Moja ya makosa makubwa ambayo watu wamekuwa wanafanya kwenye maisha yao katika karne hii ni kudharau mambo ambayo ni muhimu sana, lakini huja kujutia baadaye wakati wameshayapoteza. Huwa tunakazana kutafuta fedha na mali na kusahau vitu muhimu sana, ambavyo tumepewa bure kabisa, mpaka pale tunapovipoteza ndipo tunajua gharama yake halisi.
Moja ya vitu tunavyovidharau na kuvisahau ni afya zetu, ukiwa na afya njema, huwezi kujua gharama halisi ya afya yako, na hivyo unaweza kuichukulia kirahisi. Ni mpaka pale unapopoteza afya hiyo njema, kwa kupata magonjwa ndipo unagundua kweli kwamba afya ina gharama kubwa sana.
Msingi wa mafanikio ambao nimekuwa nawashirikisha wanagroup wote ni mafanikio yenye mlinganyo kwenye maeneo yote muhimu ya maisha yetu. Tukianza na sisi binafsi, kazi na biashara, familia, afya zetu na hata jamii inayotuzunguka.
Hebu jiulize hili, umeweka juhudi kubwa sana kwenye kutafuta mafanikio, umejitoa kwa kila hali, na ukayapata mafanikio kweli, lakini muda mdogo baada ya kufika kwenye kilele cha mafanikio, unagundulika kuwa na ugonjwa usiokuwa na tiba, ambao utakuwekea vikwazo vingi kwenye maisha yako. Je utayafurahia mafanikio uliyopata?
Jibu ni hapana, hakuna mafanikio unaweza kuyafurahia kama katika kuyatafuta umepoteza vitu muhimu kama afya au familia.
Leo tutakuwa na darasa la afya ambapo tutaangalia hatari ya magonjwa yasiyoambukizwa na jinsi tunavyoweza kujikinga nayo ili yasiwe kikwazo kwetu kufanikiwa katika maisha yetu, au yasifanye mafanikio yetu yakose maana.
Wacha nikupe siri moja, siku za nyuma kulikuwa na magonjwa ya watu masikini na watu matajiri. Magonjwa yanayoambukizwa, kama malaria, kipindupindu, TB na mengine yalikuwa ni magonjwa ya watu masikini, kwa sababu waliishi kwenye mazingira yanayochochea magonjwa hayo kusambaa baina yao.
Magonjwa yasiyoambukizwa kama presha, kisukari na hata magonjwa ya figo yalionekana kuwa magonjwa ya matajiri kwa sababu yalisababishwa na mtindo wa maisha ambao matajiri ndiyo waliweza kumudu kuwa nao. Mfano kula chakula chenye virutubisho vingi, ambapo kulipelekea mtu kuwa na uzito uliopitiliza, huku akiwa hana kazi za nguvu za kufanya.
Lakini siku hizi, huo utofauti umeondoka, na umekuwa hasara zaidi kwa masikini kuliko matajiri. Sasa hivi magonjwa yasiyoambukizwa yamekuwa mzigo mkubwa kwa masikini kuliko hata matajiri. Hii ni kwa sababu bado masikini wanasumbuliwa na magonjwa ya kuambukizwa, na pia gharama za kutibia magonjwa yasiyoambukizwa ni kubwa sana, kwa mfano mgonjwa tukimwambia kuwa NEOTONIC tunauza shilingi 35,000/=, yeye ataona gharama kubwa mno au bei kubwa, lakini mwenye uwezo kwake sio tatizo wala halalamiki.
Hivyo kila mmoja wetu, anapaswa kuwa makini sana na afya yake. Na kama nilivyosema awali, ni rahisi kuchukulia poa afya yako pale ambapo huumwi, lakini ukishaanza kuumwa, ndiyo utagundua afya yako ina thamani kubwa sana.
Sasa iwe umeshaingia kwenye changamoto ya magonjwa yasiyoambukizwa, au bado, nakukaribisha kwenye darasa la James Herbal Group ujifunze mengi juu ya afya.
Katika Group letu tutazidi kujadili kwa kina changamoto ya magonjwa haya yasiyoambukizwa na jinsi ya kujikinga nayo kama hujayapata, na kama umeshayapata, jinsi ya kuhakikisha hayawi kikwazo kwako kufanikiwa kwako katika ajira yako, biashara zako, nk, na kuyafurahia maisha yako.
Kwenye group hili tutajifunza mambo yafuatayo;
- Umuhimu wa afya imara kwa maisha ya mafanikio.
- Mabadiliko ya hatari kutoka magonjwa yanayoambukizwa kwenda magonjwa yasiyoambukizwa.
- Aina za magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ni hatari kwa maisha ya wengi.
- Mitindo ya maisha inayokaribisha magonjwa yasiyoambukizwa.
- Jinsi ya kutengeneza mfumo wa maisha ambao unakuepusha na magonjwa yasiyoambukizwa.
Kama upo hapa duniani, na upo makini na maisha na mafanikio yako, basi kuna sehemu moja ambayo unapaswa kuwa, nayo ni JAMES HERBAL GROUP. Ninakuambia hili nikimaanisha, kwa sababu najua ukiwa ndani ya JAMES HERBAL GROUP, hutabaki hapo ulipo sasa, nakuhakikishia hilo, lazima utajikuta unasonga mbele zaidi, hata kama unaona umekwama kiasi gani.
Utajifunza jinsi ya kujua vyanzo vya magonjwa, dalili zake, madhara yake na tiba zake. Pia kuna vitabu vizuri ambavyo vitakufundisha tiba za asili unapokuwa nyumbani mwako.
Karibu sana, nakuachia kipindi cha maswali na maoni yako.
Unahitaji huduma, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Rafiki na Dokta wako,
Dr. Samson.
Karibu sana!