Kwa kawaida figo zinapokuwa zikichuja uchafu kwenye damu, hutengeneza mkojo. Wakati mwingine chumvi na madini katika mkojo hukusanyika pamoja ili kuunda mawe madogo ya figo. Nayo huwa na umbo kama punje ya sukari, lakini huonekana kwa nadra sana mpaka pale yanasababisha hali ya kuziba sehemu ya mirija ya mkojo. Mawe haya yanaweza kusababisha maumivu makali yanapopita nakuingia kwenye mirija ya mkojo, na mirija midogo inayoelekea kwenye kibofu cha mkojo. Mawe ya figo kwa kawaida huwapata hasa watu wa umri wa kati na wazee pia, lakini wanawake wengi inaonyesha kuwa wanapatwa na tatizo hili.
Dalili Zake
Wakati mawe ya figo yanapokuwa yakisafiri kwenye mirija ya mkojo, yanaweza kusababisha mambo yafuatayo:
- Maumivu makali mgongoni, tumboni, au kwenye nyonga.
- Kukojoa mara kwa mara au maumivu makali wakati wa kukojoa
- Damu kwenye mkojo
- Kuhisi kichefuchefu na kutapika
- Mawe madogo yanaweza kupita bila kusababisha dalili
Kama ukihisi maumivu makali kwa ghafla sehemu za mgongoni au tumbo la chini, basi ni vyema kuanza matibabu mapema. Maumivu ya tumbo huambatana na hali nyingi mbalimbali, ikiwa pamoja na magonjwa ya kidole tumbo na matatizo ya kutunga mimba nje ya kizazi. Maumivu makali wakati wa kukojoa ni dalili za kawaida za maambukizi katika njia ya mkojo(UTI) au maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Vyanzo Vyake
Kwa kawaida mawe ya figo hutokana na mapungufu ya madini ya chokaa(calcium) na magnesium ambayo mara nyingi husababishwa na mambo yafuatayo:
- Unywaji wa soda badala ya maji ya kunywa. Madini yanayokuwa kwenye mawe hutoka kwenye mifupa yako!
- Vyakula vilivyoondolewa uasili wake, hususani sukari huchochea hali ya kuunda mawe ya figo. Kiwango cha sukari kwenye kongosho huongezeka; na hutengeneza insulin ya nyongeza ambayo, badala yake husababisha figo kutoa madini mengi ya chokaa(calcium) na kuingia kwenye mkojo. Kumbuka madini ya chokaa(calcium) huhitajika mwilini. Ikiwa kama hakuna madini ya chokaa ya kutosha kwenye mlo wako, tezi za parathyroid zitaupa mwili ishara na kuamuru kuchukua madini ya chokaa kutoka kwenye mifupa yako ili kuifanya chokaa(calcium) iliyoko kwenye damu iweze kuwa katika kiwango cha kawaida.
- Mapungufu ya vitamini B6 na madini ya Magnesium
- Kutokunywa maji ya kutosha
- Ulaji wa vyakula vya nyama, unga wa sembe, sukari nyingi, kahawa, vyakula vilivyosindikwa, nk.
Tiba Zake
Ndugu msomaji, ikiwa kama unahitaji kupata huduma, James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo wa kuondoa matatizo haya ya mawe ya figo.
Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626