Tatizo la kuziba kwa mirija ya mayai ya uzazi au mirija ya kupitishia mayai ya mwanamke ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa mwanamke ambapo mwanamke anakosa uwezo wa kuzaa. Mirija inapoziba yai linashindwa kukutana na mbegu ya mwanaume na kutungisha mimba.
Matatizo ya ugumba kwa mwanamke yana vyanzo vingi lakini kuziba kwa mirija ni tatizo kubwa ambalo huathiri wanawake wengi wenye tatizo hili. Katika makala yaliyopita tuliona uchunguzi wa kuthibitisha tatizo hili, na tumekuwa tukiongelea mambo mengi sana juu ya matatizo ya mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Je, Aina Za Uzibaji Wa Mirija Ziko Ngapi?
Kwa mujibu wa utafiti ambao umeshawahi kufanyika, asimilia 20 ya matatizo ya ugumba kwa wanawake husababishwa na tatizo la mirija ya uzazi.
Mirija inaweza kuziba upande wa mwisho jirani na vifuko vya mayai ‘Distal tubal occlusion’ na hii huhusiana zaidi na hali ya kuvimba mirija ambayo tutakuja kuiona hapo baadaye na chanzo cha tatizo la mirija kuvimba husababishwa na maambukizi ya ugonjwa wa pangusa(Chlamydia Trachomatis).
Mwanamke mwenye tatizo la kuvimba mirija au mirija kujaa huwa na maumivu upande wa kulia au kushoto au pande zote mbili chini ya tumbo na hupata maumivu baada ya tendo la ndoa na huwa hashiki mimba.
Tunaposema ugumba maana yake unatafuta ujauzito ndani ya mwaka mmoja bila ya mafanikio.
Aina ya pili ya uzibaji wa mirija ya uzazi ni kushikamana hiyo mirija hali iitwayo kitaalamu ‘Pelvic adhesions.’
Tatizo hili linasababishwa na jamii hiyohiyo ya vimelea ambavyo tumeshaviona hapo awali vya maambukizi ya pangusa(Chlamydia), nayo ni magonjwa ya zinaa. Tatizo hili huwa siyo kali na mara chache mgonjwa hulalamika maumivu, na kushikamana huku ni hali ya makovu ndani na nje ya mfumo wa uzazi, upande wa vidole vinavyoshika mayai hujikunja na wakati mwingine mrija wenyewe hukamatana na viungo vingine jirani, hivyo kuzuia yai kupenya na kusafiri kwenye mrija.
Wakati mwingine katika tatizo hili pia mrija unaweza kuwa wazi na kuruhusu yai kupenya. Mirija inaweza kuziba sehemu ya kati ‘midsegment tubal osbsraction’ na hii inaweza kusababishwa na oparesheni ya kufunga kizazi.
Mirija inaweza kuziba upande wa juu karibu na mfumo wa uzazi na chanzo kikuu ni maambukizi ndani ya kizazi hasa baada ya kutoa au kuharibika mimba.
Mirija inaweza kuziba kwa bahati mbaya baada ya upasuaji wa uzazi au kuondoa uvimbe.
Je, Nini Chanzo Cha Tatizo Hili?
Chanzo cha mirija kuziba ni maambukizi ndani ya kizazi au maambukizi ya viungo vya uzazi (Pelvic Inflammatory diseases) au kwa kifupi “PID”. Ugonjwa huu wa PID siyo mzuri kwani utafiti unaonyesha kwamba asilimia 12 ya wanawake wanaopata ugumba kwa kuziba mirija wameugua ugonjwa wa PID na kutibiwa na kupona mara moja, waliougua PID zaidi ya mara tatu wana zaidi ya asilimia 53 ya kupata tatizo hili la kuziba mirija ya uzazi.
Wapendwa wanagroup akina mama nawaombeni sana unapopima na kukutwa na maambuki ya viungo vya uzazi au PID, tafadhali fanya haraka sana kupata tiba ili kuondoa tatizo hili. James Herbal Clinic tuna dawa nzuri tu za kuondoa ugonjwa wa PID kwa haraka tu.
Je, Nini Dalili Za Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi?
Dalili za ugonjwa huu wa PID huwa ni kama ifuatavyo:
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara,
- Kutokwa na uchafu ukeni aidha ukiwa na harufu au muwasho,
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa na siku za hedhi kuvurugika.
Maambukizi ndani ya tabaka la ndani la kizazi pia huchangia na dalili zake zinafanana na zile za PID. Maambukizi pia unaweza kuyapata baada ya kujifungua au endapo utakuwa na ugonjwa wa kidole tumbo. Mirija pia inaweza kukatwa siyo tu kwa kufunga uzazi lakini hata endapo mimba itatunga na kukua kwenye mrija.
Je, Mgonjwa Anapaswa Afanyeje Ili Kuondoa Ttatizo Hili?
Tatizo hili la kuziba mirija ya mayai huchunguzwa kwa kina ili kujua aina ya uzibaji na hatua za kuchukua. Vipimo kama tulivyovionyesha katika makala zilizopita, mfano
- Kipimo cha HSG ambapo dawa huingizwa katika kizazi na kupiga picha. Kipimo hiki hakizibui mrija bali kinaonyesha jinsi mrija ulivyo.
- Kipimo cha Ultrasound au ‘Sonography’ huonyesha mrija kwa nje kama una kasoro zozote, aidha umevimba au la, Laparoscopy na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa vifanyike.
Baada ya hapo tiba sahihi itafanyika kama ni kuzibua au upasuaji.
Endapo mirija itazibua na ikaziba tena, basi uwezekano wa kuizibua huwa mdogo na mshauri huwa ni upandikizaji au IVF. Ni vema uwahi katika hospitali ya mkoa uwaone madaktari wa matatizo ya uzazi kwa uchunguzi wa kina.
Tiba Yake
James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo haya ya uvimbe na kuziba kwa mirija ya uzazi, nazo ni REDEEMER, VITAMAKA na FRESH HERB. Dawa zetu hurejesha mfumo asili, na afya ya kamili ya vizazi. Hurekebisha mwili wako, na kutowesha chochote ambacho hakitakiwi kiasili, na hufufua vikinga uzee na kinga ya mwili na kukuepusha na magonjwa yote ikiwemo PID na mengineyo.
Je, unahitaji huduma? Tupigie 0752389252 au 0712181626