Je, Unaweza Kupata Ujauzito Huku Ukiwa Na Maambukizi Ya UTI?

Maambukizi ya UTI, kusema kweli hakuna mtu anayeweza kuwaza kwamba tatizo hili haliwezi kumpata. Maambukizi haya yanaweza kusababisha dalili za masumbufu kiasi kwamba zinaweza kuvuruga utaratibu wa siku moja baada ya nyingine. Lakini kuna wakati ambapo maambukizi ya UTI yanapokuwa yanakupatia changamoto hasa pale unapokuwa ukijaribu kupata mimba.

Kutibu maambukizi ya UTI pale unapokuwa ukijaribu kupata mimba kunaweza kuleta maswali mengi mno. Unaweza kujiuliza, je unaweza kweli kupata ujauzito huku ukiwa na magonjwa ya UTI? Je, vipi kama ukianza kutumia vidonge vya antibiotic? Je, madawa hayo yataweza kweli kuathiri ujauzito wako?

Kama wewe ni mwanamke ambaye umekuwa ukitiwa na mashaka sana juu ya maambukizi kwamba yataweza kuathiri ujauzito wako, basi unaweza ukatuliza akili yako tu. Maambukizi ya UTI hayataathiri uwezo wako wa kupata mimba. Lakini kuna baadhi ya mambo unapaswa kuyafahamu juu ya maambukizi ya UTI pamoja na ujauzito ambayo yatakusaidia na mwenzi wako atakuwa mwenye afya na hivyo kuboresha ujauzito wako.

Watu Wengi Wamekuwa Wakijiuliza Je, UTI Ni Nini?

UTI ni kifupi maneno haya(urinary tract infection) yaani maambukizi katika njia ya mkojo. Njia ya mkojo huanza na figo(ambazo hutengeneza mkojo) kuelekea kwenye kibofu cha mkojo(ambacho hushikilia mkojo) mpaka kwenye mrija wa mkojo. Mrija wa mkojo ni kinjia kidogo kutoka kwenye kibofu cha mkojo mpaka nje ya mwili wako. Maambukizi ya UTI hutokea pale bakteria wanapoingia kwenye njia ya mkojo na kuamua kupapenda mahali hapo. Kadiri bakteria hawa wanapoweka makazi, ndivyo wanavyosababisha dalili kadhawakadha kama hizi zifuatazo:

  • Baada ya kumaliza kukojoa, unahisi tena kama unahitaji kukojoa muda uleule,
  • Mkojo wenye damu
  • Kuhisi kama moto pale unapokojoa
  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara kuliko kawaida
  • Kuhisi maumivu kwenye eneo la tumbo la chini au kwenye nyonga

Kama ukihisi dalili hizi, basi hakikisha unafika hospitali haraka bila kuchelewa. Ufikapo huko utafanyiwa vipimo na hivyo kuanza kupatiwa matibabu. Unapaswa pia uzingatie dalili zako na uhakikishe kwamba zinatoweka. Aina moja ya maambukizi ya UTI huhusika na figo. Aina hii ya UTI inaitwa, “pyelonephritis. Maambukizi haya yanaweza kuwa mabaya Zaidi kuliko maambukizi yanayokuwa kwenye kibofu cha mkojo, na husababisha dalili kama hizi:

  • Kuhisi homa
  • Baridi
  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Maumivu kiunoni au kwenye eneo la mgongo wako

Kama ukihisi dalili hizi wahi pia kwenye kituo cha afya uweze kupata matibabu mapema.

Je, Vipi Kuhusu Maambukizi Ya UTI Pamoja Na Ujauzito?

Maambukizi ya UTI mara nyingi huwapata wanawake, lakini wanaume nao wanaweza kuyapata pia. Kwakuwa njia ya mkojo ya mwanamke imetengena kabisa na mfumo wa uzazi, hivyo UTI haiathiri ujauzito wa mwanamke.

Njia ya mkojo ya mwanaume, kwa upande mwingine, iko karibu sana na mfumo wa uzazi. Kwahiyo, mwenzi wako anaweza kuwa na maambukizi ya UTI pale unapojaribu kupata mimba, unaweza kupata shida ya kubeba ujauzito mpaka pale atakapokuwa ameshapata matibabu na kupona kabisa.

Je, Vipi Kama Tayari Umeshapata Ujauzito?

Watu wajawazito hupata UTI Zaidi kwasababu mtoto hubadirisha mambo kadiri anavyozidi kukua. Kama nilivyosema awali, unaweza kujaribu kubeba mimba huku ukiwa na UTI.  Hata hivyo, unapopata mimba, bakteria wanaokuwa kwenye mkojo wanaweza kusababisha madhara kwenye ujauzito kama vile:

  • Mtoto kukua tumboni taratibu mno
  • Kujifungua kabla muda haujakamilika
  • Kujifungua mtoto mwenye uzito kidogo sana

Mtoa huduma wako wa afya ataangalia mkojo wako  zaidi (utakuwa mzuri sana wakati u utakapokojoa kwenye kikombe), lakini hakikisha kuwa umemfahamisha iwapo utapata dalili zozote za UTI wakati unapofika hospitalini.

Je, Suluhisho Lkae  Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo na amdhara ya maambukizi ya UTI. Unaweza pia kutuma namba yako ya WAHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya.

Unahitaji Huduma? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!