JE, FIBROIDS NI NINI? JE, WAJUA VYANZO NA DALILI ZAKE?

 

Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao unaweza kuwa ndani ya kizazi (Ukuta Wa Kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi. Naomba wanaofanyiwa vipimo hospitalini, wapatapo majibu wawe makini kumuuliza dakatri kuwa je, uvimbe uko sehemu gani na una ukubwa wa sentimita ngapi? Nasema hivyo kwasababu baadhi ya kina mama unakuta wakati mwingine kapokea kadi lakini hajapata maelezo vizuri kutoka kwa daktari ama daktari anaweza kumweleza vizuri lakini akashindwa kumuelewa kutokana na hali ya wasiwasi anayokuwa nayo mgonjwa moyoni mwake.

Kuna aina kuu tatu za Fibroids, nazo ziko kama ifuatavyo:

1. Sub mucosal fibroids (ndani ya kizazi)
2. Intramural fibroids (ndani ya nyama za kizazi)
3. Sub serosal fibroids(nje ya kizazi)

Wanawake amabo hawajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa, ama wenye unene wa kupindukia, ama waliowahi kuingia katika kipindi cha hedhi mapema, ndio wako katika hatari kubwa ya kupatwa na ugonjwa huu.

Fibroids sio kansa bali ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen  ndio maana wanawake kuanzia umri wa kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako katika hatari ya kupatwa na janga hili.  Na mara nyingi uvimbe huu huwa unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huo ili kulinda makazi ya mtoto.

DALILI ZAKE

Kwa kawaida dalili za uvimbe wa fibroids huwa kama ifuatavyo:
1. Kutokwa damu kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi.
2. Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya au ambao hauna harufu lakini mwingi na mweupe.
3. Maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma uvimbe huo.
4.Tumbo kuuma sana chini ya kitovu.
5. Hedhi zisizokuwa na mpangilio.
6. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
7. Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
8. Maumivu makali wakati wa hedhi.

 

Uvimbe huu unapokua mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo

  • Kukojoa Mara Kwa Mara Kwani uvimbe unakandamiza kibofu cha mkojo.
  • Mkojo kubaki kwenye kibofu cha mkojo
  • Haja Kuwa Ngumu.
  • Kupungukiwa damu kwasababu fibroid hunyonya damu nyingi.

 

Je, uvimbe unaweza kuzuia mwanamke asipate mtoto?

Kwa kawaida tatizo hili linaweza kusababisha mambo yafuatayo:

  • Uvimbe(Fibriods) unapokuwa sana hukandamiza mishipa ya kupitisha mayai kutoka kwenye kiwanda cha mayai yanakozalishwa yaani Ovari.
  • Uvimbe huu pia unazuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi, hasa submucosal fibroids.
  • Pia huzuia mfuko wa kizazi kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.

 

JE, NINI CHA KUFANYA ILI UPATE KUPONA?

Ndugu msomaji, ikiwa kama unahitaji huduma kwa ajili ya kuondoa tatizo la uvimbe,  James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uhakika mkubwa wa kuponya na kuzuia matatizo ya uvimbe katika via vya uzazi. Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626