Zijue Faida Za Kukojoa Baada Ya Kumaliza Kushiriki Tendo La Ndoa.

Wakati mwanamke anaposhiriki tendo la ndoa, bakteria wanaweza kupita kutoka kwenye sehemu za siri na kuingia kwenye mrija wa mkojo.

Mrija wa mkojo ni mrija unaounganisha kibofu na uwazi ambapo mkojo hupitia na kutoka nje. Bakteria wanaweza kuingia kwenye kibofu cha mkojo kutoka kwenye mrija wa mkojo, na kusababisha UTI.

Kukojoa baada ya kujamiiana husaidia kuondoa bakteria kwenye mrija wa mkojo, hivyo husaidia kuzuia UTI.  Jifunze kuwa na mazoea ya kukojoa kila unapomaliza tu kushiriki tendo la ndoa.

118 Black Couple Waking Up Stock Photos - Free & Royalty-Free Stock Photos from Dreamstime

Wanawake wana uwezekano wa kupata maambukizi ya UTI mara 30 zaidi kuliko wanaume. Hii ni kutokana na sababu mbili: Kwanza, mrija wa mkojo wa mwanamke uko karibu na uke pamoja njia ya haja kubwa.  Hii ina maana kwamba bakteria wanaweza kuingia na kuenea kwa urahisi kutoka maeneo haya hadi kwenye njia ya mkojo. Pili, mrija wa mkojo  kwa wanawake ni mfupi kuliko ilivyo kwa wanaume. Hii ina maana kwamba bakteria wanaoingia kwenye njia ya mkojo wanaweza kufika na kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa urahisi zaidi.

Kwa wanawake, kukojoa baada ya kujamiiana kunaweza kusaidia kuondoa bakteria yoyote kwenye mrija wa mkojo.

Kwa wanaume, kukojoa baada ya kujamiiana sio muhimu sana. Hii ni kwa sababu wanaume wana mrija mrefu wa mkojo. Matokeo yake, bakteria kutoka eneo la uzazi hawawezi kufika kwenye kibofu cha mkojo.

Ingawa hakuna ushahidi thabiti wa kuthibitisha kuwa kukojoa baada ya kujamiiana kunaweza kuzuia UTI, lakini hakuna ubaya kufanya mazoea haya. Inaweza kusaidia kupunguza hatari ya UTI, haswa kwa wanawake na watu ambao wako kwenye hatari ya kupata UTI. Pia kama unataka kujua madhara ya UTI bonyeza link hii: Epuka, Maambukizi Ya UTI Kwani Yanaweza Kukufanya Ukose Ujauzito Kabisa.

Je, Kukojoa Baada Ya Kushiriki Tendo La Ndoa Kunazuia Kushika Mimba?

Kukojoa baada ya kujamiiana hakuwezi kuzuia mimba. Mrija wa mkojo na uke ni sehemu tofauti za anatomia ya mwanamke. Matokeo yake, kukojoa hakutaathiri mbegu za mwanaume (manii) yoyote inayoingia ukeni. Kutumia aina fulani ya uzazi wa mpango ndiyo njia pekee ya kuzuia mimba wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

Je, Inazuia Kupata Magonjwa Ya Zinaa?

Kukojoa baada ya kujamiiana hakuzuii magonjwa ya zinaa (STIs). Watu hupata magonjwa ya zinaa kwa kunyonya bakteria kupitia utando unaokuwa ndani ya miili yao wakati wa kujamiiana, hasa ukeni. Kukojoa baada ya kujamiiana hakutazuia bakteria hawa kuingia mwilini.

Kutumia kondomu au aina nyingine ya vidhibiti vya mimba wakati wa kujamiiana kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya zinaa.

Je, Unapaswa Kukojoa Muda Gani Mara Unapomaliza Kushiriki Tendo La Ndoa?

Hakuna muda unaopendekezwa wa kukojoa baada ya kujamiiana, ingawa baadhi ya watu husema ni ndani ya dakika 30 baada ya kujamiiana. Kwa ujumla, watu wanakojoa haraka baada ya kujamiiana, ndiyo wanaoweza kutoa bakteria kwa haraka kabla ya kuingia kwenye mrija wa mkojo.

Ikiwa watu wanahangaika kukojoa haraka baada ya kujamiiana, lakini pia bado ukinywa maji glasi 1 au 2 itakusaidia. Kiasi kikubwa cha mkojo pia kitakuwa nguvu kubwa ya kuondoa bakteria.

Njia Zingine Za Kuzuia UTI

Vidokezo vifuatavyo vinaweza pia kusaidia kupunguza hatari ya mtu kupata UTI:

  • Kunywa maji glasi 8 kila siku
  • Kojoa mkojo pale unapojihis kukojoa, kuliko kubana mkojo
  • Mara zote jitawaze kwa kupitisha vidole vyako kutoka mbele kurudi nyuma
  • Safisha maeneo ya uzazi kwa maji vuguvugu, epuka kutumia maji moto maeneo hayo,
  • Epuka kutumia sabuni au vitu vyenye marashi maeneo ya uke
  • Vaa nguo za ndani zenye uzi wa pamba
  • Epuka nguo za ndani zenye kubana
  • Epuka kuvaa nguo za ndani zikiwa mbichi ambazo hazijakauka kwani husababisha unyevunyevu na kusababisha bakteria kuanza kuzariana ukeni.

Je, Ni Muda Gani Unapaswa Uonane Na Daktari?

Watu wanapaswa kumuona daktari iwapo watapata dalili zifuatazo za UTI:

  • Kuhisi kama hali ya kuwaka moto pale unapomaliza kukojoa,
  • Kuhisi haja ya kukojoa mara kwa mara, licha ya kupitisha kiasi kidogo tu cha mkojo kila wakati,
  • Mkojo wenye rangi ya ukijivu
  • Mkojo wenye harufu,
  • Damu kwenye mkojo
  • Maumivu makali kwenye kitovu,
  • Kuhisi uchovu, homa au kutetemeka

Ikiwa watu wana UTI, daktari anaweza kupendekeza kutumia dawa za antibiotics ili kuondoa maambukizi. Kwa kawaida watu wataanza kujisikia vizuri ndani ya siku chache tu, lakini ugonjwa utakuja kwa namna nyingine na utaendelea kukusumbua.

Katika baadhi ya matukio, UTI inaweza kuingia kwenye figo. Ugonjwa wa figo unaweza kuwa mbaya na unahitaji matibabu ya haraka. Dalili za maambukizi kwenye figo ni pamoja na:

  • Homa
  • Baridi
  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Maumivu kwenye kiuno

Watu wanapaswa pia kuonana na daktari wao ikiwa wanaona dalili zozote zisizo za kawaida au mbaya wakati au baada ya kujamiiana. Hizi zinaweza kuwa dalili za magonjwa ya zinaa.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa maambukizi ya UTI, nk.

Unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!