JE, WAJUA CHANZO NA DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA?

 

Ndugu msomaji, katika makala hii leo napenda tuzungumzie  ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa tishio kubwa na kusababisha vifo vingi ulimwenguni, khususan katika nchi za Kiafrika, vifo ambavyo zaidi huwaandama watoto walio na umri chini ya miaka mitano, licha ya kuwa ni rahisi kutibika.

 

Vyanzo Vyake

 

Malaria ni ugonjwa unaoambukiza wanadamu wakati mbu aina ya Anopheles anapomuuma mtu. Mbu huyo wakati akimuuma mtu huacha vimelea vinavyojulikana kama ‘plasmodium’ ndani ya mwili. Vimelea hivyo wakati vikiwa ndani ya mwili, husafiri mpaka katika ini kupitia damu. Itafahamika kuwa mtu aliyeambukizwa vimelea vya malaria haugui mpaka vimelea vyote vya ugonjwa huo vitoke nje ya ini, ambapo huchukua muda wa wiki mbili tangu mtu aumwe na mbu.
Dalili Zake

Dalili za awali za malaria ambazo mara nyingi mtu huwa nazo ni hizi
zifuatazo:

  • Homa kali,
  • Kutetemeka mwili,
  • utokwa na jasho,
  • Maumivu ya kichwa na misuli,
  • Kuhisi kichefuchefu na kutapika.

Lakini katika malaria kali inayosababishwa na kimelea hicho cha plasmodium mtu huwa na dalili zifuatazo:

 

  • Huonyesha hali ya kuchanganyikiwa,
  • Kupoteza fahamu,
  • Kuwa na upungufu mkubwa wa damu na matatizo ya kupumua.

Kwa hiyo kwa kutegemea dalili hizo tunaweza kujua iwapo mtu ameambukizwa malaria au la. Hata hivyo, ni vyema kwanza kumuona daktari baada ya kuona dalili za awali kama tulivyozitaja, ili aweze kukuandikia kipimo cha malaria.

Tutajizuia vipi na Malaria?

Kuna mambo mengi tunayoweza kuyafanya ili kuepuka kuumwa na mbu. Mbu huyo aina ya Anopheles anayesababisha ugonjwa wa malaria kwa kawaida huuma nyakati za usiku, lakini hata hivyo mbu wanaouma mchana nao wanaleta madhara mengi kwa mwanadamu, kwa hivyo nao wanapaswa kuepukwa.

Tufanye nini basi ili kujikinga na mbu?

 

Yatupasa kufanya mambo yafuatayo:

  • Vaa nguo za kuzuia (yaani mashati ya mikono mirefu na suruali pamoja na nguo ndefu zinasaidia.
  • Tuwe na tabia ya kufunga madirisha mapema kabla ya kuingia giza na tuweke nyavu kwenye madirisha ya nyumba zetu.
  • Tutumie vyandarua katika kitanda wakati wa usiku kila inapowezekana.

Njia nyingine ya kuwaepuka mbu ni kuwa na tabia ya kusafisha mazingira yanayotuzunguka, kwa kukata majani marefu, kufukia vidimbwi vya maji vinavyowavutia mbu kuzaana kwa wingi na kadhalika. Kabla sijamaliza makala hii yenye manufaa kwa kila mmoja anayeisoma, leo napenda nikufahamishe kuwa JAMES HERBAL CLINIC tuna dawa nzuri inaitwa NEOTONIC ni muhimu yenye mchanganyiko wa vyakula vya matunda na mbogamboga na mimea mbalimbali. NEOTONIC ina tangawizi kwa ndani.

Je unafahamu tangawizi ina faida gani katika mwili wa mwanadamu? Tegea sikio kwa makini mpendwa msomaji:  Wataalamu wa afya wanasema kuwa mbali ya kuwa jamii zetu zimekuwa na mazoea ya kutumia tangawizi kama kiungo katika vyakula, lakini zao hilo linafanya kazi nyingi katika mwili wa mwanadamu kama vile kuimarisha tumbo, na kusaidia uyeyushaji wa chakula tumboni. Husaidia pia katika kutibu mafua ,rheumatism, kuhara na kukosa choo au uyabisi wa choo, huondoa kichefuchefu na huzuia kutapika khususan kwa kina mama wajawazito, hupunguza maumivu ya tumbo, huondoa sumu mwilini, nk. Vile vile tangawizi ina wanga wa kutosha na haina mafuta. Aidha ina vitamini A,B1, B2, Madini ya Niacin, Sodium, Phosphorus, Potassium, Calcium, Iron au huma, Maganesium, Coper na Zinc, ambayo yote yana faida kwa miili yetu. Hivyo, naomba mpendwa uwe na amani kabisa kwamba utumiapo NEOTONIC, malaria sugu hutoweka kabisa.

Napenda kuishia ndugu msomaji, karibu sana James Herbal Clinic.

Unahitaji dawa ya NEOTONIC? Basi tupigie namba: 0752389252 au 0712181626