katika mwelekeo unaofaa. Pia, mshipa wa korodani wa kushoto hufuata njia tofauti kidogo kuliko mshipa wa kulia – njia ambayo hufanya tatizo la mtiririko wa damu kuwa zaidi upande wa kushoto.

Wakati damu iliyopungukiwa na oksijeni inaporudishwa kwenye mtandao wa mishipa midogo midogo, hupanuka, na kuunda varicocele.

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Kuwa na varicocele kunaweza kufanya iwe vigumu mwili wako kudhibiti joto kwenye korodani. Mkazo wa oxidative na mkusanyiko wa sumu unaweza kusababisha. Sababu hizi zinaweza kuchangia matatizo yafuatayo:

  • Afya Duni Kwenye Korodani:Kwa wavulana wanaoelekea kubalehe, varicocele inaweza kuzuia ukuaji wa korodani, uzalishwaji wa homoni, na mambo mengine yanayohusiana na afya na utendaji kazi wa korodani. Kwa wanaume, varicocele inaweza kusababisha kupungua taratibu kutokana na kupoteza tishu.
  • Matatizo Ya Uzazi/Ugumba:Varicocele sio lazima isababishe utasa. Inakadiriwa asilimia 10% hadi 20% ya wanaume waliogunduliwa na varicocele hupata ugumu wa kumpatia mimba mwanamke. Miongoni mwa wanaume wenye matatizo ya uzazi, takribani asilimia 40% wana ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya korodani (varicocele).

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa vyanzo vya kuvimba kwa mishipa ya korodani. Pia unaweza kutuma namba zako za WHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la afya.

Je, Unahitaji Huduma? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *