Mambo 8 Yatakayokufanya Usikie Raha Zaidi Wakati Unaposhiriki Tendo La Ndoa.

Mara nyingi tendo la ndoa huwa linahitaji maandalizi ya muda mrefu. Lakini kuna baadhi ya wana ndoa huwa wanafikiri maandalizi ya tendo la ndoa huwa chumbani peke yake pindi wanapokuwa kitandani, la hasha, suala la maandalizi ya tendo la ndoa huanza mapema na huanzia kwenye mawasiliano mazuri kati ya mume na mke tangu asubuhi hadi jioni.

Wanandoa pia wanatakiwa kula chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili watakapoanza mchezo huo wasichoke na kujikuta wanashindwa kuendelea na tendo hilo kutokana na mmoja wao kuchoka ama wote kwa pamoja.

Mwanamke anatakiwa kujipamba mapema ili amvutie mumewe (mume huvutiwa sana na kuona mkewe jinsi alivyojipamba ikiwa ni pamoja na kujipulizia pafyumu ambayo mumeo huwa anaipenda). Mwanamke pia unatakiwa kufanya usafi, kuoga vizuri, kusukutua meno kwa dawa ili kuondoa harufu kinywani. Hili ni la kila mwanandoa ili kuondoa kukwepana kubadilishana ndimi wakati wa maandalizi ya awali kabla ya kuanza tendo la ndoa.

NUKUU: Unajua huwa ni kero sana pale mwanamke anapokuwa mchafu hajui usafi wa kinywa chake, uso wake au macho yake? Je, mwanaume anaweza kuwa tayari kumuomba hata ulimi kweli!! Ni aibu.

Je, Hivi Kweli, Kunahitajika Utundu Mkubwa Katika Kumuandaa Mkeo Katika Tendo La Ndoa?

Ndoa ni safari ndefu ambayo inahitaji uvumilivu wa kila namna ili kuhakikisha kila mwanandoa anaifurahia safari hiyo. Leo hii ndoa nyingi zimejaa majuto kutokana na wahusika kukosa uvumilivu katika safari hiyo na kuhisi kuwa pengine njia aliyopita siyo sahihi. Majuto ya safari hiyo yanatokana na mambo mengi, miongoni mwa hayo ni lugha mbaya kwa wanandoa, kumiliki visasi mioyoni mwao, kutosameheana, kushindwa kujishusha pindi mmoja anapokosa na kugundua kuwa yeye ndiye chanzo cha tatizo, kutoaminiana katika mahusiano yao ya ndoa, wivu uliopitiliza, kutoheshimiana nk.

Safari ya ndoa ili iwe salama na yenye baraka tele, inahitahi kutoyaruhusu hata kidogo niliyoyaelezea hapo juu.

NUKUU: Lakini silaha kubwa kuliko yote ni msamaha, suala la kusameheana kwa wanandoa ni dawa tosha ya kuondoa mikosi ya safari ya ndoa iliyojaa kila aina ya vizingiti. Pamoja na hayo jambo lingine ambalo nalo kwa namna moja ama nyingine limechangia kuzifanya ndoa nyingi ziwe katika majuto ni wakati wa tendo la ndoa.

Eneo hili ndiyo kiungo kikubwa kwa wanandoa. Sijawahi kusikia wala kuona eti mtu ameoa ama kuolewa kwa ajili ya kufanya kazi za ndani au kumnunulia nguo mkeo na kuishi kama dada na kaka. Niimani yangu kuwa, kama kungekuwa na hali hiyo, suala la kuoa na kuolewa lisingekuwa na umhimu wowote.

Hakuna raha yoyote ambayo mwanandoa huwa anaifurahia kama tendo la ndoa. Mungu aliamua kuweka kitendo hicho kwa makusudi kabisa na alijua eneo hilo ndio muunganiko wa wanandoa. Raha inayopatikana wakati wa kufanya tendo la ndoa huwa kubwa ajabu na kumfanya mtu hata kama alikuwa na mawazo furani kuyasahau ghafla na kujikuta yupo katika ulimwengu mwingine wenye raha za kila namna na hasa anapofika kileleni hata kama kutakuwa na mtu anataka kumuua kwa bunduki atakubali afe lakini haja yake itimie.

Nikisema hivyo kwa wanandoa wote naamini mnanielewa. Hata hivyo raha hiyo hukolea zaidi pindi wanandoa wanapokuwa na uelewa wa kina katika masuala ya kuandaana vema ambapo ndani ya maandalizi hayo pia wahusika hujikuta wanahama katika ulimwengu huu na kujiona wapo anga jingine kabisa. Mwanamke anapoandaliwa na kushikwa sehemu muhimu kwake naye mawazo yake huhama katika anga hii na kujihisi yupo kwenye anga yenye raha za ajabu isiyo na matatizo hata kidogo na raha hiyo hukolezwa na mwanaume anapotumia utundu wake wote wakati wa maandalizi kwa mwenza wake.

Lakini kuna baadhi ya wanandoa huwa hawaoni raha ya tendo hilo na inapofika wakati mwenzake akamhitaji hukosa raha na kuona kama ameingia kwenye safari ya mateso makali. Na hili mara nyingi huwakumba wanawake ambao waume zao hawajui kuwaandaa vema badala yake hupanda juu haraka haraka kama kuku na kutimiza haja zake kisha anamuacha mwanamke akiwa katika maumivu makali ya kutaka afikishwe kileleni, na mfikishaji wakati huo anakuwa hoi bini taabani.

NUKUU: Ni vizuri utambue kuwa unapoamua kufanya tendo la ndoa ni vyema ukajua mahitaji ya mwenzio iwe mwanaume au mwanamke, jaribu kumfanyia mwenza wako vitu vya tofauti na alivyovizoea ama ambavyo anatarajia kuviona kwako kutokana na mazoea. Ukifanya hivyo utamfanya aendelee kuwa na hamu ya kuwa na wewe kwa muda mrefu.

Naweza kusema mwacheni Mungun aitwe Mungu. Mara nyingi mtoto anapozaliwa kuna baadhi ya vitu huwa anafundishwa lakini baadhi ya vitu huwa havihitaji kufundishwa. Kwa mfano hakuna mtu anayemfundish mtoto kulia, kunyonya, kujisaidia, kucheka, kulala na nk. Japo kuna baadhi ya vitu ambavyo pindi akikua atatakiwa kuachana navyo na kufanya vya kiutu uzima kama suala la kujisaidia. Kwa sababu yeye hujisaidia ndani ya nguo yake ama popote pale, hivyo hufika muda akaelekezwa jinsi ya kujisaidia kuliko salama. Ndivyo hivyo na katika ndoa!!

NUKUU: Hakuna mtu aliyewahi kufundishwa jinsi ya kufanya tendo la ndoa. Wewe hapo ni shahidi, lakini kuna baadhi ya vitu hulazimishwa kufundishwa kulingana na mazingira husika. Ndiyo maana kuna baadhi ya makabila huwafundisha watoto wao kabla ya kuingia katika masuala ya ndoa.

Hivi hapo chini ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kukusaidia katika kuifanya ndoa yako iwe imara na yenye furaha wakati wote:

  1. Uwe mbunifu wa kuangalia ni sehemu ipi ukimshika mke au mumeo anasisimka
  2. Ujue mwili wako na wa mpenzi wako kwa kila mmoja wapi aguswe ili asikie raha
  3. Mweleze mwenzako sehemu ambapo unapenda awe anazichezea ili akupe hisia zaidi.
  4. Jiamini katika kutafuta mitindo ambayo itakuwa faida kwa ndoa yenu
  5. Kila mmoja awe wazi kwa mwenzake na ushirikiano wa mpenzi yenu uwe mzuri.
  6. Ujue sehemu za kumsisimua kwa utundu na ufundi wako mwenyewe
  7. Muulize sehemu anazopata msisimko ili uzifanye naye asike raha wakati wa faragha
  8. Yajue yanayomkosesha raha ya kufurahia tendo la ndoa

Yajue mambo yanayomletea hisia haraka za kufanya mapenzi

NUKUU: Ieleweke kwamba, kila mtu ana maeneo yake muhimu ya kusisimka akiguswa. Watafiti wa masuala ya ndoa wanasema kuwa, maandaalizi mazuri kwa ajili ya tendo la ndoa huchukua muda wa dakika 20 hadi 30 ili kila mmoja awe tayari kwa ajili ya tendo hilo takatifu!!!

Kila mmoja asiwe na haraka, tumia muda mrefu kufurahia tendo hilo kwa pamoja na mpenzi wako. Ieleweke pia kwamba kila mtu anasehemu yake ya kuguswa ambayo humfanya asikie raha wakati wa maandalizi. Ni vizuri kuwa na mawasiliano mazuri ili kila mmoja afurahie maandalizi ya tendo la ndoa.

Wewe mwanaume kumbuka kuwa unaposhindwa kumuandaa mwenzi au mke wako vizuri, basi maeneo yake ya uke yanaweza kuwa makavu na hivyo atashindwa kufurahia tendo la ndoa.

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa visababishi vya ugonjwa huu. Pia tuma namba yako ya WHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya.

Unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *